Skip to main content

WANAWAKE WASHAURIWA KUUNGANA MKONO KUFIKIA 50% KWA 50%

Na, Ahmed Abdulla.

LICHA ya kuwa wapiga kura wengi wanawake lakini cha kushangaza wanawake wanaposimama kuomba kura ya kushika nafasi za uongozi ndani ya majimbo ikiwemo Ubunge, Uwakilishi ama udiwani hawaungwi mkono na wenzao.


Hali hiyo sijui inachangiwa na kitu gani kama choyo ama kutopendana baina ya wanawake kwa wanawake au kuangalia maslahi yao binafsi bila ya kuwajali wananchi wao kimaendeleo.


Kwa mfano tukiangalia uchaguzi wa mwaka 2020 hapa Zanzibar wanawake waliogombea uwakilishi walikuwa 61 na walioshinda walikuwa wanane, kwa nafasi za ubunge wanawake waliogombea walikuwa 81 walioshinda wanne na upande wa udiwani wanawake waliogombea walikuwa 74 na walioshinda 25.


Kwa mujibu wa takwimu hizo inaonesha wazi kwamba bado jitihada zaidi zinahitajika kwani kundi hilo bado liponyuma katika kupata nafasi hizo.


Kutokana na hali hiyo ipo haja kwa wadau wa maendeleo na taasisi zinazojali maslahi ya wanawake kuliangalia suala hili kwa kina ili kubaini sababu ya wanawake kutoungwa mkono pale wanapogombea nafasi hizo ukizingatia kuwa wao ndio wapiga kura na wafanyaji wazuri wa kampeni katika kuwapitisha wanaume.


Akizungumza hivi karibuni na Makala haya Mwakilishi mstaafu wa Jimbo la Magomeni Hafsa Said Khamis, aliwataka wanawake watakapopata nafasi za uongozi kuangalia zaidi maslahi ya wananchi ili kufikia malengo ya kugombea nafasi hizo.


Alisema lengo la kugombea nafasi hizo ni kuwaletea maendeleo wananchi na sivinginevyo hivyo ni vyema kutekeleza hayo kwa vitendo ili kuweka mazingira na ustawi mzuri kwa wananchi.


Alifahamisha kuwa wananchi wamekuwa wakikabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo uhaba wa miundombinu ya elimu, afya, maji safi na salama, barabara, umeme na huduma nyengine ambazo viongozi wa majimbo wananafasi kubwa ya kutatua changamoto hizo.


Mbali na hayo aliwataka wanawake kushirikiana pamoja bila ya kuzingatia vyama wanavyotoka hatua ambayo itasaidia kuwa na idadi kubwa ya viongozi wanawake.


Nae Mwakilishi mstaafu wa Jimbo la Amani Fatma Mbarouk Said, aliwataka wanawake wasijiweke nyuma na badala yake ni vyema kusimamakidete katika kugombea nafasi hizo kwasababu hii ni demokrasia hivyo kila mtu anauwezo wa kugombea nafasi anayotaka.


Aliwasisitiza kuhamasishana na kupeana nguvu pale wanapojitokeza kugombea nafasi hizo kupitia ngazi mbalimbali.


Alifahamisha kuwa hatua hiyo itasaidia kuongezeka kwa idadi ya wanawake katika vyombo vya maamuzi na kuweza kupambana na mfumo dume wa kiutawala na kuchochea upatikanaji wa maendeleo katika maisha yao.


Nae kiongozi wa dini ukhit Amina Salum Khalfan alisema dini haijakataza wanawake kugombea nafasi mbalimbali za uongozi na badalayake kuna mipaka kwa baadhi ya mambo.


Alisema ni vyema wanawake kushikamana na kushirikiana katika kuhakikisha wanafikia malengo ya kuwa viongozi kwa mustakbali wa kuleta maendeleo kwa wananchi.


Alisema jambo la msingi kila mmoja kumuheshimu mwenziwe iwe mwanamke ama mwanamme kwani wote wanaweza kuwa viongozi na wakaleta maendeleo kwa wananchi.


Jamii lazima ifahamu kwamba dini ya kiislamu haikumkataza mwanamke kuwa kiongozi hivyo ni vyema jamii imkubali na kumuunga mkono mwanamke pale anaposimma kugombea nafasi na dini sio kikwazo cha kumfanya mwanamke asiweze kuongeza,alisema.


Kwa baadhi ya wanawake kutoka vyama mbalimbali vya siasa ambao wanamalengo ya kuwa viongozi majimboni, walisema lazima kuwe na mkakati wa kwa wanawake kupendana wenyewe kwa wenyewe ili kusaidia kupata nafasi hizo.


