USAWA WA KIJINSIA NAFASI ZA UONGOZI NDANI YA VYAMA VYA SIASA WALETA AHUWENI.

 

Takriban haki zote zilizoelezwa katika Mkataba wa kuondoa aina zote za Ubaguzi dhidi Wanawake zilizotambuliwa na kulindwa. Katika ya Zanzibar yam waka 1984 na Sheria nyengine mbali mbali kwa mfano kuna mabadiliko makubwa katika Sheria ya ajira Zanzibar, nambari 3 ya mwaka 2005 ambayo inampa haki na fursa sawa muajiriwa mwanamke.

 


Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania upande wa Pemba Katika chaguzi zilizopita kwa upande wa Pemba Wanawake kumi (10) waligombea nafasi mbali mbali, wawili kati ya hao waligombea ubunge kupitia viti maalum na wanne waligombea Uwakilishi kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Viti maalum, wanne Kaskazini Pemba na watatu Kusini Pemba na mmoja kupitia chama cha ACT Wazalendo.

 

Takwimu zinaonesha bado kuna ushiriki mdogo wa Wanawake katika Uongozi, ingawaje kwa sasa, Wanawake Zanzibar wamehamasika kutumia haki zao za Kidemokrasia mfano wapiga kura katika Uchaguzi Mkuu wa 2020, jumla ya 294,115 Wanawake sawa na asilimia 51% wameandikishwa kama wapiga kura ukilinganisha na 272,115 Wanaume waliondikishwa sawa na asilimia 49%.

 

Kwa namna hiyo, jumla ya Wanawake 216 kati ya 939 Wanaume sawa 20% walipitishwa na vyama vyao kuwa wagombea wa vyama vyao kwa nafasi tofauti wakiwemo 61 waligombea nafasi za Wawakilishi, 74 Madiwani 8 Ubunge, ambapo mchakato huo ni 37 pekee.

 

KATIBA YA ZANZIBAR KUHUSU USAWA WA KIJINSIA

 

Katiba ya Zanzibar ya mwaka ni 1984, kifungu cha 61(1) kimeeleza kuwa “Kutakuwa na wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wanawake kwa idadi ya asilimia 40% ya wajumbe wote wa kuchaguliwa katika majimbo ya Uchaguzi.

 

Takwimu zinaonesha kwa sasa asilimia ya wanawake inaongezeka siku hadi siku, katika baraza la wawakilishi la mwaka 2010-2015 ilikuwa ni asilimia 33% ya wajumbe wanawake, mwaka 2016-2020 ilikuwa ni asilimia 36% na kwa sasa 2020-2025 ni asilimia 39.7%.

 

Kwa mujibu wa takwimu hizi, inaonesha ni kwa jinsi gani usawa wa kijinsia unavyozidi kuongezeka kila awamu.

WANANCHI

 

Mwandishi wa Makala hii amezungumza na wananchi mbali mbali juu ya mada ya usawa wa kijinsia katika nafasi uongozi ndani ya vyama vya siasa ambapo wengi wao wamesema bado kumekuwa na uzingatiwaji mdogo kwa wanawake kupatiwa nafasi sawa na wanaume kuanzia ndani ya vyama vya siasa, Serikali na hata kwenye vyombo vya kutunga Sheria ikiwemo baraza ka wawakilishi na Bunge.

 

Ali Massoud Omar miaka 52, mkaazi wa Wawi Matrekta “Kiukweli licha ya kelele zinazopigwa na vyombo vya habari pamoja mashirika mbali mbali lakini bado suala la wanawake kukubalika kushika nafasi mbali mbali za uongozi bado ni tatizo licha ya kuwepo wanawake ambao ni viongozi wanaofanya vizuri akiwemo Rais Samia”

 

Hadija Sheha Omar miaka 45, mkaazi wa Vitongoji “Licha ya wanawake kutokukubalika katika kushika nafasi mbali mbali za uongozi lakini ukiangalia viongozi wanawake ndio wanafanya vizuri Zaidi kuliko hata hao wanaume, hivyo basi tuviomba vyama vya siasa, Serikali pamoja vyombo vya habari kulisemea kwa sauti pana suala la usawa wa kijinsia katika uongozi”

