Msichana mwenye ulemavu wa viungo apewa ujauzito.
Na, Salim Hamad Pemba. Mama Mzazi wa Msichana mwenye ulemavu wa Viungo na akili jin limehifadhiwa mkaazi wa kiuyu Mbuyuni Wilaya ya Micheweni Mkoa Kaskazini Pemba, ameomba Serikali na wadau wa kupinga vitendo vya udhalilishaji kumsaidia ili haki iweze kutendeka kutokana na kitendo cha mtoto wake kupewa. Akizungumza kwa masikito Mama huyo alisema mtoto wake huyo anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 20 alikuwa hana tabia ya kutoka nje lakini akamuona mtoto wake huyo anapatwa na uchungu na kujifua. Alisema walikuwa hawajabaini chochote mshichana huyo kuwa anaujauzito walifikiri kuwa tumbo alilokuwa nilakawaida hata walipokujashtuka tayari kashakuwa karibu na kujifungua. Alisema hali hiyo ilimpa huzuni kubwa kwa kudhalilishwa mtu huyo mwenye ulemavu aliyekuwa haweze kumfahamu aliyemfanyia kitendo hicho. ‘’Kitendo hichi kimenisikisha sana cha mwanangu Mlemavu kupwa ujauzito na kimenishangaza kitendo hichi kwani mtoto wangu huyo hana tabia ya kutoka nje’’alieleza Mama ...