Skip to main content

HUDUMA ZA KIJAMII NI KIKWAZO KWA WANAWAKE KUSHIRIKI KATIKA NAFASI ZA UONGOZI.

 Habari Na,  Ahmed Abdulla.

LICHA ya elimu inayitolewa kwa jamii juu ya ushiriki wa wanawake katika nafasi za uongozi, lakini bado baadhi yao wanashindwa kujitokeza katika kuwania nafasi hizo kutokana na ukosefu wa huduma mbalimbali za kijamii.


Hayo yalibainishwa na wahamasishaji jamii (CBs) katika ripoti za mikutano ya kijamii na kupata muongozo wa wawezeshaji walizoziwasilisha katika kikao kilichofanyika katika ukumbi wa skuli ya Jangombe.


Walisema miongoni mwa huduma hizo zinazokosekana ambazo zinawafanya baadhi ya wanawake washindwe kugombea nafasi za uongozi ni pamoja na ukosefu wa maji  safi na salama, vitambulisho vya mzanzibar, vyeti vya kuzaliwa, miundombinu ya barabara za ndani na mambo mengine.


Walisema hali hiyo inawasababisha wanawake hao kutumia muda mwingi kutafuta huduma hizo na kushindwa kwenda kujishurikisha katika harakati za uongozi na kujitafutia maendeleo mengine ya kuinua uchumi wao.


Mhamasishaji jamii kutoka wilaya ya kati Bahati Issa Suleiman alisema licha ya kutolewa elimu kwa jamii ipo haja ya kuvifikia vyama vya siasa ili kuwahamasisha wanawake kuweza kugombea nafasi za uongozi.


"Kama hatutoingia katika vyama vya siasa kuwahamasisha hatuwezi kuwapata wanawake wataoweza kuwania nafasi za uongozi na badala yake tutakuwa tunasema tu miitaani,"alisema.


Mhamasishaji jamii kutoka Wilaya ya magharibi 'A' Fransisca Camilius Clement, alisema licha ya kuhamasishwa wanawake kushiriki katika nafasi za uongo lakini bado asilimia kubwa ya wanawake uwezo wao kiuchumi mdogo.


Alisema kutokana na hali hiyo ni vyema kuwezeshwa kiuchumi, hasa kupitia asilimia ambazo zimetengwa kwa ajili yao kupatiwa ili waweze kuzitumia kwa ajili ya kujipatia maendeleo.


"Kuna asilimia kumi zilizotengwa na Halmashauri ambazo asilimia nne zimewekwa kwa ajili ya kuwezeshwa wanawake, fedha hizo hivi sasa zimehamishiwa wizara ya Uwezeshaji, asilimia kubwa ya wanawake hawazifahamu fedha izo njia ya kuzipata, hivyo kunaumuhimu wa kufatiliwa ili kuweza kuwasaidia,"alisema.


Abdulrahman Khatib Mohammed kutoka Wilaya ya magharibi 'A' alisema ushirikia wa viongozi wa majimbo mdogo kwa wananchi haliambayo inasababisha kuwepo kwa changamoto nyingi na kushindwa kupatikana ufumbuzi.


Alisema hali hiyo husababisha hata kuwatia dosari baadhi ya wananchi wengine ambao wataonesha nia ya kugombea katika nafasi hizo.


Meneja miradi wa Chama cha Waandishi wa Habari, Wanawake Tanzania (TAMWA, ZNZ), Ali Mohammed, alisema ripoti hiyo wameipokea na wanaenda kujiaandaa zaidi kwa kuandaa mikakati ambayo itaweza kuweka mazingira mazuri kwa makundi hayo.


Alisema lengo la kuwaweka wahamasishaji jamii ni baada ya kubaini kwamba kundi hilo bado linakabiliwa na changamoto nyingi haliambayo inawasababisha kutofikia malengo yao ya kuwa viongozi.


Mratibu wa mradi wa kuwawezesha wanawake kushika nafasi za uongozi, kutoka Jumuiya ya Wanasheria Wanawake Zanzibar (ZAFELA), Khamis Ali Rashid, aliwataka wahamasishaji jamii kutokata tamaa na badala yake kuendelea kuhamasisha wanawake kujitokeza katika nafasi hizo, licha ya changamoto wananzokabiliana nazo.


Mkutano huo wa siku moja wa uwasilishaji ripoti za mikutano ya jamii umeandaliwa na ZAFELA kupitia mradi wa kuwawezesha wanawake kushiriki katika nafasi za uongozi (SWIL), unaotekelezwa kwa pamoja baina ya TAMWA ZNZ, ZAFELA na PEGAO chini ya ufadhili wa ubalozi wa Norway Tanzania.

