Z ANZIBAR. KAMATI ya Kitaifa ya Ushauri kuhusu utekelezaji wa Programu ya Kizazi Chenye Usawa wa kiuchumi (GEF) imezipongeza taasisi zinazowezesha upatikanaji wa haki za wanawake na watoto Zanzibar kwa jitihada zake za kukuza haki na usawa wa kiuchumi kwa makundi yote. Pongezi hizo zimekuja kufuatia ziara ya kamati hiyo kutembelea taasisi za Mwanamke Initiatives Foundation (MIF), na Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania, Zanzibar (TAMWA ZNZ) iliyolenga kufuatilia utendaji wa taasisi hizo katika kuchangia ufikiaji wa kizazi chenye Usawa wa Kiuchumi. Abeida Rashid Abdallah, mjumbe wa kamati hiyo ambaye pia ni Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Zanzibar alisema taasisi hizo zinafanya kazi kubwa ya kuisaidia serikali kufikia malengo yake ya kujenga kizazi chenye usawa wa kiuchumi kwa wanawake. Alieleza, “tumefurahishwa sana na tumeona kazi kubwa inayofanywa na taasisi hizi katika kukuza haki na usawa wa kiuchumi kwa kuwajengea uwezo wanawake ku...