Skip to main content

HAKI YA ELIMU KWA WATOTO WENYE ULEMAVU VIJIJINI BADO KIZUNGUMKUTI.

 NA, HASSAN MSELLEM, PEMBA

Juma Haji Khamis miaka 13, mwenye Ulemavu wa viungo kutoka Kwa-Azani Wambaa.

Licha Serikali kupitia Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar kuanzisha Sera ya elimu mjumuisho lakini ufikiwaji wa Sera hiyo kwa Watoto wenye Ulema wanaoishi vijijini ni changamoto iliyokosa ufumbuzi.

Hali hiyo inasababishwa na miundombinu mibovu ya Barabara, mashule pamoja hali za Watoto wenye Ulemavu kuzidi kuwa mbaya kutokana na kukosa visaidizi kama vile viti mwendo, walimu na vitendea kazi vyakusomea.

Shehia ya Wambaa ambayo inapitakana Wilaya ya Mkoani Mkoa wa Kusini Pemba ina zaidi ya Watoto 12 wenye ulemavu mchanganyiko wakiwemo Wenye Ulemavu wa Viungo, Uziwi, macho na Ualbino lakini kati yao hakuna hata mmoja aliyepata fursa kupata elimu hata kwa kiwango cha kumaliza elimu ya msingi.

Juma Haji Khamis ni mtoto wa miaka 13 mkaazi wa Kijiji cha Kwa-Azani mwenye Ulemavu wa Viungo (tatizo la kutembea) akiwa mtoto wa 5 katika familia ya Watoto 6 wenye Ulemavu, ameshindwa kuendelea na masomo kutokana na hali yake ya Ulemavu inayosababisha kushindwa kufika Shuleni.

“Watoto wangu sita kati ya Watoto tisa wana ulemavu wa miguu na wakiume ni huyu Juma kwasababu Watoto wangu wengi ni wanawake, kwahivyo huu ulemavu unawafanya washindwe kuendelea na masomo huyu Juma alikuwa anakwenda skuli lakini baadae akawa anashindwa kutokana na hali yake kuzidi kuwa mbaya” alisema mama wa mtoto huyo Fatuma Simai Faki

Hadija Haji Makame miaka 12, mwenye Ulemavu wa Ualbino na mwenye ndoto ya kuwa Daktari Mkaazi wa Chumbageni ambaye ameshindwa kuendelea na masomo na kuishia darasa la tatu, alisema ameshindwa kuendelea na masomo kutokana kushindwa kusoma na kuandika kutokana na kukosa uwezo mzuri wa kuona kwenye madaftari.

Sheha wa Wambaa Mohammed Suleiman, amekiri kuwepo kwa tatizo hilo ambalo alisema linachangiwa na hali duni za kifamilia pamoja miundombinu isiyo rafiki ya Barabara, walimu na vitendea kazi maskulini sambamba na kuahidi kulifanyia kazi tatizo hilo kwa kulitolea taarifa kwa viongozi wa Wilaya.

“Kwanza nikiri kuwepo kwa tatizo hilo ambalo limezoeleka kwa jamii nyingi za vijijini na kuonekana ni jambo la kawaida tu lakini sisi kama wawakilishi wa jamii hua tunapata nafasi kila kuzungumza na viongozi wa Wilaya juu ya matatizo yanayojiri katika Shehia zetu kwahivyo hili nalo tutalifikisha kwa mabosi zetu ili kuona ni kwa namna gani wanaweza kulifanyia kazi” 

“Tatizo hilo lipo sana katika jamii nyingi za vijijini binafsi hivi karibuni nimefanikiwa kuwarudisha Skuli, lakini tunashirikiana na kitengo cha Inclusive Education kutoka Wizara ya elimu kuwapeleka na kuwarudisha skuli wale ambao wamesha acha masomo ” Afisa wa Watu Wenye Ulemavu Wilaya ya Mkoani Warda Wally Mohammed

Mratibu wa Baraza la Watu Wenye Ulemavu Mashavu Mabrouk Juma, Sera ya Elimu ya mwaka 2022, imetoa fursa ya elimu kwa Watu Wenye Ulemavu ikiwemo ikiwemo kuboresha miundombinu rafiki maskulini, vifaa vya kufundishia pamoja na walimu wenye taaluma ya elimu mjumuishi.

