Skip to main content

Katibu wa Siasa Itikadi na Uenezi Kijitoupele awaasa Vijana wa kike kugombea nafasi za ngazi ya juu ya Uongozi.

 Na, Thuwaiba habibu

Katibu wa Siasa Itikadi na Uenezi katika Wadi ya Kijitoupele, Riziki Abdallah Ali, ambaye alikuwa Spika mstaafu wa Bunge wa serikali ya wanafunzi ya Chuo Kikuu Cha Zanzibar (ZU) aliwaasa vijna wa kike kuacha fikra potofu linapokuja suala na kuomba nafasi za ngazi ya juu ya uongozi.


Ameyasema hayo wakati akiwa na wanachama wenzake huko katika wadi ya kijitoupele amesema bado vijana wana fikra potofu ya kuwa uongozi wa ngazi ya juu ni wa watu wazima tu na wao bado wanashikilia nafasi ndogo za ndani ya matawi hali ya kuwa uwezo wa kushika nyadhifa kubwa wanao.


Alisema vijana wengi wapo na mtazamo kuwa hawaruhusiwi kugombea nafasi ndani ya chama kwani wanajuwa wameshawekewa Umoja wa vijana (UVCCM) jambo ambalo sio sahihi.


Aidha alisema kuna hitajika elimu kwa vijana katika sehemu tofatuti kuachana na mitazamo isiyofaa na kuanza kuhakikisha wanajitokeza kwa wingi kugombea nafasi tofauti.


Sambamba na hayo alisema wanashukuru kuona japo hakuna wingi wa vijana wa kike waliojitokeza kugombea nafasi kubwa katika siasa ila wapo ambao wamesubutu kuonesha kuwa jambo hilo linawezekana endapo watalipa kipaombele.


Nae katibu wa Uvccm wa tawi la kwarara Abuu salehe abuu amesema wanajitahidi kutoa nafasi mbali mbali ndani ya majimbo na hata wadi kwa vijana wa kike ili kuwapa hamasa ya kushika nyadhifa kubwa.


Aidha alisema kila mwanamke anatakiwa ajitadhimini na kuacha kujiweka nyuma wakati ambao fursa zimetokea kwani kutokujiamini ndio kunakowafanya wanawake kukosa nafasi za kuongoza.


Vile vile aliwataka wanawake kutokuwa waoga na kujivisha moyo wa ujasiri kwani woga hauchochei maendeleo.


Nao wanachama katika wadi hiyo walisema vikao hivyo vingefanywa kila baada ya wiki mbili katika wadi zote hasa wakati huu tuna kwenda katika mwaka wa uchanguzi kwani kufanya hivyo kutawazindua vijana na kuona umuhimu wa kugombania nafasi za hizo pia itasaidia hasa kwa wale waliokuwa na hofu kuweza kujiamini.

Comments

Popular posts from this blog

MWANAMKE AJINYONGA, SABABU WASI WASI - PEMBA

NA, HASSAN MSELLEM - PEMBA PICHA KUTOKA MAKTABA Mwanamke aliyefahamika kwa jina la Raya Darusi Abdallla miaka 48, mkaazi wa Mbuzini Wilaya ya Chake Chake Mkoa wa Kusini Pemba, amefariki Dunia kwa kidaiwa kujinyonga kutokana na Msongo wa mawazo. Tukio Hilo limetokea Novemba 30.2025 saa 11 alfajiri huko Mbuzini Wilaya ya Chake Chake Mkoa wa Kusini Pemba. Omar Salum Ali, ambaye ni shemeji wa marehemu amesema kabla ya marehemu alikuwa na sumbuliwa na Msongo wa mawazo kutokana na kumpoteza kaka yake ambaye alifariki hivi karibuni, kugundulika kuwa ana maradhi ya sukari, mtoto wake wa kiume wa miaka 25, kuwa na ugonjwa akili hali iliyopelekea kupatwa na Msongo wa mawazo na kuamua kujinyonga. Katibu wa Sheha (Katibu wa Mwenyekiti) Shehia ya Mbuzini Yakub Ali Msabah, amesema alipata taarifa za tukio Hilo kutoka kwa Sheha wa Mbuzini kuhusu tukio baada ya kufika eneo la tukio waliukuta mwili wa Mama huyo ukiwa unanin'gia kwenye dari ya Nyumba ambayo alikuwa anaishi zamani. Kutoka tarehe 18 ...

