Skip to main content

WAOGELEAJI WANAWAKE PEMBA WAOMBA WADAU WA MICHEZO, KUANDAA MASHINDANO YA MCHEZO KUOGELEA.

 Mchezo wa kuogelea ni miongoni mwa michezo maarufu duniani, ingawa kuna idadi ndogo ya wanawake Barani Afrika wanaoshiriki katika mchezo huo ikilinganishwa na wanawake wa Bara Ulaya.

Zanzibar ni miongoni mwa maeneo yenye idadi ndogo sana ya wanawake wanaoshiriki mchezo wa kuogelea licha ya Visiwa hivyo kuzungukwa na Bahari, huku na sababu kadhaa zinazosababisha idadi ya wanawake wanaoshiriki mchezo huo kuwa ndogo.

 

Miongoni mwa sababu hizo pamoja na wanawake wenyewe kutokuwa na hamu na shauku ya kushiriki mchezo huo,Mila, Utamaduni pamoja na Imani potofu kwa baadhi ya wanajamii wakiamini kuwa mchezo huo ni mchezo unaowahusu wanaume pekee.

 

Mwezi March, 2022 katika shamrashamra za kumpokea Rais wa Shirikisho la Mchezo wa Kuogelea Duniani (FINA) Husain Al Musallam, kutembelea Zanzibar, Kamishna wa Idara ya Michezo Zanzibar Ameir Mohammed Makame, alisema Sera ya Michezo Zanzibar yam waka 2018 inasema kuendeleza michezo ya kuogelea ikiwa ni miongoni mwa michezo 41 iliyosajiliwa Zanzibar.

 

Balozi wa heshima wa Brazil Zanzibar, Abdulsamad Abdulrahim alisema ziara ya ais wa Shirikisho la Mchezo wa Kuogelea Duniani inafanyika ikiwa Zanzibar inajipanga kujenga bwawa kubwa la kuogelea lenye hadhi ya Olimpiki ambalo linakadiriwa kugharimu dola za kimarekani milioni 3 sawa na shilingi bilioni 6 na milioni 900, ambalo litawawezesha vijana wanaoshiriki mchezo wa kuogelea kuwa nae neo mahsusi la kuogelea tofauti na ilivyo sasa ambapo hushiriki mchezo huo kupitia habarini kama kawaida.

 

Lakini licha ya idadi hiyo ndogo ya wanawake wanaoshiriki mchezo wa kuogelea wapo wanawake ambao wana vipaji vya kuogelea na kuupenda mchezo huo kiasi ya kuuota usingizini.

 

Wanawake wa Mji wa Tumbe Wilaya ya Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba, wao wameamua wanawake wa mfano kupitia mchezo wa kuogelea hasa pale walipogundua kuwa licha ya kutumia mchezo huo katika mashindano na kujiokoa inapotokea dharura lakini pia ni kwa ajili ya harakati zao za Maisha ya kilimo cha Mwani na fursa ya kujipatia kipato.

 

Kaije Said Bakar, ni nguli na kinara wa mchezo wa kuogelea ambaye ni mwalimu wa wanawake na wasichana zaidi ya 300 kutoka maeneo tofauti ya Kisiwa cha Pemba, alisema mchezo wa kuogelea umeweza kumnufisha kwa kiasi kikubwa kama vile kujenga nyumba ya kuishi na familia yake, kuwalipa ada za masomo Watoto wake pamoja kumsadia mumewe mkate wa kila siku.

 

“kwakweli mchezo wa kuogelea umenisaidia sana sana tena sana maana kabla kujua mchezo huo Maisha yetu yalikuwa magumu mno tulikuwa tunaishi kwenye banda tu hivi kama hema la wakimbizi lakini sasa nimejenga nyumba mzuri si haba tumeshajistiri, nawalipia Watoto wangu ada za Skuli pamoja kumsaidia mume wangu pesa za matumizi ya nyumbani” alisema

 

Mize Hamad Sadiki, ni miongoni mwa wapiga mbizi alisema kwasasa ana uwezo mzuri wa kuogelea lakini anautumia uwezo huo kwenye shughuli zake za upandaji wa mwani pekee kutokana na kukosekana kwa mashindano, matamasha na mabonanza ya mchezo wa kuogelea kwa wanawake.

