Posts

Showing posts from July, 2024

"Hata Dini zetu zimehimiza kushiriki michezo Ili kuwa na afya imara" Othman Massoud Othman

Image
Na, Hassan Msellem, Pemba MAKAMU wa Kwanza wa Rais Zanzibar Othman Massoud Othman, amevishauri vilabu ya mazoezi nchini, kujitengenezea kanuni, zitakazowavutia watu wingi zaidi kujiunga kwenye mazoezi, ili kuondoa dhama potofu ya mazoezi ni uhuni. Alisema, kama kundi kubwa la watu wanadhana kuwa mazoezi ni uhuni na kuvunja maadili, ni wakati sasa kwa vilabu vya mazoezi na michezo, kuwa na kanuni zitakazofuta dhana hiyo. Makamu huyo wa Kwanza, aliyasema hayo leo Julai 28, 2024 uwanja wa michezo Gombani Chake chake, kwenye bonanza la miaka 10, tokea kuanzishwa kwa ‘Gombani Fitness Club’ lilioandaliwa kwa pamoja na TAMWA-Zanzibar na Shirika la Bima. Alieleza kuwa, kwa vile mozoezi ni jambo muhimu kwa kila mmoja, ni vyema kuwepo na kanuni ndogo ndogo, ambazo zitawavutia wengine, kushiriki katika kupata kinga ya miili yao. Alifahamisha kuwa, ni kweli kama kuna viashiria vya uvunjifu wa maadili, inaweza kuwa sababu kwa baadhi ya watu, kuona sio sehemu salama, ingawa zikiwepo kanuni zitawavut...

BONANZA LA MICHEZO KUIBUA VIPAJI VYA WANAMICHEZO WANAWAKE PEMBA.

Image
Na, Hassan Msellem, Pemba. CLUB ya mazoezi ya viungo Gombani fitness kwa kushirikiana na Chama cha waandishi wa habari wanawake Tanzania Tamwa Zanzibar pamoja na Shirika la Bima Zanzibar (ZIC) wameandaa bonanza la michezo na mazoezi Kisiwani Pemba litakaloanza shamra shamra zake kuanzia kesho tarehe 20 na kufikia kilele siku ya tarehe 28.07.2024 huu kwa kufanyika matembezi ambapo zaidi ya washiriki 500 kutoka nje ya kisiwa cha Pemba wanatarajiwa kushiriki katika bonanza hilo. Akizungumza Mratibu wa Bonanza hilo KHalfan Amour Muhamed ambae pia ni Katibu wa Gombani fitness, alisema kuwa lengo Bonanza hilo litakaloanza na matembezi kutoka Madungu hadi uwanja wa Gombani kuanzia saa 12 za asubuhi ni kusaidia kuhamasisha ushiriki wa wanawake na wasichana kwa kushirikisha na kukuza usawa wa kijinsia katika michezo ya aina mbali mbali kwa wanawake kisiwani humo . Amesema Club hiyo kwa kutambua juhudi zinazofanywa na wadau wa michezo kwa wanawake wameona kuna umuhimu mkubw...

"Waandishi tumieni kalamu zenu kusisitiza sheria mpya za Habari" Mjumbe wa Bodi Tamwa-ZNZ-Hawra Shamte

Image
 Na, Thuwaiba Habibu, Zanzibar  Mjumbe wa bodi cha cha waandishi wa habari wanawake (Tamwa) Hawra Shamte aliwataka waandishi kuendelea kutumia kalamu zao kuhakikisha sheria ya habari rafiki zinapatikana. Ameyasema hayo katika kikao cha kutoa mrejesho wa kazi za mapitio ya sheria ya habari zenye vifungu vinavyo kinza uhuru wa habari zilizofanywa kwa mwaka mzima ambacho kimefanyika Tamwa Tunguu Unguja alisema tunategemea sheria zetu zitatoka kwa makatibu wakuu na kuacha kupigwa dana dana kutokana na ahadi tunazopewa kwa sheria zetu kuu mbili za habari ikiwa ni wakala wa usajili magazeti, na tume ya utangazaji kwa sababu tushazisemea sana na tunazidi kuziandikia hadi tuone mafanikio. Pia alisema kuna vyombo vya habari hawataki kusikia habari kuhusu sheria hizo lakini ipo haja ya kutumia vyombo vyengine ili kuweza kufikia lengo letu la kupata sheria mpya. Kwa upande wake Afisa mratibu wa sheria za habari Zaina Mzee alisema tunaenda mwaka wapili katika kuhamasisha upatik...

