Wanawake waongoza, Tunzo waandishi YMF.

 Habari Na, Ahmed Abdulla.

Chama cha waandishi wa habari wanawake Tanzania, TAMWA Zanzibar kimewatunuku vyeti waandishi chipukizi ishirini na nne (24) waliohitimu mafunzo ya kuandika habari za wanawake na Uongozi.


Hafla hiyo ya kuwatunuku vyeti iliofanyika ukumbi wa Bima ulioko Mperani mjni Unguja iliohudhuriwa na wahariri, wadau wa habari pamoja waandishi wa habari kutoka Zanzibar.


Mapema Kaimu Afisa Mradi wa kuwajengea uwezo waandishi chipukizi (YMF) kutoka TAMWA ZNZ Khayrat Haji amesema jumla ya vipindi na Makala 347 kati ya 348 zilikusanywa ikiwemo radio 117, magazeti 47 na mitandao ya kijamii183 zilizojikita katika ushiriki wa nafasi za Uongozi kwa wanawake.


Tumekuwa na program hii kwa kuimarisha nafasi za Uongozi kwa wanawake kwa kutumia vyombo vya habari ambapo waandishi chipukizi (24) wamepatiwa mafunzo yenye kuakisi mabadiliko chanya katika jamii, Khayrat Haji, Kaimu Afisa Mradi.


Kwa upande wake Mkurugenzi wa Chama cha Waandishi wa habari Wanawake Tanzania, TAMWA ZNZ Dk Mzuri Issa amesema waandishi chipukizi wamesaidia jamii kujua haki zao za msingi hasa wanawake na kuongeza idadi ya washiriki katika ngazi za maamuzi.


“Wanawake wengi wamekuwa na muamko baada ya kutambuwa haki zao, matarajio yetu katika uchaguzi mkuu 2025 wanawake watajitokeza wengi katika majimbo kugombea nafasi za Uongozi, Dk Mzuri Issa, Mkurugenzi TAMWA ZNZ.


Mjumbe wa Bodi TAMWA ZNZ Hawra Shamte amewasihi waandishi wa habari chipukizi kufanya kazi kwa malengo na kufata miiko na maadili ya Tasnia ya habari kwa kufanya kazi na jamii kwa lengo la kuleta mabadiliko nchini.


“Waandishi ni daraja kati ya Viongozi na jamii, pia ni mdomo wa kuwasemea wasiokuwa na sauti hivyo kutumia nafasi hiyo kwa kujitoa na kusaidia jamii, Hawra Shamte, Mjumbe wa Bodi TAMWA ZNZ.


Shifaa Said Hassan Jaji Kiongozi kati ya watatu katika Tunzo waandishi wahabari chipukizi kupitia mradi wa kuimarisha nafasi za Uongozi kwa wanawake kupitia vyombo vya habari amesema katika kazi hiyo wameangalia vigezo muhimu kama vile Uweledi na umahiri wa Uandishi, matumizi sahihi ya lugha, pamoja na upekee wa mada.


“Makundi ya watu wenye mahitaji maalum bado hatujayatendea haki tumeyasahau ni vyema tukajikita kuyafanyia kazi ipasavyo katika habari tunazoandika, Shifaa Said, Jaji Kiongozi.


Meneger kutoka Radio Jamii Mkoani Said Omar amesema mafunzo yanayotolewa na Chama cha Waandishi Wahabari Wanawake Tanzania TAMWA ZNZ kwa waandishi wahabari ni moja kati ya chachu ya mafanikio ya kituo hicho.


“Takribani kwa miaka nane(8) tokea kuanzishwa kwa Radio Jamii Mkoani Pemba, hatujawahi kupokea tunzo, Ila vijana wa YMF wametuheshimisha kutoka TAMWA ZNZ, Meneger Radio Jamii Mkoani Pemba.


Berema Suleiman Nassor ni Mwandishi Chipukizi (YMF) kutoka kituo cha Zenj FM Radio amesema katika kukamilisha majukumu yao kikwazo kikubwa ni upatikanaji wa takwimu hivyo husababisha kuchelewa kumaliza kazi kwa wakati uliopangwa.


Katika Tunzo hiyo mshindi aliefanya vizuri katika kipengele cha Radio ni Amina Masoud kutoka Radio Jamii Mkoani, Hassan Msellem, Mitandao ya Kijamii na kwa upande wa Gazeti ni Asya Mwalim, Zanzibar Leo.


Mradi wa kuwawezesha waandishi wahabari chipukizi (YMF) kuandika habari za wanawake na Uongozi ni wa miaka miwili ,ulioanza mwaka 2022 -2024, uliowashirikisha waandishi ishirini na nne (24) kutoka Unguja na Pemba uliotekelezwa na TAMWA kwa kushirikiana na National Endosment for Democracy (NAD).


MWISHO.


    

   

Comments

Popular posts from this blog

MWALIMU WA MADRASA MBARONI KWA TUHUMA ZA KUMBAKA MWANAFUNZI WAKE

Mama ajifungua kisha kukiua kichanga na kukifukia kwenye tuta- Sizini Pemba

Mtangazaji wa Wasafi Media, Dida Afariki Dunia