 

“Mimi ni Mama wa Watoto sita pia ni mjane nina uwezo mzuri wa kuogelea lakini nashindwa kupata faida ya mchezo huu kwasababu hakuna mashindano ya mara kwa mara na badala yake natumia uwezo huu katika shughuli zangu za mwani tu” alisema

Fatma Hamd Ali, mwanamke mwenye umri wa miaka 23, mwenye shauku na kipaji kizuri cha kuogelea anawaomba wadau wa michezo kuandaa mabonanza na matamasha ya mashindano ya kuogelea ili waweze kuonesha vipaji vyao na kujipatia kipato.

Hamad Amini Ali ni Mratibu wa Kamisheni ya Utalii Pemba, alisema kuna kila haja ya kuwashirikisha wanawake wenye uwezo wa kuogelea kwenye Matamasha na Mabonanza ya Utalii wanayoyafanya ili kuboresha uwezo wao na kujipatia kipato

 

Alisema “Sisi kama kamisheni ya Utalii tumelipokea kwa mikono miwili ombi la akina mama hao na tutaenda kuwatembelea ili kuwafahamu lakini mwezi Novemba mwaka huu tutakuwa na Bonanza la Utalii Kisiwani Pemba tutaanda mashindano maalumu ya kuogelea kwa wanawake ili nao waweze kushiriki katika mashindano hayo”

Wadau na wananchi mbali mbali Kisiwani Pemba wanashauku ya hali ya juu kuona mashindano ya kuogelea ya wanawake kwani muda mrefu wanashuhudia mashindano hayo kwa jinsia ya kiume pekee.

 

Shamimu Omar Shake Mkaazi wa Tibirinzi Chake Chake alisema “Watu wengi wanadhani mwanamke hana uwezo mzuri wa kuogelea kama mwanaume kwahivyo ikitokea kuna wanawake wanaogelea vizuri kama wanaume hilo litakuwa ni jambo jema na kuvutia sana na wanawake wengi watahamasika kuingia kwenye mchezo huo pamoja na kushiriki katika mashindano mbali mbali”

 

Asha Ussi Makame ni mkaazi wa Ndagoni, alisema wanajamii walio wengi wengi hawa Imani na wanawake katika mchezo huo hivyo kuwepo kwa wanawake ambao wanafanya vizuri katika mchezo kutasaidia kuondosha Imani potofu kwa baadhi ya wanaume kutokana na Imani hiyo potofu kwa wanawake

 

“wanaume wengi hawana Imani na sisi wanawake kwenye mambo mbali mbali ikiwemo michezo, uongozi nakadhalika wanatuona kama viumbe lege lege tusioweza lolote zaidi ya majukumu ya nyumbani kwahivyo kuwepo kwa wanawake kama hao wenye uwezo mzuri wa kuogelea kutapelekea wanaume kuondokana na dhana hizo mbaya kwetu lakini pia itawahamasisha wanawake wengine kuingia kwenye mchezo huo” alisema