"UCHUMI WA BULUU NI BIASHARA KATI YA SERIKALI NA BENKI YA CRDB CRDB" MWENYEKITI WA ADC TAIFA-SHABANI ITUTU.

Image
Na, Hassan Msellem, Pemba  M wenyekiti wa chama cha Alliance for Democratic Change (ADC) Taifa Shabani Itutu, ameiomba Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia Wizara ya Uchumi wa Buluu kuboresha hali za Wananchi kupitia Sera ya Uchumi wa Buluu, ambayo mpaka sasa haijafikiwa ipaswavyo. Mwenyekiti huyo ametoa kauli hiyo kwa nyakati tofauti wakati akizungumza na wanachama wa wa Chama cha ADC na Wananchi mbali mbali Kisiwani Pemba, amesema licha ya Serikali ya awamu ya nane kuanzisha Sera ya Uchumi wa Buluu kwa lengo la Kuboresha Hali za Wananchi kupitia rasilimali za baharini ikiwemo uvuvi wa Samaki na zao la mwani bado hali za Wananchi kupitia rasilimali hizo hazijaimarika. Akitaja sababu zinazobabisha kutokufikiwa kwa Sera ya Uchumi wa buluu kwa Wananchi ni pamoja kukosekana kwa vyombo vya kisasa vya uvuvi, kukosekana kwa viwanda vya kusindika samaki pamoja kutokufanya kazi kwa viwanda vya kuchakata zao la mwani. "Tunaamini dhamira ya Serikali ni njema sana kupitia Sera ya Uchumi...

Uchechemuzi mapungufu Sheria za Habari kusaidia upatikanaji sheria mpya

Image
IMEELEZWA juhudi za Chama Cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania, Zanzibar (TAMWA ZNZ) kwa kushirikiana na wadau na waandishi wa habari Zanzibar kufanya ushawishi na utetezi wa mabadiliko ya sheria zenye vifungu vinavyokwaza uhuru wa habari zimesaidia kuweka matumaini ya baadhi ya sheria hizo kufanyiwa marekebisho. Hayo yameelezwa na wadau katika kikao cha tathimini ya utekelezaji wa programu ya uchechemuzi wa sheria za habari Zanzibar kilichowashirikisha waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali kisiwani Pemba. Zaina Mzee ambaye ni afisa programu hiyo kutoka TAMWA ZNZ, amesema program ya uchechemuzi wa mabadiliko ya sheria za habari zinazokwaza uhuru wa habari Zanzibar imeonyesha kuleta mabadiliko ya maboresho kwenye baadhi ya vifungu vya sheria za habari ambazo ni kandamizi. Alieleza, kupitia programu hiyo tayari TAMWA ZNZ kwa kushirikiana na wadau mbalimbali ikiwemo Kamati ya Wataalamu wa Masuala ya Habari Zanzibar ZAMECO wamefanya vikao na taasisi za serikali ambazo zinahusika...

Uhaba wa Viwanja Vya Michezo wadumanza vipaji vya watoto wa kike katika kushiriki michezo.

Image
  MAKALA NA, SALIM HAMAD, PEMBA Katika tasnia ya Michezo katika Kisiwa Cha Pemba,kumekuwa uhababa wa Viwanja jambo linalochangia wanawake kushidwa   kutoshiriki   katika harakati za michezo kutokana na kutokuwepo kwa mazingira rafiki ya kufanyia mazoezi.   Maranyingi inaeleka kwamba wadu wengi wa Michezo wamekuwa wakiangalia na kuelekeza Nguvu zao kwenye michezo mingine kama Mpira wa Miguu lakini kwenye mchezo wa Valbal Basketi Ball imekuwa ikiwekwa Pembeni.   Sudi Saaduni ni Meneja wa timu ya Wete Star,aliomba Serekali kuangalia uwezkano wa kujenga Viwanja vya Michezo inayohusina na michezo ya wasichana ili na wao wapate fursa za kushiriki michezo kwani michezo ni afya na ni ajira. Alisema wakati Viwanja Vipatakapo Jengwa wanawake watahamasika kujiingiza kwenye michzo kwa vile tayari kutakuwa kumeshawekwa mazingira rafiki katika kwenye Viwanja vya Michezo.   ‘’Unajua uhaba wa Viwanja wa Michezo Bado Pemba,nishida jambo hili linawafanya wa...