"ZU" YAANDAA MAHAFALI YA 23, DISEMBA 17.2025.

HABARI NA, HASSAN MSELLEM - PEMBA UONGOZI WA CHUO KIKUU CHA ZANZIBAR (ZU) UNAYOFURAHA KUWAALIKA WAHITIMU WOTE WA MWAKA WA MASOMO 2024/2025, PAMOJA NA WAZAZI, WALEZI, NDUGU, JAMAA, MARAFIKI, NA WADAU WOTE WA MAENDELEO YA ELIMU KUSHIRIKI KATIKA MAHAFALI YA 23 YA CHUO KIKUU CHA ZANZIBAR (ZU). MAHAFALI HAYO YANATARAJIWA KUFANYIKA SIKU YA JUMAATANO 17 MWEZI DISEMBA 2025, KATIKA KIWANJA CHA CHUO KIKUU TUNGUU KIBELE KUANZIA SAA MBILI ASUBUHI, AMBAPO MGENI RASMI KATIKA MAHAFALI HAYO ANATARAJIWA KUWA RAISI WA ZANZIBAR NA MWENYEKITI WA BARAZA LA MAPINDUZI DKT. HUSSEIN ALI MWINYI. UONGOZI WA CHUO UNAWASHAURI WAHITIMU WOTE KUKAMILISHA TARATIBU ZOTE IKIWA NI PAMOJA NA KUCHUKUWA MAJOHO KUANZIA SIKU YA ALHAMISI YA TAREHE 11 HADI TAREHE 15.  MAZOEZI YA MAHAFALI YANI REHASAL ITAFANYIKA TAREHE 16. WATU WOTE WANAKARIBISHWA KATIKA MAHAFALI HAYO. CHUO KIKUU CHA ZANZIBAR (ZU) NI CHEM CHEM YA MAADILI NA TAALUMA. KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NA SIMU NAMBARI  0714843480/0718321095/0778777878 AHSANTENI

WATOTO KUJINYONGA ZANZIBAR, UTAFITI WAHITAJIKA.

HABARI NA, HASSAN MSELLEM, PEMBA Picha kutoka mtandaoni Visa vya watoto kujinyonga vimeanza kuwatia khofu na mashaka wazazi na walezi katika Visiwa vya Unguja na Pemba. Mashaka na khofu hiyo imeibuka baada ya matukio mawili mfululizo ya watoto wawili mmoja akiwa umri wa miaka (5) na mwengine (9) kuripotiwa kufariki dunia kwa kujinyonga kati ya tarehe 7 na 9 mwezi huu wa kumi mwaka 2025 kupitia kipindi cha Mawio kinachorushwa na Shirika la Utangazaji Zanzibar ZBC kila siku kuanzia saa 12:40 asubuhi. Katika tukio la kwanza mnamo tarehe 7.10.2025 mwandishi Masanja Mabula aliripoti tukio la Fatma Omar Kidere mwenye umri wa miaka tisa (9) mkaazi wa Mtondoo Jeuri Makaangale Wilaya ya Micheweni Mkao wa Kaskazini Pemba, amekutwa amefariki dunia na mwili wake ukiwa unanin’ginia kwa kutumia mtandio Jirani wa marehemu aliyefahamika kwa jina la Khamis Ali, amesema amepata taarifa za tukio hilo akiwa kazini baada ya kupigiwa simu na mke wake kumpa taarifa za kutokea kwa tukio hilo na kuondoka kazin...