'Mradi wa SWIL' wawafungulia wanawake dunia ya uongozi.
Makala Na, Hassan Msellem
Mradi wa Uhamasishaji wanawake kushiriki katika Uongozi (SWIL) ni mradi ulioanzishwa kwa lengo la kutambua changamoto mbali mbali zinazowakabili wanawake nakupelekea kushindwa kushiriki katika shughuli mbali mbali za kijamii na uongozi ili zipatiwe ufumbuzi ikiwemo ukosefu wa elimu ya jumla na uongozi, huduma za afya, Maji, Umeme, miundombinu bora ya barabara, mfumo dume na hatimae kuongeza idadi ya viongozi wanawake katika ngazi mbali mbali za maamuzi kama vile Bungeni, Baraza la Wawakilishi, Madiwani, Masheha nakadhalika.
Mradi huo unaotekelezwa na taasisi tatu Visiwani Zanzibar ambazo ni Jumuiya ya Utetezi wa Kijinisia na Mazingira Pemba (PEGAO) Chama cha Waandishi wa Habari Tanzania (TAMWA) Kanda ya Zanzibar pamoja na Chama cha Wanasheria Wanawake Tanzania (ZAFELA) na kuufadhiliwa na Ubalozi wa Norway Tanzani, ulioanzishwa Novemba 2020 na kutarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwaka 2023.
Kwa mujibu wa mratibu wa Jumuiya ya Utetezi wa Kijinisia na Mazingira Pemba (PEGAO) Bi. Dina Juma Makota, shebaha za mradi huo nikuwafikia wananchi 6000 Unguja na Pemba ambapo mpaka sasa tangu kuanzishwa kwa mradi huo kwa upande wa Kisiwa cha Pemba pekee jumla ya wananchi 6,895 wameshafikiwa ambapo miongoni mwa wananchi hao Wanawake ni 4,568 na Wanaume ni 2,327.
MAONI YA WANANCHI JUU YA MRADI W SWIL.
Mwandishi wa Makala hii alizungumza na baadhi ya wananchi ili kupata maoni juu ya dhahabu zinazotokana na Mgodi wa SWIL ambapo wengi kati ya wananchi hao walikiri kuwa mradi huo umeweza kuleta mabadiliko makubwa juu ya dhana ya wanawake na uongozi kwani ili umesaidia kuongeza idadi ya wanawake kuongezeka kwenye nafasi mbali mbali za uongozi ikiwemo viongozi wanawake kwenye vyama vya siasa na Serikali, Wawakilishi, Madiwani pamoja na Masheha.
Mkubwa Iddi Mohammed mwenye umri wa miaka 37 Mkaazi wa Msingini Chake
Chake amesema “Binafsi naufahamu mradi wa SWIL na ni miongoni mwa miradi ambayo imekuja kusaidia sana kutika kutoa elimu ya wanawake kupewa nafasi ya kushiriki katika mambo ya kijamii na uongozi mbapo hapo awali ilikuwa suala la uongozi hata wa kikundi cha hisa mwanamke alikuwa anaonekana hawezi au hafai lakini sasa tunoana idadi ya viongozi wanawake imeongezeka sana kuanzia kwenye Serikali, vyama vya siasa, kwenye vikundi vya kijamii nakadhalika”
ASASI ZA KIRAIA
Taasisi ya Tamwa-Zanzibar ni miongoni mwa taasisi kinara iliyobeba bango la utekelezaji wa mradi huo wa Uhamasishaji wanawake kushiriki katika Uongozi kwa upande wa vyombo vya Habari.
Kwa mujibu wa mratibu wa Tamwa Kisiwani Pemba Bi. Fat-hia Mussa Said amesema tangu kuanza kwa mradi huo wamefanikiwa kuwahamasiha wanajamii 2,194 ambapo miongoni mwa wanajamii hao wanaume ni 972 sambamba na kuwajengea uwezo Waandishi wa Habari 166 ambao wameweza kuandika Habari mbali mbali, Makala za uchambuzi, takwimu pamoja kuhamasisha masuala ya wanawake na Uongozi zinazofikia 1,588.