 

WANAWAKE WALIOWAHI KUGOMBEA NAFASI ZA UONGOZI

Aziza Ali Haji miaka 53 Mkaazi wa Mbuzini Jimbo la Ziwani Wilaya ya Chake Chake Mkoa wa Kusini Pemba ni mwanachama wa chama cha Mapinduzi CCM, ambaye kwa sasa ni katibu wa CCM jimbo la Ziwani alisema licha ya kuwa mwanachama wa muda mrefu katika chama chake cha hicho amewahi kugombea nafasi mbali mbali ikiwemo mwenyekiti wa tawi, katibu wa wadi, jimbo pamoja nafasi ya Uwakilishi katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2020 na kufanikiwa kupata kura 20 dhidi ya mshindani wake ambaye alikuwa mwanamme kupata kura 40 na kufanikiwa kushinda nafasi hiyo.

 

Alisema “Mimi ni mwanachama wa CCM tangu mwaka 1995 nikiwa na umri wa miaka 18 na niliwahi kugombea nafasi mbali mbali kuanzia nafasi ya tawi, wadi hadi jimbo na katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2020 niligombania nafasi ya ubunge na kufanikiwa kupata asilimia 50 ya kura dhidi ya mshindani wangu ambaye alikuwa mwanamme lakini nilichogundua ni kwamba bado kuna mifumu dume katika vyama vyetu vya siasa bado akina baba hawajawamini wanawake katika kushika nafasi mbali mbali za uongozi licha ya kukubali kuwa wanawake ni watendaji sana na waamini, rushwa ya ngono bado nalo ni donda ndugu katika kukatisha ndoto za wanawake kuwa viongozi”

 

Mkunga Hamad miaka 59 mkaazi wa Vitongoji Jimbo la Ole Wilaya ya Chake Chake mkoa wa Kusini Pemba, ni mwanachama wa ACT Wazalendo na Mgombea wa nafasi ya Ubunge katika Uchaguzi mkuu wa mwaka 2020, alisema suala la usawa wa kijinsia katika kugombea nafasi za kwenye vyama vya siasa ni suala ambalo limechukua sura mpya katika miaka ya hivi karibuni ukilinganisha na zamani ambapo sasa wanawake wanapewa kipaumbele katika vyama vya siasa licha ya kuwepo kwa baadhi ya wanajamii ambao bado wanaulewa mdogo juu ya suala wanawake kushika nafasi za uongozi jambo ambalo linachangia kufifisha ndoto za wanawake kuwa viongozi.

 

“Kwa upande wangu mimi nadhani sasa hivi ni tofauti sana tukilinganisha na miaka ya nyuma huko ambako mwanamke ilikuwa ni mwiko hata kujiingiza katika mambo ya siasa kwa dhana iliyokuwepo kuwa mambo ya siasa na uongozi yanawahusu wanaume peke yao, kiasi kwamba kama uko kwenye chama na kuamua kugombea nafasi Fulani unaanza kupata vikwanzo kuanzia kwenye chama, jamii n ahata familia kwa ujumla, lakini hii hali hiyo imeanza kupungua sana sasa hivi wanawake tuko huru kujiingiza katika mambo ya kisiasa na tunagombania nafasi mbali mbali za uongozi, tunateuliwa lakini pia tunafanya vizuri sana kushinda hata hao wanaume kwa mfano mimi katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2020 nilgombea na nikafanikiwa kushika nafasi ya pili, kwahivyo hii inadhirisha kuwa suala la usawa wa kijinsia katika nafasi za uongozi kwenye vyama vya siasa kwa sasa liko vizuri"

 

KATIKA YA CHAMA CHA MAPINDUZI CCM.

 

Katibu wa Chama Chama cha Mapinduzi CCM Walaya ya Mkoani Nicholaus Samson Chibwana, alisema Katiba ya Chama cha Mapinduzi CCM kimezingatia ipaswavyo usawa wa kijinsia katika kugombea nafasi mbali mbali za uongozi pamoja uteuzi na kutolea mfano nafasi 100 za Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) ambapo wateule wa nafasi hizo wanaweza kugombea nafasi ya Ubunge katika majimbo yao.

