Skip to main content

Posts

Maumivu ya kukosa sheria mpya ya habari Zanzibar.

Na, Thuwaiba Habibu Raha na furaha ya safari ni kufika ulikokusudia kwa salama na amani. Baadhi ya safari huwa ngumi na huwa zenye maumivu na athari nyingi Miogoni mwa safari hizi ni ya waandishi wa habari kutaka kuwa na sheria zenye mazingira bora ya kazi zao. Kwa Takribani miaka 20 sasa waandishi na wadau wengine wa habari wamekuwa wakionyesha vifungu vya sheria ya habri vinavyominya uhuru wa habari na wa kujieleza. Lengo ni kutaka sheria rafiki itakayofanya mazingira ya kukusanya na kutoa habari Zanzibar kuwa rafiki na kuweza kuchangia vizuri maendeleo ya visiwa vya Unguja na Pemba. Lakini kelele hizo zimekuwa kama zile za msemo maarufu wa Kiswahili wa kelele za mpangaji hazimzuwii mwenye nyumba kulala. Zanzibar ilikuwa na historia nzuri na ya kuvutia ya habari na vijana wake kuchangia maendeleo ya sekta ya habri, hasa ya kufungua idhaa za Kiswahili katika nchi mbali mbali duniani. Kutoka zama hizo na hadi leo visiwa hivi vimetoa manguli wa taaluma ya habari kwa nyakati mbali mbal...

Kichanga chafariki kwa kukosa huduma ya OXYGEN Hospitali ya Chake Chake.

  Taarifa na Mwandishi Wetu. Inadaiwa taarifa za kichanga hicho kufariki dunia zilisambaa jana April 28, 2024 baada ya mama anayefahamika kwa jina la Saumu Hamduni Juma Mkaazi wa Michungwani Wilaya ya Chake Chake Mkoa wa Kusini Pemba, kujifungua watoto mapacha akiwa na ujauzito wa miezi sita katika hospitali ya Chake Chake na kusababisha hali za vichanga hivyo kuhitaji huduma ya dharura ya oksijini, ambayo ilikosekana katika hospitali hiyo.   Kwa mujibu wa Afisa Ustawi wa Wilaya ya Chake Chake, Afisa Ustawi wa Wilaya, Afisa Afya wa Wilaya ya Chake Chake Abdalla Haji Ali na Daktari Dhama wa Wilaya ya Chake Chake  (DMO) Sharif  Hamad Khatib a mbao walinukuliwa na afisa watu wenye ulemavu Wilaya ya Chake Chake Mwadini Juma  Ali alisema   “Nikweli jana majira ya mchana alifikishwa mama mjamzito katika Hospital ya Chake Chake na hatimaye kujifungua watoto wawili pacha ila mama huyo alijifungua akiwa bado muda wa kujifungua kitaalamu kufika ambapo ni mie...

Uzembe wa madereva wasababisha vifo vya watu 2 katika ajali mbili tofauti Pemba.

  Habari Na, Hassan Msellem-Pemba. Hassan Ali Hassan miaka 20, amefariki dunia baada ya gari aliokuwa amepanda aina ya Hino Lorry yenye namba ya usajili Z 572 ES iliokuwa ikiendeshwa na Ali Juma Hassan miaka 35, mkaazi wa Vitongoji kupata ajali katika eneo la Meli tano Wilaya ya Chake Chake Mkoa wa Kusini Pemba. Akizungumza na Bahari fm Radio Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kusini Pemba Richard Mchomvu, alisema majira ya saa 8 mchana wakati gari hiyo ikitokea maeneo ya Ole kuelekea Ziwani ikiwa imebeba watu sita (6) ilipofika eneo la Meli Tano kutokana na mwendo kasi iliacha njia na kuelekea mabondeni kitendo kilichopelekea mtu mmoja kufariki dunia papo hapo na wengine wa tano kujeruhiwa. Aidha Kamanda Mchomvu aliwataja majeruhi hao kuwa ni Iddi Omar Mgunya mwenye umri wa miaka 35, mkaazi wa Vitongoji, Said Ali Said miaka 25, mshirazi wa Vitongoji, Khamis Ali Shaaban miaka 19 mkaazi wa Vitongoji, Nassor Said Khamis miaka15 mkaazi wa Vitongoji ambapo wamelekwa hospitali kwa ajili matibabu...

Jeshi la Polisi Mkoa wa Kusini Pemba likusanya Shillingi laki saba na eflu tisini na tano kutokana na faini za makosa ya usalama barabarani.

