UKOSEFU WA VIWANJA RASMI VYA MICHEZO MASKULINI, WAKATISHA NDOTO ZA WANAFUNZI WAKIKE KUWA WANAMICHEZO.
Michezo ni sehemu ya Maisha na moja kati shughuli zinazomfanya mwanadamu kufurahia Maisha kuwa na afya imara, kukuza ufahamu na hata ukakamavu wa mwili.
Kuna aina nyingi ya
michezo ingawa baadhi ya michezo huendana na utamaduni na jamii fulani, kwa
mfano mchezo wa Ngware ni mchezo maarufu kwa jamii ya Micheweni, mchezo wa YOGA
katika jamii nyingi za Kichina, Nage, Kobole, Bao la Kete, Karata, Drafti huku
mpira wa miguu ukiwa mchezo maarufu duniani kuliko mchezo mwengine wowote licha
ya mchezo huo kuwa na idadi ndogo ya wanawake.
Maskulini ni sehemu muhimu
ya kukuza michezo kwa wanafunzi hususan wanafunzi wakike kwani kutokana na
utamaduni na mila nyingi za kiafrika watoto wakike hawapati muda wa kutosha
kushiriki michezo wakiwa nyumbani kutokana na majukumu ya kazi na mitazamo mibaya
kwa baadhi ya wanajamii walio wengi.
Miongoni mwa malengo ya
mchakato wa kufanya mapitio, kufupisha na kuandika upyaya Mtaala wa Elimu ya Msingi
Zanzibar mwaka 2008/2009 ili uendane na Sera ya Elimu Zanzibar ya mwaka 2006 ni:-
·
Kugundua vipaji vya kila mwanafunzi kuanzia umri mdogo ili
kuvidumisha na kuviendeleza
Malengo ya kupitia mtaala
wa elimu yam waka 2008\2009 ili kuendana na Sera ya Elimu yam waka 2006 ni
kugundua vipaji vya kila mwanafunzi kuanzia umri mdogo ili kuvidumisha na
kuviendeleza ingawa hakuna sehemu kwenye Mtaala huo hautaja kabisa suala la
michezo kwa wanafunzi.
Ukosefu wa viwanja vya
michezo kwa Skuli nyingi za msingi na sekondari kunachangia kwa kiasi kikubwa kufifia
kwa vipaji vya michezo kwa wanafunzi wakike.
Kwa mujibu wa mwalimu wa
Skuli ya Uweleni na Kocha wa timu ya mchezo wa mpira wa kikapu katika Skuli
hiyo Mohammed Salim Khamis, alisema Skuli zote za Pemba ni Skuli ya Maziwa ya
Ng’ombe Micheweni.
Miongoni mwa skuli hizo
sizizo na viwanja vya michezo ni Skuli ya Sekondari Uweleni Mkoani, Msingi
Kunguni Wambaa, Skuli ya msingi Nanguji, Skuli ya msingi mahuduthi Shehia ya
Mkungu, Skuli ya msingi Minazini.
Maimuna Fatawi Khamis, ni mwanafunzi wa kidato cha tatu Skuli ya Sekondari Uweleni, alisema anapenda kucheza mpira wa kikapu (Baskateball) na anajihisi anakipaji cha hali cha kucheza mchezo huo lakini kukosekana kwa kiwanja cha kuchezea mchezo huo skulini kwao kumesababisha kushindwa kushiriki kucheza mchezo huo na kudumaza ndoto yake ya kufika mbali kupitia mchezo huo.
Salma Mohammed Bakar,
mwanafunzi wa darasa la nne skuli ya msingi Mahuduthi, alisema kutokuwepo kwa
kiwanja cha michezo katika Skuli yao kumezima ndoto za wanafunzi wengi wakike
kushiriki katika michezo Pamoja na kufanya vizuri kwenye mashindo mbali mbali
ya michezo ikiwemo Tamasha la Elimu Bila ya Malipo
Mkuu wa divisheni ya
Michezo na Utamaduni kutoka Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Kisiwani
Pemba Mzee Ali Abdalla, alikiri kuwepo kwa changamoto kwa baadhi ya Skuli
kukosa Viwanja vya michezo hali inayosababisha wanafunzi hasa wakike kushindwa
kushiriki katika michezo mbali mbali.
