TAMWA-Zanzibar yawatunuku vyeti na zawadi waandishi wa Habari 23, Mradi wa Waandishi Habari Chipukizi (YMF).
Habari Na, Nihifadhi Issa.
Akizungumza katika mahafali hayo Khairat Haji ni Kaimu Afisa Programmu TAMWA -Zanzibar amesema katika hatua za kumarisha uongozi kwa wanawake Visiwani Zanzibar, mradi huo wa awamu ya pili ambapo kwa awamu ya kwanza uliwafunza na kuwasimamia waandishi vijana 18 kwa 2022 Amesema mwaka 2023 waamdishi vijana 24 walipata fursa katika mradi huu wa Wamawake na Uongozi nakueleza kuwa Kupitia mradi huu ulikuwa unahitaji kazi 348 na hadi kufikia leo kazi hizo ni 347,huku magazeti 47 ,Makala za radio 117 huku Makala za mitandamo 187 ambazo zinakamilisha kazi 347.
Akiwa mmoja wa wanufaika kwa mradi huu Berema Suleiman Nassor ni mwandishi wa Zenji Fm pia ni mnufaika wa Mradi huu amesema kwenye uandishi wa Makala za wanawake na uongozi suala la upatikanaji wa data ni changamoto.
Akitoa Tuzo na kwa waandishi hao Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania -Zanzibar TAMWA -Zanzibar Dkt Mzuri Issa amesema Kuwa makala hizi kazi hizo zimeleta mabadiliko kwenye jamii kwa kuwashawishi wanawake kuingia kwenye siasa na kupata nguvu ya kusaidia kuvunja dhana potofu kwenye ya kuwa wanawake hawezi kuwa viongozi kuwa kwenye uongozi.
Mradi huo uliotekelezwa na TAMWA Zanzibar kwa kushirikiana na shirika la National Endowment for Democracy (NED) wa kuwawezesha waandishi wa habari vijana YMF kuandika habari za wanawake na uongozi umewashirikisha waandishi vijana ishirini na nne (24) kutoka Unguja na Pemba.
Comments
Post a Comment