Miongoni mwa wanawake hao Halima Abdalla kutoka chama cha ADA TADEA, alisema hapo awali wanawake walikuwa wakiogopa kugombea nafasi za uongozi lakini baada ya kupatiwa mafunzo mbalimbali hivisasa wamehamasika na wapo tayari kujitokeza katika kushika nafasi mbalimbali za majimboni.


Hivyo alitumia fursa hiyo kuwaomba wadau na taasisi mbalimbali zinazohtaji maendeleo ya mwanamke kuendelea kuwapatia mafunzo wanawake mara kwa mara na mbinu za kukabiliana na vikwazo vyote viliyopo katika uchaguzi ili waweze kuwa jasiri na kusimamaimara mwaka 2025 kuingia katika kinyang'anyiro cha kuwania kuongoza majimbo.


Saada Shaibu Ahmada kutoka chama cha ACT Wazalendo, alisema washajiandaa kuona wakati ukifika kugombea nafasi hizo na kuahidi kufuata nyayo za wanawake waliokuwa viongozi majimboni ili waweze kushika nafasi hizo kwa lengo la kuwaletea maendeleo wananchi kupitia nyanja mbalimbali.


Catherina Paskal Mgoli kutoka CCM, alisema licha ya wanawake hivi sasa kuhamasika na kuwa tayari kugombea nafasi hizo lakini changamoto kubwa inayowakabili ni hali za kiuchumi kutokana na asilimia kubwa ya wanawake uchumi wao mdogo haliambayo inasababisha kukosa kushindwa nafasi za majimboni kwasababu harakati za uchaguzi zinahitaji fedha kuanzia uchukuaji wa fomu na mzunguko mzima wa kampeni.


Kutokana na uwezo wetu wa fedha mdogo hata kama tukitaka na tunataka lakini kinachoturejesha nyuma fedha hatuna zakutuwezesha kutekeleza malengo yetu, hivyo tunawaomba wadau wa maendeleo ikiwemo tamwa na wengine wasiishie kutupa mafunzo bali watushike mkono pia kupitia harakati zote za uchaguzi kuanzia mwanzo hadi mwisho ili kutuwezesha kufikia malengo yetu,walisema.


Ghanima Omar Sultan kutoka chama cha CUF, alisema licha ya kuhamasishwa wanawake kushiriki katika nafasi za uongo lakini bado asilimia kubwa ya wanawake uwezo wao kiuchumi mdogo.


Alisema kutokana na hali hiyo ni vyema kuwezeshwa kiuchumi, hasa kupitia asilimia ambazo zimetengwa kwa ajili yao ni vyema kupatiwa ili ziwasaidia katika shughuli mbalimbali za kimaendeleo ikiwemo masuala ya kisiasa, ujasiriamali na shughuli nyengine ili kuinua uchumi wao.


"Kuna asilimia kumi zilizotengwa na Halmashauri ambazo hivi sasa zimehamishiwa wizara ya Uwezeshaji, asilimia kubwa ya wanawake hawazifahamu fedha izo njia ya kuzipata, hivyo kunaumuhimu wa kufatiliwa ili kuweza kuwasaidia,"alisema.


Naima Salum Hamad kutoka chama cha UDP, alitumia fursa hiyo kuviomba vyama vya siasa kuwa na mifumo rafiki kwa wanawake kujitokeza katika kugombea nafasi hizo nasio kuonekana wanaume pekee ndio wenyeuwezo wa kugombea na kushika nafasi hizo.


Mratibu wa mradi wa kuimarisha wanawake kushika nafasi za uongozi kutoka Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA-ZNZ), Maryam Ame Chum, alisema taasisihiyo imekuwa ikisimamia mradi huo ili kuwajengea uwezo wanawake kushika nafasi hizo na kuweza kuwa na idadi kubwa ya wanawake kuingia katika ngazi za maamuzi.


Alisema hatua hiyo itasaidia kuondosha changamoto mbalimbali kwa wanawake na kuweza kupata haki zao kwa haraka.


Alisema tamwa mbali ya kuwapa mafunzo hayo lakini pia kama hali itaruhusu wanamalengo ya kuwa nao bega kwa bega hadi pale watakapoweza kufanikisha ndoto zao.


TAMWAZNZ, ZAFELA na PEGAO kwa pamoja zinatekeleza mradi wa kuwawezesha wanawake kushiriki katika nafasi za uongozi (SWIL), mradi ambao unaf

adhiliwa na Ubalozi wa Norway.

