Sheria ya Makosa ya Mtandao namabri 14 ya 2015, ni kandamizi kwa wanahabari Zanzibar.

Na, Hassan Msellem-Pemba.


Habari ni taarifa halisi juu ya matukio mbali mbali yanayojiri ulimwenguni ambayo mtu huhitaji kusikia, kuona au kusoma kwa lengo la kupata taarifa Fulani.


Haki ya kutafuta, kutoa na kupokea habari ni haki ya msingi ya mwanadamu iliyoainishwa kwenye Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 kifungu cha 18 (1) na (2) ambavyo vimeeleza kuwa kila mtu ana haki ya kupewa taarifa wakati wowote kuhusu matukio mbali mbali nchini na duniani kote ambayo ni muhimu kwa maisha na shughuli za wananchi, na pia juu ya masuala muhimu kwa jamii.

                Picha kutoka Maktba

Vyombo mbali mbali vya Kimataifa vinatambua umuhimu wa haki ya kupata taarifa ikiwa ni pamoja na haja ya kuwa na Sheria madhubuti kwa ajili kulinda utoaji wa haki hiyo.


Vyombo hivyo ni pamoja na Umoja wa Mataifa (UN), Muungano wan chi za Amerika (OAS), Baraza la Ulaya (CE) na Umoja wa Afrika (AU).

 

Licha ya sheria, sera pamoja na mikataba mbali mbali juu ya uhuru na haki ya kutafuta taarifa na kuzisambaza kwa umma, lakini bado kuna sheria ambazo ni kandamizi kwa vyombo vya habari na wanahabari kwa ujumla.

 

Miongoni mwa Sheria hizo ni Sheria ya Makosa ya Mtandao namabri 14 ya 2015, ambayo ufafanuzi wake haukujitosheleza kueleza namna aambavyo mwandishi wa habari anaweza kutenda kosa kupitia mitandao ya kijamii katika utekelezaji wa majukumu yake, kwa mfano ibara ya 15 (1) inasema " Mtu hatajifanya kuwa mtu mwengine kwa kutumia mfumo wa komputa" na (2) inasema " Mtu atakayekiyuka suala la kujifanya mtu mwengine kwenye mtandao, linaweza kuleta utata kwani kuna baadhi ya mitandao hutumia majina yasiyo halisi"


Kupitia ibara hii tafsiri ya nano kujifanya mtu mwengine haijitoshelezi kimaana kiasi ya kuweza kuthibitisha ni nani aliyetenda kosa hilo, hivyo basi inaonesha wazi kuwa sheria hii inamapungufu na inapaswa kufanyiwa marekebisho ya haraka.

 

Kifungu hichi kinaonesha wazi jinsi ambavyo vyombo vya habari na uhuru wa wanahabari unavyoingiliwa na kukandamizwa kupitia mtandao.

 

WADAU WA HABARI WANASEMAJE JUU YA SHERIA HIYO.

 

Kwa upande wake mwandishi wa habari wa Shirika la Utangazaji Zanzibar Abuubakar Harith, alisema Sheria hiyo imepitwa na wakati na haikuzingatia maendeleo ya sayansi na teknolojia kwani kupitia mtandao kosa linaweza kufanywa na mtu mwengine asiyekuwa mwandishi husika baada ya kurasa za mwaindishi mwenye kurasa hizo kudukuliwa na kuchapishwa maudhui yasiyozingatia maadili ya uandishi na kupelekea kufunguliwa mashtaka na kutiwa hatiani.

 

Kimsingi mataifa yote ya kidekrasia ambayo yanafuata misingi ya demokrasia na utawala bora masuala ya afisa wa polisi kukamata na kukagua yanahitaji idhini na vibali vya mahakama afisa wa Polisi hawezi kuwa yeye ndiye anatuhumu na yeye ndiye anakamata hiyo itakuwa ni Sheria ya ajabu” amesema

 

Fathiya Mussa Said ni mratibu wa chama cha waandishi wa habari wanawake Tanzania Kisiwani Pemba (TAMWA), alisema uwepo wa sheria hizo ni pigo kwa vyombo vya habari kwani watashindwa kufanya kazi zao kwa kujiamini na uhuru kupitia mitandao ya kijamii kwa kukokhofia kufanya makosa ya mtandao ambapo makosa hayo hayakuainishwa kwa uwazi ikizingatiwa mitandao ya kijamii kwa sasa ndio vyombo pekee vinavyochukuwa nafasi kubwa katika kufikisha taarifa kwa umma.


"Mimi nashauri tu sheria hiyo ifanyiwe mabadiliko ya haraka kwasababu inawanyima waandishi wa habari haki yao ya kutumia mitandao ya kijamii katika kutekeleza majukumu yao ya kihabari na tukizingatia sasa hivi mitandao ya kijamii ndio vyombo pekee vinavyofikisha taarifa katika jamii kwa haraka na huko kwenye mitandao ndiko idadi kubwa ya wafuatiliaji wa habari" alisema

                                  Fathiya Mussa Said Mratibu wa Tamwa Pemba.

Mkurugenzi Uratibu Shirika la Magazeti Pemba Haji Nassor Mohammed, anasema kulingana na mabadiliko ya teknolojia ya habari, Sheria hiyo imefika muda wa kufanyiwa marekebisho kwa uhai wa vyombo vya habari na maslahi ya Umma kwani lengo kuu la vyombo vya habari ni kufikisha taarifa mbali mbali kwa umma na uwajibikaji katika taifa.

 

                        MAONI YA WAHARIRI WA VYOMBO VYA HABARI. 

