Skip to main content

Wanaume watoe ruhusa kwa wanawake kuingia katika uongozi.

Na, Thuwaiba Habibu.

Sheha wa michamvi Khadija hassani haji amewaomba wanaume watoe ruhusa kwa wanawake kushiriki katika uongozi.


Ameyasema hayo wakati alipokuwa akizungumza na muandishi wa habari hizi huko michamvi mkoa wa kusini Unguja amesema wanaume waache tabia ya kutowapa uhuru wake zao katika kugombania nafasi za uongozi.


Alisema baadhi ya wanaume wanapoowa wanatumia mamlaka hiyo kuwazuia kushiriki katika shughuli mbali mbali ikiwemo suala la uongozi kufanya hivyo kuna wakosesha fursa muhimu wanawake.


Nae katibu wa kikundi cha kaya maskini shehiya ya michamvi Zawadi Sudi Ame alisema lazima iandalie kampeni ndani ya vikundi vya ushirika kuhamasisha wanawake kugombea nafasi hizo.


Alisema wanawake wengi hujihusisha na vikundi vya ushirika huku vijijini kwenye sehemu hizo ndiko kunako hitajika kampeni na hamasa ya nguvu kuhakikisha wanawake wanagombania nafasi za uongozi ifikapo mwaka 2025 ili kupigania maendeleo ya taifa.


Nao mwanakijiji wa michamvi wamesema wanawake ni watu wenye huruma sana wakati wanapopatiwa nafasi hizo hutaka maendeleo yaonekane na hawajivutii faida wao na familia zao.


Pia walisema kwanza wanawake wanatakiwa kujirekebisha katika suala la kuvunja moyo na kudharauliana wenyewe kitendo hicho huwapa mwanya mwanaume kuwakandamiza.


Walisema wanawake hawaoneshani ushirikiano na wanabaguwa endapo ikitokea nafasi ya uongozi huchangua mwanaume kuliko mwanamke mwenzao na hapo wanaume huwaona hawana uwezo lakini wakiamua kuacha kudharauliana na kuoneana wivu na wakawa na mashirikiano watafikia asilimia hamsini kwa hamsini na wanaume kwani kuongoza wanaweza.

Comments

Popular posts from this blog

MWANAMKE AJINYONGA, SABABU WASI WASI - PEMBA

NA, HASSAN MSELLEM - PEMBA PICHA KUTOKA MAKTABA Mwanamke aliyefahamika kwa jina la Raya Darusi Abdallla miaka 48, mkaazi wa Mbuzini Wilaya ya Chake Chake Mkoa wa Kusini Pemba, amefariki Dunia kwa kidaiwa kujinyonga kutokana na Msongo wa mawazo. Tukio Hilo limetokea Novemba 30.2025 saa 11 alfajiri huko Mbuzini Wilaya ya Chake Chake Mkoa wa Kusini Pemba. Omar Salum Ali, ambaye ni shemeji wa marehemu amesema kabla ya marehemu alikuwa na sumbuliwa na Msongo wa mawazo kutokana na kumpoteza kaka yake ambaye alifariki hivi karibuni, kugundulika kuwa ana maradhi ya sukari, mtoto wake wa kiume wa miaka 25, kuwa na ugonjwa akili hali iliyopelekea kupatwa na Msongo wa mawazo na kuamua kujinyonga. Katibu wa Sheha (Katibu wa Mwenyekiti) Shehia ya Mbuzini Yakub Ali Msabah, amesema alipata taarifa za tukio Hilo kutoka kwa Sheha wa Mbuzini kuhusu tukio baada ya kufika eneo la tukio waliukuta mwili wa Mama huyo ukiwa unanin'gia kwenye dari ya Nyumba ambayo alikuwa anaishi zamani. Kutoka tarehe 18 ...

"ZU" YAANDAA MAHAFALI YA 23, DISEMBA 17.2025.

HABARI NA, HASSAN MSELLEM - PEMBA UONGOZI WA CHUO KIKUU CHA ZANZIBAR (ZU) UNAYOFURAHA KUWAALIKA WAHITIMU WOTE WA MWAKA WA MASOMO 2024/2025, PAMOJA NA WAZAZI, WALEZI, NDUGU, JAMAA, MARAFIKI, NA WADAU WOTE WA MAENDELEO YA ELIMU KUSHIRIKI KATIKA MAHAFALI YA 23 YA CHUO KIKUU CHA ZANZIBAR (ZU). MAHAFALI HAYO YANATARAJIWA KUFANYIKA SIKU YA JUMAATANO 17 MWEZI DISEMBA 2025, KATIKA KIWANJA CHA CHUO KIKUU TUNGUU KIBELE KUANZIA SAA MBILI ASUBUHI, AMBAPO MGENI RASMI KATIKA MAHAFALI HAYO ANATARAJIWA KUWA RAISI WA ZANZIBAR NA MWENYEKITI WA BARAZA LA MAPINDUZI DKT. HUSSEIN ALI MWINYI. UONGOZI WA CHUO UNAWASHAURI WAHITIMU WOTE KUKAMILISHA TARATIBU ZOTE IKIWA NI PAMOJA NA KUCHUKUWA MAJOHO KUANZIA SIKU YA ALHAMISI YA TAREHE 11 HADI TAREHE 15.  MAZOEZI YA MAHAFALI YANI REHASAL ITAFANYIKA TAREHE 16. WATU WOTE WANAKARIBISHWA KATIKA MAHAFALI HAYO. CHUO KIKUU CHA ZANZIBAR (ZU) NI CHEM CHEM YA MAADILI NA TAALUMA. KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NA SIMU NAMBARI  0714843480/0718321095/0778777878 AHSANTENI

WATOTO KUJINYONGA ZANZIBAR, UTAFITI WAHITAJIKA.

HABARI NA, HASSAN MSELLEM, PEMBA Picha kutoka mtandaoni Visa vya watoto kujinyonga vimeanza kuwatia khofu na mashaka wazazi na walezi katika Visiwa vya Unguja na Pemba. Mashaka na khofu hiyo imeibuka baada ya matukio mawili mfululizo ya watoto wawili mmoja akiwa umri wa miaka (5) na mwengine (9) kuripotiwa kufariki dunia kwa kujinyonga kati ya tarehe 7 na 9 mwezi huu wa kumi mwaka 2025 kupitia kipindi cha Mawio kinachorushwa na Shirika la Utangazaji Zanzibar ZBC kila siku kuanzia saa 12:40 asubuhi. Katika tukio la kwanza mnamo tarehe 7.10.2025 mwandishi Masanja Mabula aliripoti tukio la Fatma Omar Kidere mwenye umri wa miaka tisa (9) mkaazi wa Mtondoo Jeuri Makaangale Wilaya ya Micheweni Mkao wa Kaskazini Pemba, amekutwa amefariki dunia na mwili wake ukiwa unanin’ginia kwa kutumia mtandio Jirani wa marehemu aliyefahamika kwa jina la Khamis Ali, amesema amepata taarifa za tukio hilo akiwa kazini baada ya kupigiwa simu na mke wake kumpa taarifa za kutokea kwa tukio hilo na kuondoka kazin...