“Na jambo kubwa na la msingi ambalo tumelifanya ambapo kupitia mikutano ya kijamii ambayo tuliifanya na vyombo vya habari tumeibua wanawake mbali mbali mbali ambao wametamani kuiwa viongozi kuna wale ambao tayari wameshajiwekeza kwenye vyao lakini kuna wale ambao walikuwa hawaja wahi kuwa viongozi na tumewashawishi na tumewajengea uwezo na lengo letu ni kwamba ifikapo mwaka 2025 tuwe na wanawake wengi wawe tayari wameshajitengenezea mazingira ya kukubalika kuwa viongozi” alisema Mratibu wa Tamwa Kisiwani Pemba Bi. Fat-hia Mussa Said
Mratibu wa Jumuiya ya Utetezi wa Kijinsia na Mazingira Pemba (PEGAO) Bi. Dina Juma Makota, amesema tangu kuanza kwa mradi huo mwezi Novemba 2020 wameweza kuwafikia jumla ya Wananchi 6,895 ambapo miongoni mwa wananchi hao Wanawake ni 4,568 na Wanaume ni 2,327 idadi ambayo imeshapindukia kiwango cha idadi inayolengwa Unguja na Pemba.
“Mradi ulitakiwa kuwafikia watu 6,000 Zanzibar mzima lakini mpaka sasa kwa Pemba tayari tumeshafikisha watu 6895 hii inamaanisha kwa upande wa Kisiwa cha Pemba pekee tumeshapindukia idadi iliyopangwa kwa Zanzibar mzima, hii inatoa picha kuwa watu ambao wameshapata elimu ya uongozi Unguja na Pemba ni wengi mno na tayari tumeshatatua changamoto nyingi sana ambazo tumegundua kuwa ni vikwazo vinavyowafanya wanawake wakose muda wa kutosha wa kushiriki kwenye harakati za uongozi za kupitia wahamasishaji jamii wetu na ziko ambazo zinaendelea kutatuliwa na idadi ya wanawake waliohamasika na kutia nia ya kugombea nafasi mbali mbali za uongozi wameongezeka” Alisema
Mkurugenzi wa Jumuiya ya PEGAO Hifidh Abdi Said, amesema katika utekelezaji wa mradi huo wamegundua visiki mbali mbali amabvyo vinawakwamisha wanawake kutoshikiri ipaswavyo katika ulingo wa uongozi ambapo miongoni mwa visiki hivyo ni pamoja ukosefu wa elimu ya jumla na uongozi, Imani potofu za dini, ukosefu wa huduma bora za kijamii kama vile Maji, huduma za afya na barabara mambo ambayo huwafanya akina mama kutumia muda mrefu kufuata huduma hizo.
“Tumegundua changamoto nyingi sana zinazowakabili akina mama kukosa muda wa kushiriki mikutano mbali mbali na hiyo inatokana na kukosa muda wa kutosha kushiriki katika mikutano hiyo na harakati za siasa kwasababu anamkuta mwanamke tangu anaamka alfajiri anakabiliwa na majukumu ya kifamilia mpaka usiku ikiwemo kutembea masafa marefu kutafuta maji, huduma za afya barabara zenyewe mbovu kwahivyo hata akipata muda wa kupunzika hana tena uwezo wala hamu wakusema awaze kitu chengine cha kumuendeleza kimaisha” Mkurugenzi Pegao
KIKASHA (PACKAGE)
Ilinichukua wastani wa dakika 40 kutoka Mjini Chake Chake mpaka Shehia ya Kiuyu Minungwini na lengo la kwenda huko ni kukutana na Bi. Nasra Salum Mohammed ambaye ni Diwani wa Wadi ya Kiuyu Minungwini na mratibu wa Wanawake na Watoto na pia ni mnufaika wa mradi wa SWil.
Nje ya nyumba ya Bi. Nasra kumepangwa bustani za aina mbali mbali zilizosongamana mithili ya nywele za kimanga, nilibisha hodi mara tatu na kisha kukaribishwa alitoka nje mama wa makamo sio kijana sana wala kizee sana akiwa na umbo la wastani sio mfupi sana mfano wa dawa aina PIRITON wala mrefu mfano wa Gorofa ya Hong Kong ya China alinikaribisha na kukaribia na kisha tukaanza mazungumzo yetu.
Bi. Nasra alikiri kuwa mafunzo mbali mbali aliyoyapata kupitia mradi wa Uhamasishaji wanawake kushiriki katika Uongozi (SWIL) umempiga msasa kwa kiasi kikiubwa katika harakati zake za uongozi kwani mafunzo hayo yamemfanya atekeleze majukumu yake kwa ufanisi zaidi mithini ya rubani aliyebaba vichwa 300 vya wat una kuvitua salama ardhini baada kuruka angani kwa masaa kadhaa.
