Skip to main content

Posts

Showing posts from August, 2025

MWEZI JULY NA AGOSTI VICHANGA VIWILI VYATELEKEZWA NA KUTUPWA PEMBA.

NA, HASSAN MSELLEM, PEMBA   Visa vya Watoto kuzaliwa kutelekezwa na kutupwa vinaendelea kuchukua nafasi Kisiwani Pemba, hii ni baada ya mtoto mchanga wakike anaekadiriwa kuwa na wiki moja kukutwa ametelekezwa mbepezoni mwa Msikiti wa Mkanjuni Chake Chake Mkoa wa Kusini Pemba. Akisimulia kuhusu tukio hilo Sheha Mkoroshoni Zuwena Suleiman Salahi, alisema siku ya Ijumaa Agosti 29.08.2025 saa 1:30 usiku alipata taarifa kutoka kwa mjumbe wake za kuonekana kwa mtoto huyo akiwa ametelekezwa na mtu asiefahamika. Aidha Sheha huyo ametoa wito kwa wanawake kuacha tabia za kuwatelekeza na kuwatupa Watoto kwa kuhisi aibu ya kuzaa nje ya ndoa au sababu nyenginezo kwani kufanya hivyo ni kinyume na Sheria za Serikali na Dini. “Jana siku ya Ijumaa saa 1:30 usiku nilipata taarifa kutoka kwa mjumbe wangu wa sheha kuwa kuna mtoto ametupwa msikiti mkanjuni ndio nikatoka nikaenda nilipofika mtoto alikuwa ameshaondoshwa pale msikitini yupo kwa mjumbe wangu wa sheha nikenda kumuona kisha nikampigia simu M...

HAKI YA ELIMU KWA WATOTO WENYE ULEMAVU VIJIJINI BADO KIZUNGUMKUTI.

 NA, HASSAN MSELLEM, PEMBA Juma Haji Khamis miaka 13, mwenye Ulemavu wa viungo kutoka Kwa-Azani Wambaa. Licha Serikali kupitia Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar kuanzisha Sera ya elimu mjumuisho lakini ufikiwaji wa Sera hiyo kwa Watoto wenye Ulema wanaoishi vijijini ni changamoto iliyokosa ufumbuzi. Hali hiyo inasababishwa na miundombinu mibovu ya Barabara, mashule pamoja hali za Watoto wenye Ulemavu kuzidi kuwa mbaya kutokana na kukosa visaidizi kama vile viti mwendo, walimu na vitendea kazi vyakusomea. Shehia ya Wambaa ambayo inapitakana Wilaya ya Mkoani Mkoa wa Kusini Pemba ina zaidi ya Watoto 12 wenye ulemavu mchanganyiko wakiwemo Wenye Ulemavu wa Viungo, Uziwi, macho na Ualbino lakini kati yao hakuna hata mmoja aliyepata fursa kupata elimu hata kwa kiwango cha kumaliza elimu ya msingi. Juma Haji Khamis ni mtoto wa miaka 13 mkaazi wa Kijiji cha Kwa-Azani mwenye Ulemavu wa Viungo (tatizo la kutembea) akiwa mtoto wa 5 katika familia ya Watoto 6 wenye Ulemavu, ameshindw...

WANANCHI WA VIJIJI VYA KWA-AZANI NA KUTUKUU WATAKIWA KUWADHIBITI WATOTO WAO “AJIRA ZA UTOTONI”

 NA, HASSAN MSELLEM, PEMBA Watoto wenye umri kati ya miaka 12 na 13 wakiwa wamebeba Kiroba cha Pweza Bandari ya Msije Wambaa na kupeleka Kijijini Kwa-Azani  Wazazi na walezi wa Vijiji vya Kwa-Azani na Kutukuu Shehia ya Wambaa Wilaya ya Mkoani Mkoa wa Kusini Pemba, wametakiwa kuwalea Watoto wao katika misingi bora ili kuepukana na matatizo yanayoweza kujitokeza ikiwemo ajira za utoto na udhalilishaji. Akizungumza na wananchi hao katika Uwanja wa mpira Kwa-Azani Afisa Ustawi wa Jamii Wilaya ya Mkoani Bimchanga Mussa Mohammed, amesema kumekuwepo na wimbi kubwa la Watoto wanaojishughulisha na shughuli za Uvuvi na kutumikishwa na wafanya biashara hali inayosababisha hali inayochangia Watoto hao kuacha kwenda Skuli. “Jamani tunatakiwa kuwalea Watoto wetu katika misingi bora ya kijamii na kidini sio kuishia tu kuwatunza tu kwa kuwapa chakula na nguo mtoto usipomsimamia ukahakikisha kuwa anawenda Skuli na madrasa vizuri kinachofata ni kujiingiza katika makundi maovu yakiwemo ya ...