“Kwakweli suala la kukosekana
kwa viwanja vya michezo kwa baadhi ya Skuli hilo ni tatizo kwasababu huwezi
kushiriki mashindano mbali mbali ya michezo bila ya kuwa na viwanja vya michezo
na ndio maana Serikali ikaitaka Wizara ya Elimu kumiliki ardhi ya kutosha ili
inapojenga Skuli iwe na nafasi ya kuwepo kwa kiwanja cha michezo ili wanafunzi
waweze kushiriki kwenye michezo” alisema
Mwalimu wa Skuli ya Sekondari
Uweleni na Kocha wa timu ya mchezo wa mpira wa kikapu (Basketball) katika Skuli
hiyo Mohammed Salim Khamis, alisema ukosefu wa kiwanja cha kufanyia mazoezi ya mpira
wa Kikapu kwa wanafunzi wakike wa Skuli hiyo kunawasababishia wanafunzi hao
usumbufu wa kuingia Skulini hapo mara mbili pamoja na kutumia wa Umoja ni nguvu
katika kufanya mazoezi.
“Tuna jumla ya wanafunzi
wakike ishirini na tatu ambao wanashiriki mchezo wa mpira wa Kikapu na
wanafanya vizuri kwenye mashindano mbali mbali lakini changamoto inayotukabili
ni hatuna kiwanja cha kufanyia mazoezi katika mazingira ya Skuli tunalazimika
kutumia kiwanja cha Umoja ni Nguvu jambo ambalo baadhi ya wanafunzi wanaona
shida sana Kwenda kule lakini kama tungekuwa na kiwanja chetu hapa hapa nadhani
wanafunzi wangejitokeza kwa wingi zaidi” alisema
Aliongeza kwa kutoa ushauri kwa Wizara ya Elimu na mafunzo ya amali Zanzibar kuzingatia ujenzi wa viwanja vya michezo maskulini ili wanafunzi wapate fursa ya kushiriki michezo mbali mbali hali itakayosaidia kugundua na kukuza vipaji vyao.
Msaidizi mwalimu Mkuu wa
Skuli ya Msingi Uweleni Khamis Mohammed Ussi, alisema miongoni mwa hatua
walizozichukua katika kuhakikisha wanapata uwanja wa kufanyia michezo katika
skuli hiyo ni kuongea na uongozi wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali
Zanzibar ili kuona changamoto hiyo inatatuliwa.
Mkuu wa divisheni ya
michezo na utamaduni Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Pemba Mzee Ali
Abdalla, alisema mpango wa Wizara ya Elimu imeandaa mkakati wa kutambua maeneo yake
ya ardhi nakupata hati miliki ili kuwa na maeneo ya kutosha katika kuweka
miundombinu mbali mbali ikiwemo viwanja vya michezo.
Akizingumzia suala la
baadhi ya Skuli ukosefu wa viwanja rasmi vya kufanyia michezo, alisema suala
hilo ni changamoto kwa Skuli nyingi kwani kutokuwepo kwa viwanja rasmi kunachangia
wanafunzi kutokushiriki katika michezo ipaswavyo.
“Tuelekee kule ambako
Serikali inataka michezo ni fursa michezo, michezo ni somo kama masomo mengine
na inatakiwa kuwa na maabara yake na maabara ya michezo ni viwanja sisi
tunaamini na tunatambua umuhimu wa viwanja maskulini lakini maendeleo siku zote
hayaji tu kama homa bali ni hatua kwa hatua” Mkuu wa Divisheni ya michezo na
utamaduni Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Pemba




Comments
Post a Comment