Uhaba wa Viwanja Vya Michezo wadumanza vipaji vya watoto wa kike katika kushiriki michezo.
MAKALA NA, SALIM HAMAD,
PEMBA
Katika tasnia ya Michezo
katika Kisiwa Cha Pemba,kumekuwa uhababa wa Viwanja jambo linalochangia
wanawake kushidwa kutoshiriki katika harakati za michezo kutokana na
kutokuwepo kwa mazingira rafiki ya kufanyia mazoezi.
Maranyingi inaeleka kwamba
wadu wengi wa Michezo wamekuwa wakiangalia na kuelekeza Nguvu zao kwenye
michezo mingine kama Mpira wa Miguu lakini kwenye mchezo wa Valbal Basketi Ball
imekuwa ikiwekwa Pembeni.
Sudi Saaduni ni Meneja wa
timu ya Wete Star,aliomba Serekali kuangalia uwezkano wa kujenga Viwanja vya
Michezo inayohusina na michezo ya wasichana ili na wao wapate fursa za
kushiriki michezo kwani michezo ni afya na ni ajira.
Alisema wakati Viwanja
Vipatakapo Jengwa wanawake watahamasika kujiingiza kwenye michzo kwa vile
tayari kutakuwa kumeshawekwa mazingira rafiki katika kwenye Viwanja vya
Michezo.
‘’Unajua uhaba wa Viwanja
wa Michezo Bado Pemba,nishida jambo hili linawafanya wanawake kutoshiriki
michezo kwa kukosekana maeneo maalumu ya kufanya mazoezi na kuomba Serekali
wakati ikijnga Viwanja iangalie na michezo ya akina mama isiangalie tu mpira wa
Miguu’’alisema Sudi.
Hata hivyo alisema mbali
ya Changamoto ya Viwanja kuna Changamoto ya uhaba wa Kifedha pia jambo hilo ni
kikwazo kwa wanawake katika kuzifikia ndoto zao walizojiwekea.
Alisema timu yao imekuwa
ikishiriki michuano y ligi Kuu ya Zanzibr ,kwa upande wa Valbal lakini kwa
zaidi ya misimu miwili imekosa kushiriki kwa kukosa fedha za kujiendeshea.
Alisema wakati timu
ikiingia kwenye mashindano kuna ghara za kufanya mazoezi na kuipeleka timu
kwenye mchezo jambo hilo limekuwa likiwakwaza katika kuendeleza Vipaji vya
akina mama.
Alisema timu hiyo
ilishashiriki ligi kuu ya Zanzibar,kwa zaidi ya Misimu mitano na kufanya Vizuri
lakini katika msimu uliopita walishindwa kushiriki kutokana na ukata wa kifedha
unaojitokeza kwenye Clabu hiyo.
Hata hivyo aliomba
Serikali kuangalia uwezekano wa kuweka bajeti ya kuanzishi timu za michezo kwa
wasichana na kuziendeleza ili kutoa fursa kwa jinsia zote akiamini vijana wengi
wanaweza kujiendesha kimaisha kupitia michezo kama nchini nyengine.
Tatu Abdalla Khamis ni
Mchezaji wa timu ya Wete Star katika mchezo wa Valbal alisema bado mazingira
sio rafiki kwao na jambo hili linawafanya akinamama wengi kutowaruhusu watoto
wao kushiriki michezo kwa kuona hakuna maeneo rasmi ya michezo hiyo.
Alisema wapo baadhi ya
akina mama wanauwezo mkubwa wa kuendeleza Vipaji Vyao lakini wamekuwa
wakishindwa mana wakipata sehemu ya mazoezi wanashidwa kwenye uwezeshaji jambo
la msingi ni Serikali kunagalia mana ya kuboresha michezo kwa pande zote na sio
tu kuangalia mpira wa Miguu.
Alisema haiwezekani
walishapiga hatua ya kushiriki hata michuano ya ligi Kuu lakini wanashindwa
kujiendeleza kwa vile hakuna msaada wa kifedha jambo hilo pia ninarudisha nyuma
juhudi zao.
‘’tukiangalia maeneo rasmi
ya kufanyia mazoezi mara tuende huku bado tunashidwa na maeneo sahahi ya
kujiendeleza Vaji vyetu ,akiachana na shida hiyo pia ukata wa kifedha pia ni
tatizo tunashidwa hata kushiriki kwenye michuano ya ligi ‘’alisema.
Alisema Kiwanja maarufu ni
kimoja pale Wete na kuna timu nyingi zote zinaania kiwanja hicho sasa kama
Serikali haikungalia jambo hili kwa karibu vipaji vya akina mama vitashinda
kuimarika.
Katika kipindi Cha hivi
karibuni Rais wa Zanzibar,na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dokta Husein Ali
Mwinyi ktika hutuba zake kwenye majukwaa
alisema katika Serikali ya awamu ya Nane imeelekeza Nguvu zake katika michezo
kwa ujenzi wa Viwanja vya Michezo ili kuona kila mmoja anapata nafasi ya
kushiriki michezo.
Alisema anatambua michezo
ni afya na ni ajira na ndio maana sasa Serekali ipo katika mpango wa ujenzi wa
Viwanja Kila Wilaya za Unguja na Pemba,kwa lengo la kutoa fursa sawa kwa
wanawake na wanaume katika Nyanja zote.
‘’Serikli ya awamu ya Nane
itahakikisha inajenga Viwanja Vya Michezo kila Wilaya natambua Changamoto za
uhaba wa Viwanja hivyo kutakuwa na bajeti maalumu ya ujenzi na tunatunapambana
kutafuta wafadhili watakaotusaidia katika kufanikisha mpanga huo’’alisema Dk
Mwinyi.
Alisema katika Uongozi
wake kwenye Sekta ya Michezo ni moja
katia ya Vipaumbe vyake akiamini kwamba michezo ni afya kwa kuondosha maradhi
mbali mbali na inaongeza ufahamu hasa kwa wanafanzi na kufanya vizuri kwenye
mitihani yao.
Comments
Post a Comment