 

Alisema “Katiba ya Chama Cha Mapinduzi CCM kimezingatia ipaswavyo suala la Usawa wa kijinsia ndani ya chama katika ngazi mbali mbali kwa mfano tukiangalia kanuni za uongozi na maadili ya chama na jumuiya zake fungu la kwanza ibara ya 2 ya muundo wa kamati za usalama wa maadili ngazi ya Wilaya ambao ni Mwenyekiti wa Wilaya, Katibu wa Wilaya na wajumbe 3 wa kamati ya Siasa ambao kwa msisitizo kabisa kwamba ndani yake jinsia zingatiwe, kwahivyo kaamti zetu za maadili kwa ngazi zote hakuna kamati ya maadili ambayo haijazingatia jinsia, lakini pia wajumbe 2 watakuwa ni wazee ambapo mjumbe 1 atakuwa mwanamke na 1 atakuwa mwanamme, lakini ukienda kwenye kanuni za uchaguzi wa wa CCM ibara ya 56 utaratibu wa wajumbe wa halmashauri kuu ya wajumbe 10 utazingatia mgawanyo na utaratibu wa chama kutakuwa na wagombea wa nafasi 4 kwa ajili ya wanawake na nafasi 4 kwa ajili ya vijana ambapo katika hizo nafasi 4 za vijana suala la jinsia limezingatiwa  na nafasi 2 ni wagombea wa nafasi za wazazi ambapo kutakuwa na mwanamke mmoja na mwanamme mmoja, aidha katika kanuni za uteuzi kugombea uongozi katika vyombo vya dola bunge letu sisi lina wabunge 393 sisi CCM kwa makusudi kabisa ukienda kwenye ibara ya 17 ambayo ikiangalia mgao wa wabunge wanawake kwa mkoa na makundi maalumu kifungu kidogo cha 2 kinasema kutakuwa na jumla ya nafasi 100 za wanawake za katika bunge la jamhuri wa Muungano na wanawake hao hao  wanaruhusiwa kugombea kwenye majimbo" 

 

KATIBA YA ACT WAZALENDO

 

Ali Juma Omar, Mwenyekiti wa ACT Walendo Mkoa wa Kaskazini Pemba, alisema Sheria nambari 8 ibara ya 2 ya Katiba ya chama cha ACT Wazalendo imefafanua juu usawa na haki sawa kwa wanachama wote ndani ya chama kuanzia ngazi ya tawi hadi taifa, hivyo basi wanawake wakiwa ni sehemu ya wanachama hao wamepewa haki sawa na wanaume ya kugombea nafasi mbali mbali za uongozi pamoja kuteuliwa kwenye nafasi za juu za chama.



Alifafanua"Kwahivyo Katiba ya Chama cha ACT Wazalendo kimezingatia kwa kiasi kikubwa sana suala la usawa na haki ya kijinsia katika nafasi mbali mbali za uongozi, kwa mfano ukiangalia kwa sasa Makamo mwenyekiti wa ACT Wazalendo taifa ni mwanamke hii inamaanisha kuwa katika chama chetu hakuna ubaguzi wa kijinsia wanachama wote ni sawa mbele ya sheria na wanahaki ya kushika nyadhifa zote kwa mujibu wa Katiba yetu"

suala la usawa kijisia kwenye vyama vya siasa, mashirika pamoja Serikali kwa ujumla ni suala linapigiwa chapuo sana na wadau mbali mbali wanaopenda kuwaona wanawake wanapewa kipaumbele katika vyombo mbali mbali vya Kutunga Sheria ikiwemo Bunge, Baraza la Wawakilishi pamoja nyadhifa za juu za Serikali. 

 

Comments

Popular posts from this blog

MWALIMU WA MADRASA MBARONI KWA TUHUMA ZA KUMBAKA MWANAFUNZI WAKE

Mama ajifungua kisha kukiua kichanga na kukifukia kwenye tuta- Sizini Pemba

Mtangazaji wa Wasafi Media, Dida Afariki Dunia