Na, Thuwaiba Habibu.
Mwalimu wa vikundi vya kueka na kukopa kutoka Umbuji kheri Omari amewataka wanawake kutumia vikundi kujifunza uongozi pamoja na kujikwamua kiuchumi.
Amesema hayo wakati akizungumza na muandishi wa habari hizi huko umbuji wilaya ya kati mkoa wa kusini unguja amesema ndani ya vikundi ni rahisi kwa wanawake kuweza kujifunza uongozi kwasababu vikundi ni wanawake watupu na kuna nafasi mbali mbali za kuwajengea uzoefu.
"kuna nafasi za mwenyekiti , makatibu na washika hazina hivyo basi nafasi hizi wakizitekeleza kiuwadilifu ikitokea nafasi ya uongozi wa juu inakuwa ni wepesi kwa mtu kugombea na kutekeleza majukumu yao kiusahihi.
Pia alisema najitahidi kuwamasisha wanawake kuwa imara katika shughuli za vikundi na uongozi kwani watajikwamua kiuchumi na kuleta maendeleo katika nchi zetu.
Huu sio muda tena wa mwanamke kusubiri kulitewa na kuongozwa tu bali wanawake watakiwa wapambane kutafuta ila kwa utaratibu mzuri.
Kwa upande wake katibu wa kikundi cha wanawake na maendeleo khadija fundi hiari alisema mwalimu kheri ni mtu ambaye yupo na mawazo hali juu ya wanawake kuongoza na kuweza kumiliki Mali zao kitendo hicho kilimfanya azishe kikundi kwani ingekuwa vigumu kupita kila nyumba kuhamasisha.
Vile vile alisema mwalimu huyo ni kigezo cha kuigwa na wanaume wote kwani kupoteza muda wake kwa ajili ya wanawake hilo ni suala la ujasiri sababu wanaume wengi hushindwa kufanya jambo hilo.
Nae mwanakikundi mwengine bi chiku ramadhani anaeleza kuwa kama watajikokeza wanaume wengine kama bwana kheri Omar kuwaunganisha wanawake kwa kuwaanzishia vikundi basi itakuwa ni kitu Cha muhimu na wanawake watajiimarisha kiuchumi na watajifunza zaidi kuongozi na watakuwa sio tegemezi Tena kwani watakuwa na muamko wa kimaendeleo.
Pia alisema tunataka kufanye kazi kwa kuendana na kauli mbiu ya mama Samia ya hapa kazi tu kauli hii itazidi kuwahamasisha kushiriki kikamilifu katika masuala ya uongozi.

Comments
Post a Comment