“Kusema kweli baada ya mradi wa SWIL kuja katika Shehia yangu nilifurahi sana kwasababu licha kuwa Diwani na Mratibu wa Wanawake na Watoto tangu mwaka 2016 lakini bado nilikuwa nahitaji elimu zaidi ili niweze kutekeleza majukumu yangu vizuri ziadi kwahivyo mradi wa SWIL umenisaidia sana kwani kuna mambo mengi sana nilikuwa siyajui lakini kupitia mradi wa SWIL nimeweza kuyajua ikiwemo namna bora ya kuripoti changamoto za kijamii kwa mamlaka husika ambazo zinawakwaza wanawake kushindwa kushiriki katika harakati za uongozi pamoja na kufahamu viashiria vya vitendo vya udhalilishaji, ukatili wa kijinsia na namna ya kukabiliana navyo” Bi. Nasra Salum Mohammed
Licha ya uwepo wa baadhi ya wanaume kutokuwaruhusu wake zao kushiriki katika nafasi za uongozi hali hiyo ni tofauti kabisa na kwa upande wa Bi. Nasra yeye amepata baraka zote kutoka kwa mume wake Bwana Bakari Abdalla Hamad sambamba chakufurahisha zaidi alisema hata baadhi ya nyakati hupata msaada wa mume wake pale inapobidi.
“Kwakweli kwa upande wa ruhusa kutoka kwa mume wangu namshukuru Mungu hana tatizo lolote na mimi ameniruhusu kwa moyo mkunjufu na wala hajawahi kusikia jambo lolote la kumvunjia heshima hata baadhi ya wakati ananisaidia maana naweza kupigiwa simu saa 6 usiku kuna tukio limetokea basi tunatoka wote maana usiku siwezi kutoka peke yangu”
Suala la uongozi kwa wanawake na majukumu ya familia ni miongoni mwa mwiba unaowachoma kila uchao lakini kwa upande wa Bi. Nasra kwake ni ni tofauti kwani yeye ameweza kuudhibiti muda mithili ya mvuvi anamvuta Samaki aliyemeza ndoano.
“Kuhusu majukumu ya kazi na familia ni namna ya kujipanga tu mwenyewe, majukumu ya familia nafanya mimi mwenyewe na kisha nafanya majukumu ya kazi mwenyewe na hakuna kinachonikwaza ukizingatia majukumu ya kazi hayana muda maalumu ni mimi mwenyewe ninavyojipangia, kwahivyo nawasihi wanawake wenzangu wasiogope kuwa viongozi kutokana na kukhofia majukumu yao kifamilia” Alisema
Bakari Abdalla Hamad ni mume wa Bi. Nasra alisema suala la mke wake kuwa Diwani na Mratibu wa Wanawake na Watoto kwake sio tatizo kwani anatekeleza majukumu ipaswavyo bila ya kuathiri ndoa yao na majukumu ya nyumbani ingawa kwa wanaume wengi imekuwa ni jambo zito kwao.
“Kwa upande suala la mke wangu kuwa kiongozi kwangu ni jambo la kawaida na nimemruhusu kwa nia safi kwasababu sina wasi wasi nae na mtu kama akiamua kukufanyi visivyo hata asiwe kiongozi anaweza kufanya, jambo la msingi ni kuaminiana na kuheshimiana mimi namuamini mke wangu na ananiheshimu na kila kitu kina kwenda vizuri, ni waombe tu wanaume wenzangu wasiwanyime wake zao ruhusa pindi wanapotaka kugombea nafasi za uongozi kwa kisingizio cha kwamba watasalitiwa au wataharibika kwani nao wana haki ya kuwa viongozi kama sisi wanaume” Mume wa Bi. Nasra
Ushuhuda kutoka kwa Bi. Nasra Salum Mohammed Diwani wa Wadi ya Kiuyu Minungwini na Mratibu wa Wanawake na Watoto ni tochi pekee inayotoa mwaga unaonesha jinsi mradi wa Uhamasishaji wanawake kushiriki katika Uongozi (SWIL) ulivyoweza kun’goa visiki ambavyo vilikuwa kikwazo kwa wanawake kushiriki katika nafasi mbali mbali za uongozi kabla ya mradi huo.
MAONI YA MHARIRI.
Mwandishi wa Makala hii anawaomba wadau na wafadhili wa utekelezaji wa mradi wa SWIL kuongeza muda wa miaka minne mengine ili kuwafikia wananchi wengi zaidi na lengo la SERA ya 50 kwa 50 kwenye vyombo vya kutunga Sheria liweze kufikiwa.
Comments
Post a Comment