Comments

Popular posts from this blog

MWANAMKE AJINYONGA, SABABU WASI WASI - PEMBA

NA, HASSAN MSELLEM - PEMBA PICHA KUTOKA MAKTABA Mwanamke aliyefahamika kwa jina la Raya Darusi Abdallla miaka 48, mkaazi wa Mbuzini Wilaya ya Chake Chake Mkoa wa Kusini Pemba, amefariki Dunia kwa kidaiwa kujinyonga kutokana na Msongo wa mawazo. Tukio Hilo limetokea Novemba 30.2025 saa 11 alfajiri huko Mbuzini Wilaya ya Chake Chake Mkoa wa Kusini Pemba. Omar Salum Ali, ambaye ni shemeji wa marehemu amesema kabla ya marehemu alikuwa na sumbuliwa na Msongo wa mawazo kutokana na kumpoteza kaka yake ambaye alifariki hivi karibuni, kugundulika kuwa ana maradhi ya sukari, mtoto wake wa kiume wa miaka 25, kuwa na ugonjwa akili hali iliyopelekea kupatwa na Msongo wa mawazo na kuamua kujinyonga. Katibu wa Sheha (Katibu wa Mwenyekiti) Shehia ya Mbuzini Yakub Ali Msabah, amesema alipata taarifa za tukio Hilo kutoka kwa Sheha wa Mbuzini kuhusu tukio baada ya kufika eneo la tukio waliukuta mwili wa Mama huyo ukiwa unanin'gia kwenye dari ya Nyumba ambayo alikuwa anaishi zamani. Kutoka tarehe 18 ...

Mariam Muhene – mfano wa kuigwa kwa wanawake kwenye ulingo wa siasa ni

MAKALA NA, HASSAN MSELLEM -PEMBA Tangu Tanzania iruhusu mfumo wa vyama vingi mwaka 1992, Mariam Muhene alijiunga na chama cha Civic United Front (CUF) ambapo mwaka 1995, aligombea nafasi ubunge wa viti maalumu na kuvuka hatua zote ikiwemo kula kiapo mahkamani lakini hakufanikiwa kukikalia kiti hicho. “Mwaka 1995 niligombea ubunge wa viti maalum na nikapita kila kipengele mtu wa kwanza wilaya, taifa bodi ya uongozi, nikala kiapo mahkmanai lakini katika nafasi mbili zilizoletwa kwa kila mkoa Kusini na Kaskazini Pemba mimi sikubahatika” amesema  Safari yake ya kisiasa za upinzani iliendelea na mnamo mwaka 2000, aligombea nafasi ya ubunge wa kuchahguliwa kupitia chama cha Allience for Democratic Change (ADC) Jimbo la Chake Chake lakini kutokana na changamoto zilizojitokeza ikiwe mawakala wa Chama chake kutokuruhisiwa kuingia kwenye vya kupiga kura jambo ambalo amesema lilichangia kukosa nafasi hiyo. Kwasasa Mariam Mohammed Muhene anashika nafasi ya Kamishna wa ADC kanda ya Pemba, nafas...

WATOTO KUJINYONGA ZANZIBAR, UTAFITI WAHITAJIKA.

HABARI NA, HASSAN MSELLEM, PEMBA Picha kutoka mtandaoni Visa vya watoto kujinyonga vimeanza kuwatia khofu na mashaka wazazi na walezi katika Visiwa vya Unguja na Pemba. Mashaka na khofu hiyo imeibuka baada ya matukio mawili mfululizo ya watoto wawili mmoja akiwa umri wa miaka (5) na mwengine (9) kuripotiwa kufariki dunia kwa kujinyonga kati ya tarehe 7 na 9 mwezi huu wa kumi mwaka 2025 kupitia kipindi cha Mawio kinachorushwa na Shirika la Utangazaji Zanzibar ZBC kila siku kuanzia saa 12:40 asubuhi. Katika tukio la kwanza mnamo tarehe 7.10.2025 mwandishi Masanja Mabula aliripoti tukio la Fatma Omar Kidere mwenye umri wa miaka tisa (9) mkaazi wa Mtondoo Jeuri Makaangale Wilaya ya Micheweni Mkao wa Kaskazini Pemba, amekutwa amefariki dunia na mwili wake ukiwa unanin’ginia kwa kutumia mtandio Jirani wa marehemu aliyefahamika kwa jina la Khamis Ali, amesema amepata taarifa za tukio hilo akiwa kazini baada ya kupigiwa simu na mke wake kumpa taarifa za kutokea kwa tukio hilo na kuondoka kazin...