Unyanyapaa unavyokatisha ndoto za watoto wa kike wenye ulemavu kwenye michezo.

Image
  NA SALIM HAMAD, PEMBA. Mara nyingi katika jamii kumekuwa na tamaduni ambazo zimekuwa zikiwanyima fursa watu wenye ulemavu wakiwemo wanawake katika kushiriki michezo na kuwaona kuwa hawana uwezo wa kushirki.   Pamoja na juhudi zinazochukuliwa Serikali na wadau mbali mbali katika kuondosha changamoto hiyo lakini bado wapo baadhi ya wanajamii na  uwazi wa uthubutu katika kuwapambania watu hao kwenye mambo ya msingi ikiwemo elimu na hata kushiriki katika michezo.   Makala hii itangazia vikwazo vinavyokwamisha watoto wa kike wenye ulemavu kushindwa kufikia ndoto zao.   Rashid Hamad Khamis ni Katibu wa timu ya watu wenye Ulemavu Mkoa wa Kaskazini Pemba,alisema jamii haijatilia mkazo kwa watu wenye ulemavu wa akili katika kushiriki michezo.   Alisema hawafahamu umuhimu wa michezo kwa watu hao ,  ambapo kwa kiasi kikubwa michezo inawafanya kukua kimaadili, kimwili na kiakili   hivyo  kuchukulia  kwamba sio jambo la lazim...

USAWA WA KIJINSIA NAFASI ZA UONGOZI NDANI YA VYAMA VYA SIASA WALETA AHUWENI.

Image
  Takriban haki zote zilizoelezwa katika Mkataba wa kuondoa aina zote za Ubaguzi dhidi Wanawake zilizotambuliwa na kulindwa. Katika ya Zanzibar yam waka 1984 na Sheria nyengine mbali mbali kwa mfano kuna mabadiliko makubwa katika Sheria ya ajira Zanzibar, nambari 3 ya mwaka 2005 ambayo inampa haki na fursa sawa muajiriwa mwanamke.   Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania upande wa Pemba Katika chaguzi zilizopita kwa upande wa Pemba Wanawake kumi (10) waligombea nafasi mbali mbali, wawili kati ya hao waligombea ubunge kupitia viti maalum na wanne waligombea Uwakilishi kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Viti maalum, wanne Kaskazini Pemba na watatu Kusini Pemba na mmoja kupitia chama cha ACT Wazalendo.   Takwimu zinaonesha bado kuna ushiriki mdogo wa Wanawake katika Uongozi, ingawaje kwa sasa, Wanawake Zanzibar wamehamasika kutumia haki zao za Kidemokrasia mfano wapiga kura katika Uchaguzi Mkuu wa 2020, jumla ya 294,115 Wana...

'Mradi wa SWIL' wawafungulia wanawake dunia ya uongozi.

Image
  Makala Na, Hassan Msellem Mradi wa  U hamasishaji wanawake kushiriki katika Uongozi  (SWIL) ni mradi ulioanzishwa kwa lengo la kutambua changamoto mbali mbali zinazowakabili wanawake nakupelekea kushindwa kushiriki katika shughuli mbali mbali za kijamii na uongozi ili zipatiwe ufumbuzi ikiwemo ukosefu wa elimu ya jumla na uongozi, huduma za afya, Maji, Umeme, miundombinu bora ya barabara, mfumo dume na hatimae kuongeza idadi ya viongozi wanawake katika ngazi mbali mbali za maamuzi kama vile Bungeni, Baraza la Wawakilishi, Madiwani, Masheha nakadhalika. Mradi huo unaotekelezwa na taasisi tatu Visiwani Zanzibar ambazo ni  Jumuiya ya Utetezi wa Kijinisia na Mazingira Pemba (PEGAO)  Chama cha Waandishi wa Habari Tanzania (TAMWA) Kanda ya Zanzibar pamoja na Chama cha Wanasheria Wanawake Tanzania (ZAFELA) na kuufadhiliwa na Ubalozi wa Norway Tanzani, ulioanzishwa Novemba 2020 na kutarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwaka 2023. Kwa mujibu wa mratibu wa Jumuiya ya Utete...