Ukosefu wa timu, wakatisha ndoto za kuwa mchezaji Bora wa mpira wa miguu.
Makala Na, Hassan Msellem, Pemba
Mchezo wa mpira wa miguu
kwa wanawake Visiwani Zanzibar ni miongoni mwa mchezo unaoangaliwa kwa jicho
tofauti na wazanzibari wengi kwa kile kinachoaminika kuwa ni ukiukwaji wa mila,
silka na utamaduni wa Zanzibar kwa miaka mingi, hali iliyolekea Zanzibar
kuwa idadi Ndogo ya timu za mpira za Wanawake.
Ingawa tafiti zinaonesha
kuwa wapo wanawake wengi visiwani Zanzibar ambao wana uwezo na shauku ya
kucheza mpira wa miguu ikiwa ni sehemu ya kuonesha uwezo na umahiri wao katika
mchezo huo.
Riziki mwenye umri wa
miaka 17, anayeishi Mkoani Kusini mwa Kisiwa cha Pemba ni miongoni mwa wasichana
Kisiwani Pemba ambao wana uwezo mzuri wakucheza mpira wa miguu kiasi ya
kutokumtofautisha na mwanamme pindi anapokuwa uwanjani.
Kipaji cha Riziki
kiligundulika tangu akiwa na umri wa miaka kumi kwani alikuwa akipenda sana
kucheza mpira wa miguu na watoto wa kiume pindi wanapocheza mchezo huo kwenye
chochoro za mitaani na hata muda wa mapunziko wakati akiwa skuli ya msingi.
Baadhi ya watoto wenzake
wa kike, wazazi, walimu, ndugu na jamaa walianza kumshangaa na kukhofia
kutokana na tabia hiyo huku wengine wakimpa jina la dume dume, lakini Riziki hakujali
na aliendelea kusukuma kabumbu kama kijana wa kiume hukua afya yake ikionekana
kuimarika zaidi.
Malengo ya Riziki ni kusakata
kabumbu hadi kucheza timu ya Taifa ya Wanawake Tanzania Twiga Stars na kuwa mchezi
kinara Tanzania na Barani Afrika.
“Nina malengo mengi sana kwenye
football na miongoni mwa malengo hayo ni kucheza timu ya Taifa ya Wanawake
Tanzania Twiga Stars na nikifika hapo nitaongeza bidi ili nifanye vizuri zaidi
na kuwa mchezi kinara katika mashindano na ligi mbali mbali ndani nan je ya nchini”
alisema
Lakini licha ya malengo hayo Riziki anasema anakabiliwa na changamoto mbali mbali kutoka jamii inayomzunguka kwa kuhisiwa kuwa ni mwanamke aliyekosa malezi sahihi ya familia yake.
Maswali yaliyoanza kuibuka
mitaani na skuli, ni pamoja na ni kwa namna gani kipaji cha Time kitaweza
kuimarika zaidi?
Lakini swali hilo lilianza
kupata majibu pale uongozi wa Skuli aliyokuwa akisoma Riziki kuunda time ya
mpira wa miguu ya wanawake ya MKOANI QUEENS na kushiriki mechi na timu ya MAKOONGWE
GIRLS na kuibuka kinara katika mechi hizo kwa kushinda magoli zaidi ya
moja.
Nyota ya Riziki ya kukanyaga kabumbu ilianza kung’ara kwenye ya mechi mbali mbali n ahata kwenye Ligi ya Wanawake Zanzibar timu ya MKOANI QUEENS kwa kwa kushirikiana na timu ya MAKOONGWE GIRLS zikiungana na kuwa timu moja ambayo hushiriki ligi ya wanawake Zanzibar.
Mwaka 2022 Riziki alikuwa
miongoni mwa wachezaji 20 kutoka visiwani Zanzibar kupata mualiko wa kushiriki
katika mashindano ya ‘CHAN’ iliyofanyika nchini Uganda.
Kushiriki katika michuani
hiyo kuongeza moyo na ari mpya kwa Riziki kuzidisha bidi katika kufanya mazoezi
na kujiweka katika nafasi mzuri, lakini sio kwa Riziki peke yake hata wachezaji
wenzake, familia yake, ndugu jamaa, marafiki na wanajamii kwa ujumla
walihamasika sana ushiriki wa Riziki katika michuano hiyo.
Riziki alisema ana malengo
makubwa sana kwenye soka la wanawake, miongoni mwa malengo hayo nikuwa mchezaji
maarufu Zanzibar na kisha kupata nafasi ya kujiunga na timu ya taifa ya
Wanawake Tanzania yani Twiga Stars.
“nina malengo mengi sana kwakweli
na miongoni mwa malengo hayo ni kuwa mchezaji maarufu Zanzibar hii lakini pia
nataka nipate nafasi ya kuwa mchezaji kwenye timu ya taifa ya wanawake ya Tanzania
Twiga Stars na nikifika huko nitazidisha bidi ili kufanya vizuri zaidi”
Lakini licha malengo hayo
Riziki alisema anakabiliwa na changamoto lukuki miongoni mwa changamoto hizo ni
kutokana kwa wanajamii waliomzunguka kwa kumuona ni mwanmke aliyekosa malezi
sahihi na kuvunja vuhunzi vya mila, silka na utamaduni wa Mzanzibar.
