Skip to main content

VIONGOZI WA 'ACT' KIZUIZINI UWANJA WA NDEGE ANGOLA

Mwenyekiti wa Chama cha ACT-Wazalendo, Othman Masoud Othman na Mwenyekiti wa Chadema Tundu Lissu wanadaiwa kuzuiwa kuingia nchini Angola kushiriki mazungumzo ya Jukwaa la Demokrasia Afrika (PAD). 



Othman, ambaye pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar kwenye msafara wake ameambatana na Kiongozi wa ACT-Wazalendo, Dorothy Semu, Waziri Kivuli wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Dk Nasra Nassor Omar na maofisa wengine wa chama hicho.


Makamu Mwenyekiti wa ACT Wazalendo-Zanzibar, Ismail Jussa ameliambia Mwananchi leo Alhamisi Machi 13, 2025 kuwa Othman na msafara wake wamezuiwa kwenye Uwanja wa Ndege wa Luanda jijini Angola.

 

Tayari ACT Wazalendo imetoa taarifa ya kulaani tukio hilo ililoliita la udhalilishaji wa kiongozi huyo huku kamati yake ya uongozi ikikutana kwa dharura kujadili suala hilo, ambalo mamlaka za Angola hazijajitokeza kulizungumzia.


Wakati huohuo, Lissu ameandika kwenye ukurasa wake wa X kuwa mamlaka za uhamiaji za Angola zimewazuia na kukataa kuwaruhusu kuingia nchini humo, yeye pamoja na ujumbe wa zaidi ya viongozi wakuu 20 na wawakilishi wa vyama vya siasa kutoka Kusini mwa Afrika, ambao tuliwasili Luanda mapema leo kwa ajili ya mkutano huo wa siku mbili.


“Kundi hili linajumuisha Makamu wa Kwanza wa Rais wa sasa kutoka Tanzania (Othman) , Rais wa zamani wa Botswana, Waziri Mkuu wa zamani wa Lesotho, pamoja na viongozi na wajumbe waandamizi kutoka Kenya, Sudan, Tanzania, Afrika Kusini, Namibia, Eswatini, Lesotho, Ujerumani, Marekani, Uganda, DRC, na Msumbiji,” Lissu ameeleza katika andiko hilo.


“Waangola na Watanzania ni ndugu wa damu. Tanzania ilimkaribisha Dk Antonio Agostinho Neto na wapiganaji wa MPLA katika miaka ya mwanzo ya harakati zao za uhuru. Tuliisaidia Angola kwa hali na mali wakati wa uvamizi wa kikoloni wa utawala wa kibaguzi wa Afrika Kusini katika Kusini mwa Angola katika miaka ya 1970 na 1980.


#mwananchiupdates 

#tunaliwezeshataifa

Comments

Popular posts from this blog

MWANAMKE AJINYONGA, SABABU WASI WASI - PEMBA

NA, HASSAN MSELLEM - PEMBA PICHA KUTOKA MAKTABA Mwanamke aliyefahamika kwa jina la Raya Darusi Abdallla miaka 48, mkaazi wa Mbuzini Wilaya ya Chake Chake Mkoa wa Kusini Pemba, amefariki Dunia kwa kidaiwa kujinyonga kutokana na Msongo wa mawazo. Tukio Hilo limetokea Novemba 30.2025 saa 11 alfajiri huko Mbuzini Wilaya ya Chake Chake Mkoa wa Kusini Pemba. Omar Salum Ali, ambaye ni shemeji wa marehemu amesema kabla ya marehemu alikuwa na sumbuliwa na Msongo wa mawazo kutokana na kumpoteza kaka yake ambaye alifariki hivi karibuni, kugundulika kuwa ana maradhi ya sukari, mtoto wake wa kiume wa miaka 25, kuwa na ugonjwa akili hali iliyopelekea kupatwa na Msongo wa mawazo na kuamua kujinyonga. Katibu wa Sheha (Katibu wa Mwenyekiti) Shehia ya Mbuzini Yakub Ali Msabah, amesema alipata taarifa za tukio Hilo kutoka kwa Sheha wa Mbuzini kuhusu tukio baada ya kufika eneo la tukio waliukuta mwili wa Mama huyo ukiwa unanin'gia kwenye dari ya Nyumba ambayo alikuwa anaishi zamani. Kutoka tarehe 18 ...

Mariam Muhene – mfano wa kuigwa kwa wanawake kwenye ulingo wa siasa ni

MAKALA NA, HASSAN MSELLEM -PEMBA Tangu Tanzania iruhusu mfumo wa vyama vingi mwaka 1992, Mariam Muhene alijiunga na chama cha Civic United Front (CUF) ambapo mwaka 1995, aligombea nafasi ubunge wa viti maalumu na kuvuka hatua zote ikiwemo kula kiapo mahkamani lakini hakufanikiwa kukikalia kiti hicho. “Mwaka 1995 niligombea ubunge wa viti maalum na nikapita kila kipengele mtu wa kwanza wilaya, taifa bodi ya uongozi, nikala kiapo mahkmanai lakini katika nafasi mbili zilizoletwa kwa kila mkoa Kusini na Kaskazini Pemba mimi sikubahatika” amesema  Safari yake ya kisiasa za upinzani iliendelea na mnamo mwaka 2000, aligombea nafasi ya ubunge wa kuchahguliwa kupitia chama cha Allience for Democratic Change (ADC) Jimbo la Chake Chake lakini kutokana na changamoto zilizojitokeza ikiwe mawakala wa Chama chake kutokuruhisiwa kuingia kwenye vya kupiga kura jambo ambalo amesema lilichangia kukosa nafasi hiyo. Kwasasa Mariam Mohammed Muhene anashika nafasi ya Kamishna wa ADC kanda ya Pemba, nafas...

WATOTO KUJINYONGA ZANZIBAR, UTAFITI WAHITAJIKA.

HABARI NA, HASSAN MSELLEM, PEMBA Picha kutoka mtandaoni Visa vya watoto kujinyonga vimeanza kuwatia khofu na mashaka wazazi na walezi katika Visiwa vya Unguja na Pemba. Mashaka na khofu hiyo imeibuka baada ya matukio mawili mfululizo ya watoto wawili mmoja akiwa umri wa miaka (5) na mwengine (9) kuripotiwa kufariki dunia kwa kujinyonga kati ya tarehe 7 na 9 mwezi huu wa kumi mwaka 2025 kupitia kipindi cha Mawio kinachorushwa na Shirika la Utangazaji Zanzibar ZBC kila siku kuanzia saa 12:40 asubuhi. Katika tukio la kwanza mnamo tarehe 7.10.2025 mwandishi Masanja Mabula aliripoti tukio la Fatma Omar Kidere mwenye umri wa miaka tisa (9) mkaazi wa Mtondoo Jeuri Makaangale Wilaya ya Micheweni Mkao wa Kaskazini Pemba, amekutwa amefariki dunia na mwili wake ukiwa unanin’ginia kwa kutumia mtandio Jirani wa marehemu aliyefahamika kwa jina la Khamis Ali, amesema amepata taarifa za tukio hilo akiwa kazini baada ya kupigiwa simu na mke wake kumpa taarifa za kutokea kwa tukio hilo na kuondoka kazin...