Skip to main content

Posts

PENYE NIA PANA NJIA: SAFARI YA KISIASA YA ZULEKHA ALI JUMA.

Na, Fatma Muhammed Suleiman, Unguja  Zulekha Ali Juma ni mama mwenye maono na dhamira ya kweli ya kutimiza ndoto zake. Alizaliwa mwaka 1971 visiwani Zanzibar, na safari yake ya elimu ilianza mwaka 1980 katika Skuli ya Haile Salasi Zanzibar, ambako alisoma darasa la kwanza hadi la nne. Aliendelea na masomo katika Skuli ya Konde, Micheweni Pemba, hadi kidato cha kwanza. Bi Zulekha alipendelea zaidi somo la siasa kwa sababu alikuwa na ndoto ya kuwa mwanasiasa, alipenda somo la historia na kujua asili ya nchi yake na maendeleo , na jiografia kwa shauku ya kutembelea maeneo mbalimbali. Akiwa skuli alikuwa kiongozi wa darasa ambapo pia alishiriki michezo mbalimbali. Alichagukliwa kuwa mwenyekiti wa chipukizi wa skuli na hatimae mwenyekiti wa chipukizi Mkoa wa Kaskazini Pemba. Ingawa alishindwa kuendelea na masomo kutokana na changamoto zilizo nje ya uwezo wake, hakukata tamaa ya kutimiza malengo yake. Ndoto yake ilitimia rasmi mwaka 1993 alipojiunga na chama cha CUF ambapo alipata nafa...

RAHIMA SAID ABDALLAH: MWANAMKE JASIRI ANAYEVUNJA VIKWAZO VYA UONGOZI.

Makala Na Fatma M. Suleiman, Unguja “Sijatokea kwenye familia yenye uzoefu wa kisiasa, nimepata hamasa kuionyesha jamii mwanamke anaweza kuwa kiongozi na kutatua changamoto za jamii Mwanamke ni mlezi, mbunifu na mwenye fikra pevu, kwa hiyo hakuna sababu ya kunizuia kuingia kwenye uongozi wa kisiasa.”  Kauli hii inaakisi Taarifa ya Baraza la Taifa la Wanawake, Tanzania, 2023 inayoeleza kwamba “Kuhakikisha usawa wa kijinsia katika uongozi si chaguo, bali ni wajibu wa kijamii.”  Rahima Said Abdallah ni mfano wa mwanamke jasiri aliyevunja vikwazo vya kijamii na kugombea nafasi ya uwakilishi kupitia Chama cha Ukombozi wa umma (CHAUMMA) Jimbo la Mwanakwerekwe katika Uchaguzi Mkuu wa 2025. Rahima ana miaka 26 amethibitisha kuwa uongozi haujali jinsia, bali ni uwezo, bidii na dhamira ya kweli ya kuwatumikia watu. Kupitia safari yake, amekuwa kielelezo cha matumaini mapya kwa wanawake na vijana wanaotamani kushiriki katika uongozi wa kisiasa nchini. Rahima alizaliwa mwaka 1...

Elimu ya Uongozi Nguzo Muhimu kwa Mwanamke Katika Uongozi

 Makala Na  Fatma M. Suleiman Mitazamo kuhusu nafasi ya mwanamke katika uongozi imeendelea kubadilika taratibu. Wapo wanaoamini kwamba mila na desturi haziruhusu mwanamke kuwa kiongozi, wengine wanaona hakuna pingamizi la kimaadili wala kidini linalozuia mwanamke kushika nafasi za juu za maamuzi.  Bikame Sheha Ussi, Mkuu wa Divisheni ya Pensheni Jamii na Maendeleo ya Wazee, anabainisha kuwa historia za dini pia zinaonyesha wazi kwamba wanawake hawajazuiwa kuwa viongozi.   “Kwa upande wa Dini ya kiislamu haijakataza mwanamke kuwa kiongozi, bali inasisitiza kuzingatia mipaka na maadili.” Anaongeza kuwa, mfano wa Bi Khadija (R.A.), mke wa Mtume Muhammad (s.a.w.), ni kielelezo cha mwanamke aliyekuwa kiongozi wa kiuchumi na kijamii katika zama zake. Ni Dhahiri, uwezo wa mwanamke kuhudumia familia na mifano ya wanawake walioleta mabadiliko katika jamii kitaifa na kimataifa ni chachu ya kubomoa mitazamo hasi na mawazo mgando hususan katika zama hizi.  Mkurugenz...

Mwezi mmoja matukio 106, ya Ukatili na Udhalilishaji Zanzibar, Magharabi ‘B’ yaongoza.