Ali Khamis ni baba mzazi
wa Riziki alisema ameridhika kwa binti yake kucheza mpira licha ya kuwa mgumu
mwanzoni wakati binti yake anaanza kushiriki katika mchezo huo kwa kile alichokikhofia
kuwa binti yake atapata mabadiliko ya kitabia kama ilivyo kwa wazazi wengine
kisiwani Pemba.
Alisema “mwanzo nilikuwa mgumu sana kumuona mtoto wangu anajihusisha na mchezo wa mpira ukizingatia yeye ni mwanamke na kama unavyojua mtoto wa kike kwa tamaduni zetu hatakiwi kuonekana onekana ovyo ovyo lakini baada ya kuona anavaa vizuri na hakuna mabadiliko yoyote ya kitabia zaidi ya ukakamavu mimi na mama yake tukaona bora tumruhusu aendelee na kazi yake huenda akapata mafanikio baadae na kweli ameanza kupata mafanikio kwasababu mwaka juzi alikwenda Uganda kushiriki michuano ya CHAN”
Mariam Mussa Ame, ni jirani
na familia ya Riziki alisema anavutiwa sana na kipaji, bidii na nidhamu ya
mwanasoka huyo anapokuwa mtaani na hata uwanjani na kuwashangaa wale wenye
fikra hasi kwake.
“Mwanzo wakati alipokuwa anajiingiza kwenye uchezaji wa mpira watu wengi mtaani hata wazazi wake pia walikuwa wanamuhisi kama ni muhuni tu lakini kadri alivyokuwa ana shiriki mashindano mbali mbali mpaka akafikia kwenda Uganda ndipo watu waliposhituka na kujua kuwa kumbe kucheza mpira kwa mwanamke sio uhuni bali ni ajira na maendeleo kama wanavyojiajiri wanaume” alisema
Uongozi wa timu ya MKOANI QUEENS inamtegemea kama nahodha wa timu mwenye jukumu zito la kuhakikisha anasimamia kikosi chake mithili ya jeshi la anga la Urusi ili kupata matokeo yenye kuleta tabasam
Abuu Bakar Mzee ni kocha wa timu ya MKOANI QUEENS alisema Riziki ni kiungo nambari 10 mwenye akili, nguvu, ari na nidhamu humtegemea sana kwa kila mechi ili kuhakikisha timu yake inavimba mjini.
“Kwangu mimi Riziki namchukulia
kama uhai wa timu kwasababu ana uwezo na kiwango kizuri sana ukilinganisha na wachezaji
wengine kwanza anajituma sana kuanzia kwenye mazoezi na hata kwenye mechi na
ana nidhamu ya hali ya juu kiasi kwamba hata inapotokea tofauti uwanjani yeye
ndio huwatuliza wenzake” alisema kocha wa timu ya MKOANI QUEENS Abuu Bakar Mzee
Ni ipi mipango ya Shirikisho
la mpira wa miguu Kisiwani Pemba katika kukuza soka la wanawake?
Mpaka sasa Pemba ina timu
tatu tu za wanawake ikiwemo Makoongwe Stars, Mkoani Green na Wete ambapo ni
sawa na kusema Pemba kuna timu mbili tu za wanawake zinazosakata ndinga kwani
zinaposhiriki katika mashindo ya Ligi ya Wanawake Zanzibar timu ya Mkoani Green
huungana na timu Makoongwe Girls nakuwa timu moja kwa upande wa Mkoa wa Kusini
na timu ya Wete husimama kama timu pekee kwa upande wa Mkoa wa Kaskazini Pemba.
Msemaji wa ZFA Pemba
Khamis Ussi Mtumwa alisema katika kuhakikisha kuwa timu za mpira wa miguu za
wanawake zinaongezeka wameandaa utaratibu wa kupita maskulini ili kuangalia
wanafunzi wenye shauku, uwezo na vipaji vya kukanyaga ndinga (kucheza mpira) na
kuanzisha timu za skuli ambazo zitapata fursa ya kushiriki katika mashindo
mbali mbali kama vile mashindo ya UMISSETA na UMITASHUMTA yanayofanyika Tanzania
bara.
“ZFA tuna mipango mengi ya
kuhakikisha timu za mpira za wanawake zinaongezeka Kisiwani Pemba miongoni mwa
mipango hiyo tumeanza kupita maskulini kutafuta wanafunzi wenye vipaji vya
kucheza mpira baada ya kuwapata tunauomba uongozi wa skuli kuanzisha timu ya
mpira ya miguu baada ya hapo tunakuwa tunafuatilia kwa ukaribu maendeleo ya
timu hizo kisha kuwashirikisha katika mashindo mbali mbali zanzinbar nan je ya Zanzibar
yakiwemo mashindano ya UMISSETA na UMITASHUMTA ya kule Tanzania bara” alisema
Comments
Post a Comment