Skip to main content

WILAYA YA MKOANI YAFANYA KONGAMANO LA "AMANI" KUELEKEA UCHAGUZI MKUU 2025.

NA, HASSAN MSELLEM, PEMBA

Mkuu wa Wilaya ya Mkoani Miza Hassan Faki, akimkabidhi Nishani Makamo wa Pili wa Rais Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla

Viongozi wa vyama vya Siasa wametakiwa kutotumia hotuba zinazochochea Ubaguzi, Chuki na Uhasama katika kampeni zinazotarajiwa kufanyika hivi punde Visiwani Zanzibar ili kuepukana na uvunjifu wa amani.

Akifungua Kongamano lililoandaliwa na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya Mkoani huko katika Ukumbi wa Umoja ni Nguvu Mkoani, Makamo wa Pili wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla, amesema lengo la Kampeni za Kisiasa ni wagombea kunadai sera na ilani za vyama vyao kwa wananchi ili waweze kuwachagua na sio kutoa hotuba za Ubaguzi, Chuki na Uhasama hali inayoweza kusababisha uvunjifu wa amani nchini.

Aidha Mhe. Hemed amewasihi Vijana kutokutumiwa vibaya na wasiasa kwa kisingizio cha Uchaguzi kwani wao ndio wahanga wakubwa vitendo vya uvunjifu wa amani katika kipindi cha Uchaguzi.

“Niwaombe sana viongozi wa vyama vya siasa na wagombea wa nafasi mbali mbali kutotumia hotuba zenye kulenga ubaguzi, chuki na uhasama kwa haotuba kama hizo ndio chanzo cha uvunjifu wa amani kwasababu huwagawa watu na kuanza kunyooshea na vidole kwanini musinadi Sera, Ilani na sambambva na kuwaahidi wananchi mazuri” alisema 

Kwa upande Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba Mhe. Rashid Hadid Rashid, amesema AMANI na Utulivu ndio tunu pekee za Taifa na Uchaguzi ni tukio linalopita, hivyo wananchi wanapaswa kuzienzi tunu hizo kwani zikitoweka ni vigumu kuzirudisha

Sambamba na hilo Mhe. Hadid, amesema Jeshi la Polisi Mkoa wa Kusini Pemba limejipanga kuimarisha Ulinzi katika kipindi cha kampeni na Uchaguzi ili kuhakikisha wananchi wanaendelea na shughuli zao za maisha kwa amani na utulivu.

“Nasaha zangu kwa wananchi hasa Vijana musitumike vibaya katika kipindi cha kampeni na Uchaguzi kwasababu amani na utulivu ndio tunu pekee ambazo Mungu ametujaalia katika Taifa letu na tunu hizo zikitoweka kuzirudisha sio kazi rahisi kama tunavyoona leo kwenye mataifa mbali mbali duniani” RC Kusini Pemba Rashid Hadid Rashid

Nae Mkuu wa Wilaya ya Mkoani Bi. Miza Hassan Faki, amesema lengo la Kongamano hilo ni kuwaleta pamoja wadau mbali mbali wakiwemo Jeshi la Polisi, Viongozi wa vyama vya Siasa, Waandishi wa Habari na Vijana ili kujadili namna bora ya kudumisha amani na utulivu katika kipindi chote Uchaguzi.

“Tumeona ni vyema tukutane pamoja leo kwasababu suala la kudumisha Amani ni letu sote kila mmoja kwa nafasi yake ana wajibu na jukumu la kudumisha amani” DC Wilaya ya Mkoani Miza Hasssan Faki 

Akiwasilisha mada juu ya Dhamira ya Uchaguzi kuelekea Uchaguzi Mkuu kwa Amani Katibu wa Siasa Uenezi Zanzibar Mbeto, amesema suala la kura ya mapema lipo kwa mujibu wa Sheria ya Uchaguzi wa Zanzibar, hivyo basi ni jukumu la vyama kutambua kuwa suala hilo lipo kwa mujibu wa Sheria.


Akiwasilisha mada ya Kuzia hotuba za chuki na hatua muhimu katika kudumisha amani kitaifa, Katibu wa Ofisi ya Mufti Pemba Sheikh Said Ahmad, amesema suala la amani limepewa nafasi kubwa katika Dini ya Kiislam, hivyo basi amewaomba Viongozi wa Dini na Maimamu wa Misikiti kuhubri amani katika za Ibada.

Akiwasilisha mada ya Mitandao ya kijamii na Jukumu la vyombo vya Habari Mwandishi Mwandamizi Said Mohammed Ali, amewasihi Waandishi wa Habari kuitumia mitando ya kijamii kwa kuzingatia Sheria na Maadili ya Uandishi wa Habari ili kuepukana na makosa ya Kimtandao yanayojitokeza mara kwa mara

“Kuibuka kwa mitandao ya Kijamii kumeleta changamoto kubwa mno katika tasnia ya Habari kwasababu kumekuwa na kasi kubwa mno ya kusambaa kwa Habari kwa haraka na chakusikitisha zaidi kwamba hata wasiokuwa na taaluma ya Habari na wamekuwa waandishi wa Habari, hivyo basi niwasihi sana waandishi Habari wenzangu kuitumia hii mitandao ya kijamii kwa kuzingatia Sheria, kanuni na maadili yetu ili kuepukana na makosa ya kimtandao ambayo yamekuwa yakijitokeza mara kwa mara” mwandishi mwandamizi Said Mohammed Ali 

Nao wadau walishiriki katika Kongamano hilo wamewaomba viongozi kwa Siasa na Dini kuyafanyia kazi kwa vitendo wanayoyahubiri kwa wananchi ikiwemo Amani na kutenda haki ili kuendana na yale wanayoyahubiri.

