Skip to main content

Posts

Wanaume wajitoa kuhakikisha wanawake wanakuwa juu kiuchumi na uongozi.

Na, Thuwaiba Habibu. Mwalimu wa vikundi vya kueka na kukopa kutoka Umbuji kheri Omari amewataka wanawake kutumia vikundi kujifunza uongozi pamoja na kujikwamua kiuchumi. Amesema hayo wakati akizungumza na muandishi wa habari hizi huko umbuji wilaya ya kati mkoa wa kusini unguja amesema ndani ya vikundi ni rahisi kwa wanawake kuweza kujifunza uongozi kwasababu vikundi ni wanawake watupu na kuna nafasi mbali mbali za kuwajengea uzoefu. "kuna nafasi za mwenyekiti , makatibu na washika hazina hivyo basi nafasi hizi wakizitekeleza kiuwadilifu ikitokea nafasi ya uongozi wa juu inakuwa ni wepesi kwa mtu kugombea na kutekeleza majukumu yao kiusahihi. Pia alisema najitahidi kuwamasisha wanawake kuwa imara katika shughuli za vikundi na uongozi kwani watajikwamua kiuchumi na kuleta maendeleo katika nchi zetu. Huu sio muda tena wa mwanamke kusubiri kulitewa na kuongozwa tu bali wanawake watakiwa wapambane kutafuta ila kwa utaratibu mzuri. Kwa upande wake katibu wa kikundi cha wanawake ...

Wanaume watoe ruhusa kwa wanawake kuingia katika uongozi.

Na, Thuwaiba Habibu. Sheha wa michamvi Khadija hassani haji amewaomba wanaume watoe ruhusa kwa wanawake kushiriki katika uongozi. Ameyasema hayo wakati alipokuwa akizungumza na muandishi wa habari hizi huko michamvi mkoa wa kusini Unguja amesema wanaume waache tabia ya kutowapa uhuru wake zao katika kugombania nafasi za uongozi. Alisema baadhi ya wanaume wanapoowa wanatumia mamlaka hiyo kuwazuia kushiriki katika shughuli mbali mbali ikiwemo suala la uongozi kufanya hivyo kuna wakosesha fursa muhimu wanawake. Nae katibu wa kikundi cha kaya maskini shehiya ya michamvi Zawadi Sudi Ame alisema lazima iandalie kampeni ndani ya vikundi vya ushirika kuhamasisha wanawake kugombea nafasi hizo. Alisema wanawake wengi hujihusisha na vikundi vya ushirika huku vijijini kwenye sehemu hizo ndiko kunako hitajika kampeni na hamasa ya nguvu kuhakikisha wanawake wanagombania nafasi za uongozi ifikapo mwaka 2025 ili kupigania maendeleo ya taifa. Nao mwanakijiji wa michamvi wamesema wanawake...

Wanawake watakiwa kuacha uoga kugombea nafasi za Uongozi.

 Na, Thuwaiba Habibu. Muanzilishi wa kike vikundi vya ushirika kutoka mkoa wa kusini bi lela Hamadi Makame amewataka wanawake kugombea nafasi za uongozi kwani wao ndio watatuzi wakubwa wa shida za wanawake wenzao. Ameyasema hayo wakati akitoa mafunzo katika kikundi cha ushirika kiitwacho "hizo ndio fikra zenu"huko koani wilaya ya kati mkoa wa kusuni unguja amesema kuna wanawake wanakabiliwa na matatizo mengi ndani ya jamii yetu na wanashindwa pakuyapeleka na kubakia yakiwathiri wao na vizazi vyao. Alisema kabla ya kuwa kuanzisha vikundi hivi na kupata nafasi hii ya uongozi nilikuwa mama wa nyumbani tu lakini kitu kilicho nisukuma ni kuona wanawake wanadhalilika hasa wale ambao wameachwa na waume zao na kufikia hatua ya ya kutumia miili yao ili waweze kukidhi haja zao na watoto wake. "Inafika wakati mwanamke anachuma mali na mume wake lakini wakiachana anamfukuza na kumuachia watoto ambao hajuwi hata awapeleke wapi" Aidha alisema hakuna mwanamke hata mmoja ...

Katibu wa Siasa Itikadi na Uenezi Kijitoupele awaasa Vijana wa kike kugombea nafasi za ngazi ya juu ya Uongozi.

 Na, Thuwaiba habibu Katibu wa Siasa Itikadi na Uenezi katika Wadi ya Kijitoupele, Riziki Abdallah Ali, ambaye alikuwa Spika mstaafu wa Bunge wa serikali ya wanafunzi ya Chuo Kikuu Cha Zanzibar (ZU) aliwaasa vijna wa kike kuacha fikra potofu linapokuja suala na kuomba nafasi za ngazi ya juu ya uongozi. Ameyasema hayo wakati akiwa na wanachama wenzake huko katika wadi ya kijitoupele amesema bado vijana wana fikra potofu ya kuwa uongozi wa ngazi ya juu ni wa watu wazima tu na wao bado wanashikilia nafasi ndogo za ndani ya matawi hali ya kuwa uwezo wa kushika nyadhifa kubwa wanao. Alisema vijana wengi wapo na mtazamo kuwa hawaruhusiwi kugombea nafasi ndani ya chama kwani wanajuwa wameshawekewa Umoja wa vijana (UVCCM) jambo ambalo sio sahihi. Aidha alisema kuna hitajika elimu kwa vijana katika sehemu tofatuti kuachana na mitazamo isiyofaa na kuanza kuhakikisha wanajitokeza kwa wingi kugombea nafasi tofauti. Sambamba na hayo alisema wanashukuru kuona japo hakuna wingi wa vija...