WAANDISHI WA HABARI PEMBA WABEBESHWA ZIGO LA “AMANI” KUELEKEA UCHAGUZI MKUU WA 2025.

NA, HASSAN MSELLEM, PEMBA Waandishi wa Habari Kisiwani Pemba wametakiwa kuzingatia weledi, maadili na taaluma ya Habari katika kuandika na kuripoti taarifa zinazochochea amani na utulivu nchini. Akizungumza na Waandishi hao katika Ukumbu wa Baraza la Mji Chake Chake Afisa mdhamini Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo Mfamau Lali Mfamau katika Kongamano la Kuimarisha Amani kati ya Jeshi Polisi na Vyombo vya habari kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025, amesema waandishi walioshiriki katika Kongamano hilo wanapaswa kuzingatia maelekelezo waliyopatiwa katika kipindi cha Uchaguzi. Aidha Afisa huyo ameliomba Jeshi la Polisi kuwashughulikia Waandishi watakaokiuka maelekezo yaliyotolewa kwenye Kongamono ili iwe mfano kwa waandishi wengine. “Kwa habati mzuri hapa munazungumza Kiswahili kimoja lakini mukikutana fild (eneo la kazi) katika wale watu ambao mumewapa maelekezo halafu mukaja kugundua wale watu wambao tumekaa tumedicuss nao haya mambo umuhimu wa amani kuelekea katika kipindi cha Uchag...

"TUNAOMBA USALAMA WA WAANDISHI WA HABARI, WANAWAKE WAGOMBEA NA WASIMAMIZI WA UCHAGUZI" ZAMECO

NA, HASSAN MSELLEM, PEMBA KAMATI ya Wataalamu wa Masuala ya Habari Zanzibar (ZAMECO) imeiomba Serikali ya mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) kushirikiana na Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) kuhakikisha usalama wa Waandishi wa Habari, Wanawake wagombea, na Wasimamizi wa Uchaguzi (Mawakala) katika kipindi chote cha mchakato wa uchaguzi mkuu wa Zanzibar ambao utafanyika mwishoni mwa mwezi Oktoba mwaka huu. Kamati hiyo imesema inatambua kuwa mazingira salama kwenye masuala muhimu yenye maslahi mapana na mustakabali wa nchi hususan suala la uchaguzi, ni sharti la msingi ili kuhakikisha kila mdau anatekeleza majukumu yake kwa uhuru na bila ya hofu kama ilivyoelezwa katika Ibara ya 15(1) ya Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984: "(Kila mtu anastahiki kuheshimiwa na kupata hifadhi kwa nafsi yake, maisha yake binafsi na ya nyumbani kwake, na pia heshima, na hifadhi ya maskani yake na mmawasiliano yake)." Aidha Kamati imesisitiza kuzingatiwa hatua mahsusi kwa mujibu wa sheria na kanuni za kulind...

"NINA IMANI NA MAKUZI, MALEZI NA MAENDELEO YA AWALI YA MTOTO" MAMA MARIAM MWINYI

NA, HASSAN MSELLEM- PEMBA MKE wa Rais wa Zanzibar, Msarifu na Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Foundation (ZMBF) Mama Mariam Mwinyi amesema ana imani kuwa makuzi, malezi bora na maendeleo ya awali ya mtoto ni msingi imara wa kujenga taifa lenye raia wenye afya, elimu, nidhamu na maendeleo endelevu. Mama Mariam Mwinyi, ameyasema hayo Agosti 13. 2025, wakati alipozindua Kampeni ya Makuzi, Malezi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto (ECD) katika viwanja vya Kisonge, Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja, a mesema kuwa ni vyema kwa jamii kuhakikisha inawapatia watoto malezi na makuzi bora ya awali, ili kuwajengea mustakbali mwema wa maisha bora ya baadae. Mama Mariam Mwinyi ameeleza kuwa, ZMBF imekuwa mstari wa mbele kusaidia maendeleo ya makuzi ya mtoto, hususan katika programu za lishe pamoja na huduma za afya ya mama na mtoto, ambapo kupitia jitihada hizo, imeweza kuwafikia wanufaika zaidi ya 50,000 katika Shehia 67 na vijiji 644 vya Unguja na Pemba. Alisema kuwa, k...

