Msichana mwenye ulemavu wa viungo apewa ujauzito.
Na, Salim Hamad
Pemba. Mama Mzazi wa Msichana mwenye ulemavu wa Viungo na akili jin limehifadhiwa mkaazi wa kiuyu Mbuyuni Wilaya ya Micheweni Mkoa Kaskazini Pemba, ameomba Serikali na wadau wa kupinga vitendo vya udhalilishaji kumsaidia ili haki iweze kutendeka kutokana na kitendo cha mtoto wake kupewa.
Akizungumza kwa masikito Mama huyo alisema mtoto wake huyo anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 20 alikuwa hana tabia ya kutoka nje lakini akamuona mtoto wake huyo anapatwa na uchungu na kujifua.
Alisema walikuwa hawajabaini chochote mshichana huyo kuwa anaujauzito walifikiri kuwa tumbo alilokuwa nilakawaida hata walipokujashtuka tayari kashakuwa karibu na kujifungua.
Alisema hali hiyo ilimpa huzuni kubwa kwa kudhalilishwa mtu huyo mwenye ulemavu aliyekuwa haweze kumfahamu aliyemfanyia kitendo hicho.
‘’Kitendo hichi kimenisikisha sana cha mwanangu Mlemavu kupwa ujauzito na kimenishangaza kitendo hichi kwani mtoto wangu huyo hana tabia ya kutoka nje’’alieleza Mama huyo.
Sheha wa Shehia ya Shanake Kiuyu Ali Hamad Sharifu alisema baada ya kupata taarifa ya hiyo aliifkisha kwa Serikali ya Wilaya hiyo ili kuona hatua stahiki zinachukuliwa kwa alidaiwa kufanya kitendo hicho.
‘’Mimi nilipokea taarifa kutoka kwa wazazi wa Msichana huyo mwenye ulemavu amepewa ujauzito na tayari Alishajifungua ingawa matokea haya tumekuwa tukiyakemea lakini bado yanaendelea kujitokeza’’alisema.
Mkuu wa Wilaya ya Micheweni Mgeni Khatib Yahya alilaani kitendo hicho na kueleza kuwa Serikli itaendelea kuchunguza alifanya tukio hiyo ili aweze kuchukuliwa hatua kali za kisheria.
Hata hivyo Mkuu huyo wa Wilaya aliwata Wazazi hao kuwa makini na kuacha kuwaamini wengine kukaanaye kwani kuna baadhi wamekosa ubinadamu na kutenda Vitendo hivyo.
‘’Nalaani kitendo hichi mtu kama huyo Mlemavu anafanyiwa udhalilishaji anapewa ujauzito ukweli jambo hilo linaumiza sana tutaendelea kufutilia kufahamu alifanya kitendo hichi ili tuweze kuchukua hatua kali dhidi yake’’alisema DC Mgeni’’alisema.
Hata hivyo aliwataka wazazi hao kutoa mashirikiano ya dhati pindi atakapobainika na kupelekwa kwenye Vyombo vya Sheria wasije kubali kufanya suluhu na kuahidi kuisimamia kesi hiyo hadi mtuhumiwa aweze kutiwa hatiani.
MWISHO.
ReplyForward |
Comments
Post a Comment