“Kwakweli Serikali kupitia Wizara ya elimu kwa kushirikiana na Baraza la Taifa la Watu Wenye Ulemavu imepiga hatua kubwa sana kuboresha mazingira ya watu wenye ulemavu katika sekta ya elimu licha ya kuwepo kwa changamoto kadhaa hususan kwa upande wa vijijini kama ulivyosema lakini hilo sisi kama wasaizidizi wa Baraza tutahakikisha tunalifanyia kazi ipaswavyo” alifafanua

Comments

Popular posts from this blog

MWANAMKE AJINYONGA, SABABU WASI WASI - PEMBA

NA, HASSAN MSELLEM - PEMBA PICHA KUTOKA MAKTABA Mwanamke aliyefahamika kwa jina la Raya Darusi Abdallla miaka 48, mkaazi wa Mbuzini Wilaya ya Chake Chake Mkoa wa Kusini Pemba, amefariki Dunia kwa kidaiwa kujinyonga kutokana na Msongo wa mawazo. Tukio Hilo limetokea Novemba 30.2025 saa 11 alfajiri huko Mbuzini Wilaya ya Chake Chake Mkoa wa Kusini Pemba. Omar Salum Ali, ambaye ni shemeji wa marehemu amesema kabla ya marehemu alikuwa na sumbuliwa na Msongo wa mawazo kutokana na kumpoteza kaka yake ambaye alifariki hivi karibuni, kugundulika kuwa ana maradhi ya sukari, mtoto wake wa kiume wa miaka 25, kuwa na ugonjwa akili hali iliyopelekea kupatwa na Msongo wa mawazo na kuamua kujinyonga. Katibu wa Sheha (Katibu wa Mwenyekiti) Shehia ya Mbuzini Yakub Ali Msabah, amesema alipata taarifa za tukio Hilo kutoka kwa Sheha wa Mbuzini kuhusu tukio baada ya kufika eneo la tukio waliukuta mwili wa Mama huyo ukiwa unanin'gia kwenye dari ya Nyumba ambayo alikuwa anaishi zamani. Kutoka tarehe 18 ...

Mariam Muhene – mfano wa kuigwa kwa wanawake kwenye ulingo wa siasa ni

MAKALA NA, HASSAN MSELLEM -PEMBA Tangu Tanzania iruhusu mfumo wa vyama vingi mwaka 1992, Mariam Muhene alijiunga na chama cha Civic United Front (CUF) ambapo mwaka 1995, aligombea nafasi ubunge wa viti maalumu na kuvuka hatua zote ikiwemo kula kiapo mahkamani lakini hakufanikiwa kukikalia kiti hicho. “Mwaka 1995 niligombea ubunge wa viti maalum na nikapita kila kipengele mtu wa kwanza wilaya, taifa bodi ya uongozi, nikala kiapo mahkmanai lakini katika nafasi mbili zilizoletwa kwa kila mkoa Kusini na Kaskazini Pemba mimi sikubahatika” amesema  Safari yake ya kisiasa za upinzani iliendelea na mnamo mwaka 2000, aligombea nafasi ya ubunge wa kuchahguliwa kupitia chama cha Allience for Democratic Change (ADC) Jimbo la Chake Chake lakini kutokana na changamoto zilizojitokeza ikiwe mawakala wa Chama chake kutokuruhisiwa kuingia kwenye vya kupiga kura jambo ambalo amesema lilichangia kukosa nafasi hiyo. Kwasasa Mariam Mohammed Muhene anashika nafasi ya Kamishna wa ADC kanda ya Pemba, nafas...

WATOTO KUJINYONGA ZANZIBAR, UTAFITI WAHITAJIKA.

HABARI NA, HASSAN MSELLEM, PEMBA Picha kutoka mtandaoni Visa vya watoto kujinyonga vimeanza kuwatia khofu na mashaka wazazi na walezi katika Visiwa vya Unguja na Pemba. Mashaka na khofu hiyo imeibuka baada ya matukio mawili mfululizo ya watoto wawili mmoja akiwa umri wa miaka (5) na mwengine (9) kuripotiwa kufariki dunia kwa kujinyonga kati ya tarehe 7 na 9 mwezi huu wa kumi mwaka 2025 kupitia kipindi cha Mawio kinachorushwa na Shirika la Utangazaji Zanzibar ZBC kila siku kuanzia saa 12:40 asubuhi. Katika tukio la kwanza mnamo tarehe 7.10.2025 mwandishi Masanja Mabula aliripoti tukio la Fatma Omar Kidere mwenye umri wa miaka tisa (9) mkaazi wa Mtondoo Jeuri Makaangale Wilaya ya Micheweni Mkao wa Kaskazini Pemba, amekutwa amefariki dunia na mwili wake ukiwa unanin’ginia kwa kutumia mtandio Jirani wa marehemu aliyefahamika kwa jina la Khamis Ali, amesema amepata taarifa za tukio hilo akiwa kazini baada ya kupigiwa simu na mke wake kumpa taarifa za kutokea kwa tukio hilo na kuondoka kazin...