Timu ya wanawake ya Velleyball na Basketball Pemba, yajipanga na mashindano ya Umitashumta.
Na, Salim Hamad, Pemba
Timu ya Wanawake ya Mchezo wa Volleyball
na Basketball Kisiwani Pemba,ipo katika mchakato wa kujiandaa ya Michuano ya
Umoja wa Shule za Msingi Tanzania (UMITASHUMTA) inayotarajia kuanza hivi
karibuni Mkoani Tabora.
Akizungumza na Mwandishi wa Habari
hizi Mratibu idara ya Michezo Pemba,Mzee Ali Abdalla alisema Mashindano hayo
yanashrikisha timu mbali mbali kutoka mikoa ya Tanzania Bara na Visiwani.
Alisema Michuano hiyo hufanyika kila
mwaka na kushirikisha michezo tofauti ikiwemo Volleyball, Basketball kwa wanawake
na Fotball na Riadha kwa Upande wa Wanaume.
Alisema timu za wasichana zimekuwa zikifanya
Vizuri kwenye Mashindano hayo licha ya kuwepo kwa ushindani wa hali ya juu
kutokana na timu za Tanzania bara na wao kuwania ushindi wa mashindano hayo lakini
nazo zimekuwa zikipambana.
Alisema ingawa wachezaji wanapofika
kule wanapata changamoto ya hali ya hewa kutokana badiri kwenye mikoa hiyo
lakini wamekuwa wakipambana na kupata matokeo mazuri.
Alisema katika kipindi cha Mwaka jana
timu hiyo ya wanawake kwa upande wa Volball ilishika nafasi ya pili baada ya
kuzichapa timu mbali mbali za mikoa ya Tanzania Bara.
‘’Mashinadno haya ya UMITASHUMTA kwa
upande wa Shule za Msingi Tanzania na UMMISETA kwa upande wa Shule za Sekondari
Tanzania yamekuwa yakifanyika kila mwaka ambapo timu hii ya wasichana ya mchezo
wa basket Ball na Voll Ball imeanza maandalizi ya kujiandaa na michuano hiyo’’alisema
Mzee.
Hata hivyo Mzee alisema Mashindano
hayo yapo Chini ya Wizara ya Elimu yakiwa na lengo kufufua vipaji na
kuviendeleza vipaji Vilivopo Mashuleni Tanzania.
Kwa upande wake Mmoja wa Washiriki wa
Mashindano hayo Fatma Said wanajipanga kuhakikisha warejesha ushindi Kisiwani
Pemba,ili kuijengea sifa Zanzibar, kwa kufanya Vizuri kwenye mashindano hayo
makubwa.
MWISHO.
Comments
Post a Comment