Habari Na, Hassan Msellem, Pemba Jeshi la Polisi Mkoa wa Kusini Pemba limekusanya Shillingi laki Saba na elfu tisini na tano kutoka tarehe 24\02\2022 hadi March 02\2022 kutokana na operesheni ya ukaguzi wa vyombo vya maringi mawili na Matatu yani Pikipiki na Bajaji ambapo Kwa kipindi hicho takriban vyombo 105 vilikamatwa Kwa makosa mbali mbali ikiwemo Madereva kutokuwa na leseni, uzembe, vyombo kukosa pasi nakadhalika ambapo Madereva 60 walifikishwa mahakamani na kutozwa faini. Hayo yamesemwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kusini Pemba Kamishna msaidizi wa Polisi Richard Tadeo Mchomvu wakati akizungumza na Waandishi wa Habari huko Ofisini kwake Madungu Chake Chake. Aidha Kamanda Richard ametoa wito waendeshaji wa vyombo vya Moto hususan madereva Bodaboda kuwa Makini na kufuata Sheria za Usalama Barabarani ili kuepukana na Ajali zisizo za lazima.

Mmoja afariki na wengine 30, wajeruhiwa vibaya kwa ajali ya gari Mbuzini Pemba.

Habari Na, Zuwena Shaabani Pemba Mtu mmoja amefariki dunia na wengine zaidi ya 30 wamejeruhiwa katika Ajali aliyohusisha gari ya abiria aina Dyna ruti Nambari 602 yenye namba za usajili EK 189 na vyombo vya maringi mawili aina ya Vespa katika Eneo la Mbuzini Wilaya ya Chake Chake Mkoa wa Kusini Pemba. Wakizungumzia ajali hiyo mashuhuda walisema, walishuhudia kugongana kwa gari hizo baada ya kusikia mshindo mkubwa ambao ulipelekea mtu mmoja kupoteza maisha na wengine kujeruhiwa vibaya. Akithibitisha kutokea kwa ajali hiyo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kusini Pemba Richard Tadeo Mchomvu alisema ajali hiyo ilitokana na kugongana uso kwa uso kati ya gari aina ya Dayna na ya mizigo Fuso na kupelekea gari hiyo iliyokuwa na abiria zaidi ya 30 kupinduka.

Kijana wa Miaka 20 agongwa na Gari akiwa anaendesha Vespa na kufariki Dunia.

  Na, Hassan Msellem, Pemba Kijana Mbarouk Salum Mbarouk 20, Mkaazi wa Kipapo Shehia ya Chonga Wilaya ya Chake Chake Mkoa wa Kusini Pemba, amefariki baada ya kupata Ajali ya kugongwa na Gari akiwa anaendesha chombo Cha maringi mawili aina ya Vespa katika Eneo la Kipapo Pemba. Tukio Hilo limetokea March 24 Majira ya saa 7 za Mchana Huko katika Eneo la Kipapo Shehia ya Chonga Mkoa wa Kusini Pemba. Akikiri kupokea mwili wa Marehemu huyo Daktari Dhamana wa Hospital ya Chake Chake Abraham Said Msellem, amesema March 24 Majira ya saa 8:30 za Mchana amepokea Kijana anaekadiriwa kuwa na Miaka 20 ambaye alipata Ajali ya kugongwa na Gari na kuumia maeneo mbali mbali ya mwili wake ikiwemo mbele ya fuvu la kichwa mkono wa kulia. Aidha amesema uchunguzi wa awali unaonesha kuwa Marehemu alipata majeraha makubwa katika Eneo la fuvu la kichwa jambo ambalo lilisababisha kuvuja Kwa damu na kupotezea Maisha punde wakati akifanyiwa matibabu. Ili kupata ufafanuzi juu ya ajali hiyo Mwandishi wa Habari h...

Tutasubiri upatikanaji wa sheria mpya za Habari Zanzibar mpaka lini? - Wadau

  ADAU wa vyombo vya habari wameiomba serikali ya Mapinduzi Zanzibar kukamilisha mchakato wa marekebisho ya sheria za habari zilizotolewa maoni na wadau ili  kutoa mazingira rafiki kwa waandishi wa habari kutekeleza majukumu yao bila vikwazo.   Imeelezwa kwa muda mrefu licha ya wadau mbalimbali kutoa na kuwasilisha mapendekezo yao kuhusu mapungufu yaliyopo kwenye baadhi ya sheria hizo, lakini utekelezaji wake bado umekuwa wa kusuasua jambo linalopelekea mazingira magumu ya utendaji kazi wa vyombo vya habari nchini.   Mkurugenzi wa Chama cha Waandishi wa Habari Tanzania, Zanzibar (TAMWA ZNZ), Dkt. Mzuri Issa alieleza mchakato wa mabadiliko ya sheria za habari umekuwepo kwa miaka mingi lakini bado sheria hizo ambazo nyingi ni za muda mrefu zimekwama kurekebishwa.   "Sisi wengine tangu tuko waandishi chipukizi tunazungumzia kupata hizi sheria mpya za habari, tangu 2008 kwa kweli ni muda mrefu, tunahitaji kusimamia jambo hili kwa umoja wetu na hatimae tupate sheria ...