“ANDIKENI HABARI ZA WATU WENYE ULEMAVU ILI NAO WAPATE HAKI ZAO” AFISA PROGRAMU TAMWA,ZNZ.

HABARI NA, HASSAN MSELLEM-PEMBA Waandishi wa Habari Kisiwani Pemba wametakiwa kuwa mabalozi kwa watu Wenye Wenye Ulemavu kwa kuandika na kuripoti taarifa zao ili kutoa elimu kwa jamii kuhusu Kundi hilo. Hayo yamenenwa na Afisa Programu na Mawasiliano wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA) kanda ya Zanzibar Khairat Ali Haji, wakati akifungua mafunzo ya siku tatu za kuwapiga msasa waandishi wa Habari Kisiwani Pemba katika kuandika Habari jumuishi zitakazokuza ustwahi na haki za Watu Wenye Ulemavu. Amesema lengo la mafunzo hayo ni kuongeza utetezi kwa Watu Wenye Ulemavu ili kupata haki zao kama ikiwemo haki ya kuchanganyika na wengine, elimu, kazi pamoja na kushiriki kwenye siasa. “Lengo la mafunzo ya kwenu ni kuwapiga msasa kusudi muwe na uwezo mzuri wa kuandika na kuripoti Habari za Watu Wenye Ulemavu ili nao waweze kupatiwa haki zao za msingi ambazo wamezikosa kwa muda mrefu sana kama vile haki ya kuchanganyika na wengine, haki ya elimu, kufanya kazi na kush...

MWANAHABARI TEMMY MAHONDO AFARIKI DUNIA.

Mwanahabari Temigunga Mahondo amefariki Dunia Hospital ya Benjamin Mkapa Jijini Dodoma. Mahondo alikuwa mwandishi wa habari na meneja wa kituo kikongwe cha Radio cha Country Fm cha mkoani Iringa na baada ya hapo alifanya kazi na taasisi za kimataifa za kihabari kama mkufunzi kwa wabahabari. Mahondo pia amekuwa msaada mkubwa kwa chombo cha Matukio Daima Media kwani hadi mauti yanamkuta ndie alikuwa mkuu wa kitendo cha mafunzo ya kuwajengea uwezo waandishi katika Matukio Daima Media . Mahondo pindi alipolazwa Hospitali ya Mlonganzila wanakundi wa Iringa Daima ambako alikuwa ni mmoja wa waanzilishi wa kundi hilo ambalo Admin wake mkuu ni mkurugenzi wa Matukio Daima Media Francis Godwin walimchangia zaidi ya Tsh milioni 3 na yeye alitoa sehemu ya pesa hiyo kuchangia ujenzi wa ICU Hospital ya Rufaa ngazi ya mkoa ya Tosamaganga pesa alizokwenda kukabidhi mwenyewe na baadhi ya wanakundi huku akihamasisha jamii kuchangia zaidi. Siku nne kabla ya kifo chake uongozi wa Iringa Daima ulikwenda kum...

Waandishi wapigwa msasa malezi, makuzi na maendeleo ya awali ya mtoto (ECD)

  NA, HASSAN MSELLEM-PEMBA Waandishi wa habari Zanzibar wametakiwa kuripoti na kutoa elimu  kwa jamii juu ya umuhimu wa malezi, makuzi na maendeleo ya awali ya mtoto ili kuwa na taifa lenye ustawi bora. Akizungumza na waandishi na wadau hao katika mafunzo ya siku nne yaliyofanyika huko katika ukumbi wa Hoteli ya Jamirex Mwenge Jijini Dar- Es- Salaam  Katibu Mkuu kutoka Wizara ya elimu Zanzibar Dkt. Khamis Abdalla, amesema Dira ya maenedeleo endelevu ya 2050 ya Zanzibar itafikiwa endapo watoto watakuwa katika makuzi na malezi bora yenye kujenga maadili na maarifa Aidha, Dkt. Khamis amewataka waandishi hao kuandaa vipinda, ripoti na Makala mbali mbali zitakazochochea haki za Watoto ikiwemo haki kupata elimu, chanjo, vyeti vya kuzaliwa na kuwalinda na kuwahifadhi. Kwa upande wake Meneja mradi Bi. Mariam Issa,  amesema Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kupitia Wizara ya Afya imeamuaa kuongeza nguvu katika Malezi, Makuzi na Maendeleo ya awali ya mtoto kutokana na umuhimu w...