 

 

Comments

Popular posts from this blog

MWANAMKE AJINYONGA, SABABU WASI WASI - PEMBA

NA, HASSAN MSELLEM - PEMBA PICHA KUTOKA MAKTABA Mwanamke aliyefahamika kwa jina la Raya Darusi Abdallla miaka 48, mkaazi wa Mbuzini Wilaya ya Chake Chake Mkoa wa Kusini Pemba, amefariki Dunia kwa kidaiwa kujinyonga kutokana na Msongo wa mawazo. Tukio Hilo limetokea Novemba 30.2025 saa 11 alfajiri huko Mbuzini Wilaya ya Chake Chake Mkoa wa Kusini Pemba. Omar Salum Ali, ambaye ni shemeji wa marehemu amesema kabla ya marehemu alikuwa na sumbuliwa na Msongo wa mawazo kutokana na kumpoteza kaka yake ambaye alifariki hivi karibuni, kugundulika kuwa ana maradhi ya sukari, mtoto wake wa kiume wa miaka 25, kuwa na ugonjwa akili hali iliyopelekea kupatwa na Msongo wa mawazo na kuamua kujinyonga. Katibu wa Sheha (Katibu wa Mwenyekiti) Shehia ya Mbuzini Yakub Ali Msabah, amesema alipata taarifa za tukio Hilo kutoka kwa Sheha wa Mbuzini kuhusu tukio baada ya kufika eneo la tukio waliukuta mwili wa Mama huyo ukiwa unanin'gia kwenye dari ya Nyumba ambayo alikuwa anaishi zamani. Kutoka tarehe 18 ...

"ZU" YAANDAA MAHAFALI YA 23, DISEMBA 17.2025.

HABARI NA, HASSAN MSELLEM - PEMBA UONGOZI WA CHUO KIKUU CHA ZANZIBAR (ZU) UNAYOFURAHA KUWAALIKA WAHITIMU WOTE WA MWAKA WA MASOMO 2024/2025, PAMOJA NA WAZAZI, WALEZI, NDUGU, JAMAA, MARAFIKI, NA WADAU WOTE WA MAENDELEO YA ELIMU KUSHIRIKI KATIKA MAHAFALI YA 23 YA CHUO KIKUU CHA ZANZIBAR (ZU). MAHAFALI HAYO YANATARAJIWA KUFANYIKA SIKU YA JUMAATANO 17 MWEZI DISEMBA 2025, KATIKA KIWANJA CHA CHUO KIKUU TUNGUU KIBELE KUANZIA SAA MBILI ASUBUHI, AMBAPO MGENI RASMI KATIKA MAHAFALI HAYO ANATARAJIWA KUWA RAISI WA ZANZIBAR NA MWENYEKITI WA BARAZA LA MAPINDUZI DKT. HUSSEIN ALI MWINYI. UONGOZI WA CHUO UNAWASHAURI WAHITIMU WOTE KUKAMILISHA TARATIBU ZOTE IKIWA NI PAMOJA NA KUCHUKUWA MAJOHO KUANZIA SIKU YA ALHAMISI YA TAREHE 11 HADI TAREHE 15.  MAZOEZI YA MAHAFALI YANI REHASAL ITAFANYIKA TAREHE 16. WATU WOTE WANAKARIBISHWA KATIKA MAHAFALI HAYO. CHUO KIKUU CHA ZANZIBAR (ZU) NI CHEM CHEM YA MAADILI NA TAALUMA. KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NA SIMU NAMBARI  0714843480/0718321095/0778777878 AHSANTENI

WATOTO KUJINYONGA ZANZIBAR, UTAFITI WAHITAJIKA.

HABARI NA, HASSAN MSELLEM, PEMBA Picha kutoka mtandaoni Visa vya watoto kujinyonga vimeanza kuwatia khofu na mashaka wazazi na walezi katika Visiwa vya Unguja na Pemba. Mashaka na khofu hiyo imeibuka baada ya matukio mawili mfululizo ya watoto wawili mmoja akiwa umri wa miaka (5) na mwengine (9) kuripotiwa kufariki dunia kwa kujinyonga kati ya tarehe 7 na 9 mwezi huu wa kumi mwaka 2025 kupitia kipindi cha Mawio kinachorushwa na Shirika la Utangazaji Zanzibar ZBC kila siku kuanzia saa 12:40 asubuhi. Katika tukio la kwanza mnamo tarehe 7.10.2025 mwandishi Masanja Mabula aliripoti tukio la Fatma Omar Kidere mwenye umri wa miaka tisa (9) mkaazi wa Mtondoo Jeuri Makaangale Wilaya ya Micheweni Mkao wa Kaskazini Pemba, amekutwa amefariki dunia na mwili wake ukiwa unanin’ginia kwa kutumia mtandio Jirani wa marehemu aliyefahamika kwa jina la Khamis Ali, amesema amepata taarifa za tukio hilo akiwa kazini baada ya kupigiwa simu na mke wake kumpa taarifa za kutokea kwa tukio hilo na kuondoka kazin...