Na, Hassan Msellem, Pemba Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali Zanzibar (OCGS) imetoa takwimu za matukio ya ukatili na udhalilishaji wa kijinsia Zanzibar katoka mwezi Agosti na Septemba 2025, ambapo jumla ya matukio 106 ya ukatili na udhalilishaji wa kijinsia yameripotiwa katika vituo mbali mbali vya Polisi huku Wilaya ya Magharib ‘B’ Unguja kwa kuwa jumla ya matukio 17 sawa na asilimia 16.0 Akitoa takwimu hizo kwa waandishi wa Habari, waratibu wa madawati ya jinsia na wadau wengine Oktoba 22.2025 huko Gombani Pemba Mkurugenzi wa Idara ya Takwimu za Kijamii kutoka Ofisi ya mtakwimu Mkuu Zanzibar Sabina Raphael Daima, amesema jumla ya matukio ya ukatili na udhalilishaji wa kijinsia 106 yameripotiwa mwezi Septemba 2025, ambapo waathirika wakubwa wakiwa ni watoto sawa asilimia 88.7 na wanawake wakiwa asilimia 11. 3 Aidha amesema kuwa miongoni mwa waathrika wa matukio hayo 94, wasichana 82 sawa asilimia 77.4 wavulana 12 sawa na asilimia 10.3 “Takwimu hizi zinaonesha matukio ya ukatili na udh...

JELA MIAKA 106, KWA MAKOSA NANE YA UDHALILISHAJI.

HASSAN MSELLEM, PEMBA Abdalla Rashid Hassan (Mgunya) mwenye umri wa miaka 30 mkaazi wa Ziwani Wilaya ya Chake Chake Mkoa wa Kusini Pemba amehukumiwa kwenda chuo cha mafunzo (JELA) kwa muda wa miaka 30 kwa Kutenda makosa nane ya udhalilishaji yakiwemo ya kutorosha, shambulio la aibu na kubaka. MAKOSA MATANO YA KUTOROSHA Mbele ya hakimu wa mahakama ya kupambana na makosa ya udhalilishaji Mkoa wa Kusini Pemba Chake Chake Taki Abdalla Habib imeelezwa na mwendesha mashtaka Othman Mzori kuwa tarehe 3\01\2025 saa 8:30 za mchana huko bonde la Mjananza Ziwani Wilaya ya Chake Chake Mkoa wa Kusini Pemba mshtakiwa aliwachukua watoto watano wenye umri kati ya miaka 7, 9, 11, 12 na kuwapeleka maporini katika bonde la Sinanga Ziwani, jambo ambalo ni kosa kisheria kinyume na kifungu cha 113 kifungu kidogo cha kwanza (a) Sheria nambari 6 ya mwaka 2018 Sheria ya Zanzibar. KOSA LA SITA Shambulio la kawaida Tarehe 3\01\2025 saa 9:25 za jioni huko Sininga Ziwani Wilaya ya Chakwe Chake Mkoa wa Kusini Pemba ...

WANAWAKE WENYE ULEMAVU WAOMBA PUNGUZO LA FOMU ZA KUGOMBEA

Makala Na, Hassan Msellem  Katika uzinduzi wa programu ya kuinua haki za watu wenye ulemavu ya CADir (Collective Action for Disability Rights) katika kutatua changamoto za watu wenye ulemavu, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imetaja hatua inayochukua katika kuimarisha ushiriki wao katika ngazi za uamuzi kutoka asilimia 2% hadi 5% ifikapo mwaka 20230. Utambuzi wa watu wenye ulemavu katika azimio la Arusha la mwaka 1967, kuwa miongoni mwa makundi machache yanastahili usaidizi kutoka kila sekta ikiwemo jamii, elimu, ajira na Uongozi ili kuhuisha haki na ustawi wa watu wenye ulemavu nchini. Wanawake wenye Ulemavu kupitia vyama mbali mbali vya siasa wameomba kupunguziwa kiasi cha kulipia fomu za kugombea nafasi za uongozi ili waweze kushiriki katika haki hiyo. Wakizungumza na Pemba Post Blog kwa nyakati tofauti baadhi ya wanawake wenye ulemavu wamesema gharama za fomu za kugombea nafasi za kisiasa kama vile Uwakilishi, Ubunge na Uraisi ni kubwa hali inayochangia baadhi yao kushindwa kuhim...

WAANDISHI WA HABARI VIJANA ZANZIBAR 'WASUKWA' KUZITAMBUA HABARI ZA UONGO.

NA, HASSAN MSELLEM – PEMBA Waandishi wahabari wachanga Visiwani Zanzibar wamepatiwa mafunzo ya kutambua taarifa sahihi katika kuelekea Uchanguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika mwezi Oktoba 29. 2025. Akifungua mafunzo hayo kwa waandishi vijana kutoka Unguja na Pemba Mkurugenzi kutoka Muungano wa Klabu ya Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC) Kenneth Simbaya katika Ukumbi wa Kituo cha Huduma za Sheria Kijangwani Mjini Unguja, amesema lengo la mafunzo hayo ni kuwandaa Waandishi Habari vijana kutekeleza majukumu ya kihabari kwa weledi katika Dunia ya sasa yaliyotawaliwa na matumzi mabaya ya ‘AKILI UNDE’  Aidha Mkurugenzi huyo amewasisitiza waandishi hao umuhimu wa kujifunza matumizi sahihi ya ‘AKILI UNDE’ katika kuhakikisha taarifa zinazosambazwa mitandaoni kuelewa usahihi wake. “Ngudu waandishi kama munavyofahamu kuwa katika dunia ya leo tumegubikwa na matumizi mazuri na mabaya Artificial Intelligence (AKILI UNDE) hivyo lengo la mafunzo haya kwenu ni kuona ni kwa namna gani mutaweza kutamb...