Comments

Popular posts from this blog

MWANAMKE AJINYONGA, SABABU WASI WASI - PEMBA

NA, HASSAN MSELLEM - PEMBA PICHA KUTOKA MAKTABA Mwanamke aliyefahamika kwa jina la Raya Darusi Abdallla miaka 48, mkaazi wa Mbuzini Wilaya ya Chake Chake Mkoa wa Kusini Pemba, amefariki Dunia kwa kidaiwa kujinyonga kutokana na Msongo wa mawazo. Tukio Hilo limetokea Novemba 30.2025 saa 11 alfajiri huko Mbuzini Wilaya ya Chake Chake Mkoa wa Kusini Pemba. Omar Salum Ali, ambaye ni shemeji wa marehemu amesema kabla ya marehemu alikuwa na sumbuliwa na Msongo wa mawazo kutokana na kumpoteza kaka yake ambaye alifariki hivi karibuni, kugundulika kuwa ana maradhi ya sukari, mtoto wake wa kiume wa miaka 25, kuwa na ugonjwa akili hali iliyopelekea kupatwa na Msongo wa mawazo na kuamua kujinyonga. Katibu wa Sheha (Katibu wa Mwenyekiti) Shehia ya Mbuzini Yakub Ali Msabah, amesema alipata taarifa za tukio Hilo kutoka kwa Sheha wa Mbuzini kuhusu tukio baada ya kufika eneo la tukio waliukuta mwili wa Mama huyo ukiwa unanin'gia kwenye dari ya Nyumba ambayo alikuwa anaishi zamani. Kutoka tarehe 18 ...

Mariam Muhene – mfano wa kuigwa kwa wanawake kwenye ulingo wa siasa ni

MAKALA NA, HASSAN MSELLEM -PEMBA Tangu Tanzania iruhusu mfumo wa vyama vingi mwaka 1992, Mariam Muhene alijiunga na chama cha Civic United Front (CUF) ambapo mwaka 1995, aligombea nafasi ubunge wa viti maalumu na kuvuka hatua zote ikiwemo kula kiapo mahkamani lakini hakufanikiwa kukikalia kiti hicho. “Mwaka 1995 niligombea ubunge wa viti maalum na nikapita kila kipengele mtu wa kwanza wilaya, taifa bodi ya uongozi, nikala kiapo mahkmanai lakini katika nafasi mbili zilizoletwa kwa kila mkoa Kusini na Kaskazini Pemba mimi sikubahatika” amesema  Safari yake ya kisiasa za upinzani iliendelea na mnamo mwaka 2000, aligombea nafasi ya ubunge wa kuchahguliwa kupitia chama cha Allience for Democratic Change (ADC) Jimbo la Chake Chake lakini kutokana na changamoto zilizojitokeza ikiwe mawakala wa Chama chake kutokuruhisiwa kuingia kwenye vya kupiga kura jambo ambalo amesema lilichangia kukosa nafasi hiyo. Kwasasa Mariam Mohammed Muhene anashika nafasi ya Kamishna wa ADC kanda ya Pemba, nafas...

WATOTO KUJINYONGA ZANZIBAR, UTAFITI WAHITAJIKA.

HABARI NA, HASSAN MSELLEM, PEMBA Picha kutoka mtandaoni Visa vya watoto kujinyonga vimeanza kuwatia khofu na mashaka wazazi na walezi katika Visiwa vya Unguja na Pemba. Mashaka na khofu hiyo imeibuka baada ya matukio mawili mfululizo ya watoto wawili mmoja akiwa umri wa miaka (5) na mwengine (9) kuripotiwa kufariki dunia kwa kujinyonga kati ya tarehe 7 na 9 mwezi huu wa kumi mwaka 2025 kupitia kipindi cha Mawio kinachorushwa na Shirika la Utangazaji Zanzibar ZBC kila siku kuanzia saa 12:40 asubuhi. Katika tukio la kwanza mnamo tarehe 7.10.2025 mwandishi Masanja Mabula aliripoti tukio la Fatma Omar Kidere mwenye umri wa miaka tisa (9) mkaazi wa Mtondoo Jeuri Makaangale Wilaya ya Micheweni Mkao wa Kaskazini Pemba, amekutwa amefariki dunia na mwili wake ukiwa unanin’ginia kwa kutumia mtandio Jirani wa marehemu aliyefahamika kwa jina la Khamis Ali, amesema amepata taarifa za tukio hilo akiwa kazini baada ya kupigiwa simu na mke wake kumpa taarifa za kutokea kwa tukio hilo na kuondoka kazin...