Bakari Mussa Juma ni mkuu wa gazeti la Zanzibar leo Kisiwani Pemba, ametoa ushauri kwa waandishi wa habari kuendelea kupaza sauti ili kufanyiwa marekebisho kwa sheria ambazo zinaonaka kukinzana na uhuru wa vyombo vya habari na wanahabari ili uhuru huo uweze kuakisi kwa vitendo.

 

“Hajalishi kwamba tumeshapiga kelele sana juu ya sheria hizi lakini niwasihi waandishi tusichokee kuendelea kuzipigia chapuo mpaka pale tutakapo hakikisha kuwa sheria zote kinzani zifanyiwe marekebisho ” Bakar Mussa

 

Mhariri wa Alfatah Online Tv, alisema kutokana na udhaifu wa sheria hiyo vyombo vya habari vya mtandaoni vinapitia wakati mgumu katika utekelezaji wa majukumu yao ipaswavyo kwa khofu ya kutenda makosa ya kimtandao ambapo kwa mujibu wa katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 kifungu cha 18 (1) na (2) imetoa uhuru kwa kila mwananchi kutafuta na kupokea habari ndani na nje ya mipaka ya Zanzibar na kuzisambaza bila ya kuingiliwa na mamlaka yoyote.


KLABU ZA WAANDISHI WA HABARI ZINA MAONI GAZI JUU YA KIFUNGU HIKI.

 

Ali Mbarouk Omar ni Mwenyekiti wa Klabu ya waandishi wa habari Pemba (PPC), anasema mkataba wa Afrika wa haki za binadamu na watu ya mwaka 1981 ibara ya 9 na 19 zinatoa haki ya mtu kutafuta na kupokea taarifa pasi na uhuru wake kuingiliwa, hivyo kuendelea kuwepo kwa wa sheria hiyo kuna kwenda kinyume na makubaliano ya mkataba huo, hivyo basi ameshauri sheria hiyo kufanyiwa marekebisho haraka iwezekanavyo.

 

Katibu wa jumuiya ya waandishi wa habari za maendeleo Zanzibar (WAHAMAZA) Salma Said, anasema kuendelea kutumika kwa sheria zisizozingatia uhuru wa vyombo vya habari ni miongoni mwa sababu zinazopelekea waandishi wa habari kufanyiwa matendo mbali mbali ya unyanyasaji ikiwemo kutekwa, kupigwa na hata kuawa.


“Ukiacha hiyo Sheria ya Sheria ya Makosa ya Mtandao namabri 14 ya 2015,  kuna sheria nyingi sana ambazo hazikuzingatia uhuru wa waandishi wa habari wala usalama wao ndio maana waandishi wa habari leo wanafanyiwa fujo nyingi sana ikiwemo kutekwa kiholela, kupigwa na wengine kuuawa na hakuna mamlaka yoyote inayowajibishwa kwa waandishi kufanyiwa hayo” Salma Said


“Katiba ya Zanzibar ya 1984 ibara ya 18 imeruhusu kila mwananchi kuwa huru katika kutafuta na kusambaza habari ndani na nje ya nchi wakati wowote bila ya kuingiliwa na mtu yeyote, sasa Sheria ya namna hiyo ni Sheria inayo kwenda kinyume na hata katiba yetu” alifafanua


         MAONI YA WAANDISHI WA VYOMBO MBALI MBALI VYA HABARI.

 

Waandishi wa habari kutoka vyombo mbali mbali vya habari wamesema kuendelea kuwepo kwa Sheria zisizo rafiki kwa vyombo vya habari kutapelekea waandishi kufanyakazi kwa khofu, jambo ambalo litapelekea taarifa wanazoandika kukosa usahihi.

 

                Zuhura Juma Said mwandishi wa gazeti la Zanzibar Leo Pemba

 

MAONI YA WADAU WA HABARI.

Baadhi ya wadau wa habari Kisiwani Pemba, wanasema jamii inategemea vyombo vya habari kupata taarifa mbali mbali zinazojiri ndani na nje ya nchi ambapo baadhi ya taarifa hizo huchangia katika kuleta maendeleo kwa umma hivyo endapo Sheria zisizo rafiki kwa vyombo vya habari zisipofanyiwa marekebisho zitapelekea wananchi wengi watakosa habari kwa wakati na urahisi, jambo litakalopelekea kuwa na jamii iliyokosa uelewa.

 

NINI KIFANYIKE ILI KUREKEBISHA SHERIA HIZO.

Wadau mbali mbali wa habari nchini wamekuwa wakichukua hatua kadhaa ikiwemo kuanzisha miradi, makongamano na warsha mbali mbali kusisitiza kufanyiwa marekebisho kwa sheria za habari zenye mapungufu hususani kila ifikapo siku ya uhuru wa habari duniani ili kuona ni kwa namna gani vyombo husika vinaweza kuguswa na kelele hizo na kukaa meza moja na wadau hao ili kuzipitia Sheria hizo.

 

Miongoni mwa wadau hao ni pamoja na Chama cha Waandishi wa habari Wanawake Tanzania upande wa Zanzibar yani (TAMWA-Zanzibar) Jumuiya ya Waandishi wa habari za Maendeleo Zanzibar (WAHAMAZA)   Baraza la Habari Tanzania (MCT).

Comments

Popular posts from this blog

MWALIMU WA MADRASA MBARONI KWA TUHUMA ZA KUMBAKA MWANAFUNZI WAKE

Mama ajifungua kisha kukiua kichanga na kukifukia kwenye tuta- Sizini Pemba

Mtangazaji wa Wasafi Media, Dida Afariki Dunia