HUDUMA ZA KIJAMII NI KIKWAZO KWA WANAWAKE KUSHIRIKI KATIKA NAFASI ZA UONGOZI.

 Habari Na,  Ahmed Abdulla. LICHA ya elimu inayitolewa kwa jamii juu ya ushiriki wa wanawake katika nafasi za uongozi, lakini bado baadhi yao wanashindwa kujitokeza katika kuwania nafasi hizo kutokana na ukosefu wa huduma mbalimbali za kijamii. Hayo yalibainishwa na wahamasishaji jamii (CBs) katika ripoti za mikutano ya kijamii na kupata muongozo wa wawezeshaji walizoziwasilisha katika kikao kilichofanyika katika ukumbi wa skuli ya Jangombe. Walisema miongoni mwa huduma hizo zinazokosekana ambazo zinawafanya baadhi ya wanawake washindwe kugombea nafasi za uongozi ni pamoja na ukosefu wa maji  safi na salama, vitambulisho vya mzanzibar, vyeti vya kuzaliwa, miundombinu ya barabara za ndani na mambo mengine. Walisema hali hiyo inawasababisha wanawake hao kutumia muda mwingi kutafuta huduma hizo na kushindwa kwenda kujishurikisha katika harakati za uongozi na kujitafutia maendeleo mengine ya kuinua uchumi wao. Mhamasishaji jamii kutoka wilaya ya kati Bahati Issa Suleiman alis...

Ukosefu wa timu, wakatisha ndoto za kuwa mchezaji Bora wa mpira wa miguu.

Makala Na, Hassan Msellem, Pemba  Mchezo wa mpira wa miguu kwa wanawake Visiwani Zanzibar ni miongoni mwa mchezo unaoangaliwa kwa jicho tofauti na wazanzibari wengi kwa kile kinachoaminika kuwa ni ukiukwaji wa mila, silka na utamaduni wa Zanzibar kwa miaka mingi, hali iliyolekea Zanzibar kuwa idadi Ndogo ya timu za mpira za Wanawake. Ingawa tafiti zinaonesha kuwa wapo wanawake wengi visiwani Zanzibar ambao wana uwezo na shauku ya kucheza mpira wa miguu ikiwa ni sehemu ya kuonesha uwezo na umahiri wao katika mchezo huo. Riziki mwenye umri wa miaka 17, anayeishi Mkoani Kusini mwa Kisiwa cha Pemba ni miongoni mwa wasichana Kisiwani Pemba ambao wana uwezo mzuri wakucheza mpira wa miguu kiasi ya kutokumtofautisha na mwanamme pindi anapokuwa uwanjani. Kipaji cha Riziki kiligundulika tangu akiwa na umri wa miaka kumi kwani alikuwa akipenda sana kucheza mpira wa miguu na watoto wa kiume pindi wanapocheza mchezo huo kwenye chochoro za mitaani na hata muda wa mapunziko wakati akiwa s...

RUSHWA YA NGONO YATAJWA KUWA NI KIKWAZO KWA WANAWAKE, KUFIKIA NDOTO ZAO ZAKUWA VIONGOZI.

 Na,  Ahmed Abdalla, Zanzibar. WANAWAKE nchini wametakiwa kuhamasishana kuepuka vishawishi vya rushwa ya ngono ili kuwa imara na jasiri wanapotaka kugombea nafasi za uongozi. Kauli hiyo imetolewa na Ofisa uhusiano kutoka Mamlaka ya kuzuia rushwa na uhujumu uchumi Zanzibar (ZAECA), Mwanaidi Suleiman Ali alipokuwa akiwasilisha mada kuhusu nafasi ya mwanamke katika kupambana na rushwa ya ngono katika uchaguzi, katika mafunzo kwa wagombea watarajiwa yaliyofanyika ofisi za TAMWA Zanzibar Tunguu Wilaya ya Kati Unguja. Alisema ana imani kwamba wanawake wengi wanaweza kupambana na rushwa ya ngono hivyo ni vyema kuhamasishana ili kuona kila mmoja anakuwa imara na anaweza kukabiliana na hali hiyo. Ofisa huyo alifahamisha kuwa wapo baadhi ya wanaume huutumia mwanya huo ili kuwakatisha moyo na kurudisha nyuma jitihada zao hivyo ni vyema kukitokezea kitu kama hicho kujitathmini na kuwaimara katika kukabiliana nayo kwa maslahi yao na taifa kwa ujumla. Uzoefu unaonesha kwamba wanawake waathi...