“Mimi ombi langu ni moja tu kwa wanasiasa, Viongozi wa dini na Jeshi la Polisi kwamba haya tunayoyahubiri kwa wananchi tuyatekeleze kwa vitendo sio tunahubiri amani lakini nyinyi ndio mukawa vyanzo vya uvunjifu wa amani hapo kwasababu vitendo vinazungumza zaidi kuliko kauli” Kiongozi wa Dini kutoka Kangani Fadhili Bakar Shoka

Kongamano hilo lililoandaliwa na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya Mkoani limejumuisha wadau mbali mbali wakiwemo Viongozi Chama cha Mapinduzi CCM, Jeshi la Polisi, Viongozi wa Dini, Waandishi wa Habari na Vijana likibebwa na kauli mbiu inayosema “AMANI YETU NI URITHI WETU, TUILINDE KWA AJILI 

YA VIZAZI VYETU” 



Comments

Popular posts from this blog

MWANAMKE AJINYONGA, SABABU WASI WASI - PEMBA

NA, HASSAN MSELLEM - PEMBA PICHA KUTOKA MAKTABA Mwanamke aliyefahamika kwa jina la Raya Darusi Abdallla miaka 48, mkaazi wa Mbuzini Wilaya ya Chake Chake Mkoa wa Kusini Pemba, amefariki Dunia kwa kidaiwa kujinyonga kutokana na Msongo wa mawazo. Tukio Hilo limetokea Novemba 30.2025 saa 11 alfajiri huko Mbuzini Wilaya ya Chake Chake Mkoa wa Kusini Pemba. Omar Salum Ali, ambaye ni shemeji wa marehemu amesema kabla ya marehemu alikuwa na sumbuliwa na Msongo wa mawazo kutokana na kumpoteza kaka yake ambaye alifariki hivi karibuni, kugundulika kuwa ana maradhi ya sukari, mtoto wake wa kiume wa miaka 25, kuwa na ugonjwa akili hali iliyopelekea kupatwa na Msongo wa mawazo na kuamua kujinyonga. Katibu wa Sheha (Katibu wa Mwenyekiti) Shehia ya Mbuzini Yakub Ali Msabah, amesema alipata taarifa za tukio Hilo kutoka kwa Sheha wa Mbuzini kuhusu tukio baada ya kufika eneo la tukio waliukuta mwili wa Mama huyo ukiwa unanin'gia kwenye dari ya Nyumba ambayo alikuwa anaishi zamani. Kutoka tarehe 18 ...

Mariam Muhene – mfano wa kuigwa kwa wanawake kwenye ulingo wa siasa ni

MAKALA NA, HASSAN MSELLEM -PEMBA Tangu Tanzania iruhusu mfumo wa vyama vingi mwaka 1992, Mariam Muhene alijiunga na chama cha Civic United Front (CUF) ambapo mwaka 1995, aligombea nafasi ubunge wa viti maalumu na kuvuka hatua zote ikiwemo kula kiapo mahkamani lakini hakufanikiwa kukikalia kiti hicho. “Mwaka 1995 niligombea ubunge wa viti maalum na nikapita kila kipengele mtu wa kwanza wilaya, taifa bodi ya uongozi, nikala kiapo mahkmanai lakini katika nafasi mbili zilizoletwa kwa kila mkoa Kusini na Kaskazini Pemba mimi sikubahatika” amesema  Safari yake ya kisiasa za upinzani iliendelea na mnamo mwaka 2000, aligombea nafasi ya ubunge wa kuchahguliwa kupitia chama cha Allience for Democratic Change (ADC) Jimbo la Chake Chake lakini kutokana na changamoto zilizojitokeza ikiwe mawakala wa Chama chake kutokuruhisiwa kuingia kwenye vya kupiga kura jambo ambalo amesema lilichangia kukosa nafasi hiyo. Kwasasa Mariam Mohammed Muhene anashika nafasi ya Kamishna wa ADC kanda ya Pemba, nafas...

WATOTO KUJINYONGA ZANZIBAR, UTAFITI WAHITAJIKA.

HABARI NA, HASSAN MSELLEM, PEMBA Picha kutoka mtandaoni Visa vya watoto kujinyonga vimeanza kuwatia khofu na mashaka wazazi na walezi katika Visiwa vya Unguja na Pemba. Mashaka na khofu hiyo imeibuka baada ya matukio mawili mfululizo ya watoto wawili mmoja akiwa umri wa miaka (5) na mwengine (9) kuripotiwa kufariki dunia kwa kujinyonga kati ya tarehe 7 na 9 mwezi huu wa kumi mwaka 2025 kupitia kipindi cha Mawio kinachorushwa na Shirika la Utangazaji Zanzibar ZBC kila siku kuanzia saa 12:40 asubuhi. Katika tukio la kwanza mnamo tarehe 7.10.2025 mwandishi Masanja Mabula aliripoti tukio la Fatma Omar Kidere mwenye umri wa miaka tisa (9) mkaazi wa Mtondoo Jeuri Makaangale Wilaya ya Micheweni Mkao wa Kaskazini Pemba, amekutwa amefariki dunia na mwili wake ukiwa unanin’ginia kwa kutumia mtandio Jirani wa marehemu aliyefahamika kwa jina la Khamis Ali, amesema amepata taarifa za tukio hilo akiwa kazini baada ya kupigiwa simu na mke wake kumpa taarifa za kutokea kwa tukio hilo na kuondoka kazin...