Skip to main content

“ANDIKENI HABARI ZA WATU WENYE ULEMAVU ILI NAO WAPATE HAKI ZAO” AFISA PROGRAMU TAMWA,ZNZ.

HABARI NA, HASSAN MSELLEM-PEMBA

Waandishi wa Habari Kisiwani Pemba wametakiwa kuwa mabalozi kwa watu Wenye Wenye Ulemavu kwa kuandika na kuripoti taarifa zao ili kutoa elimu kwa jamii kuhusu Kundi hilo.

Hayo yamenenwa na Afisa Programu na Mawasiliano wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA) kanda ya Zanzibar Khairat Ali Haji, wakati akifungua mafunzo ya siku tatu za kuwapiga msasa waandishi wa Habari Kisiwani Pemba katika kuandika Habari jumuishi zitakazokuza ustwahi na haki za Watu Wenye Ulemavu.

Amesema lengo la mafunzo hayo ni kuongeza utetezi kwa Watu Wenye Ulemavu ili kupata haki zao kama ikiwemo haki ya kuchanganyika na wengine, elimu, kazi pamoja na kushiriki kwenye siasa.

“Lengo la mafunzo ya kwenu ni kuwapiga msasa kusudi muwe na uwezo mzuri wa kuandika na kuripoti Habari za Watu Wenye Ulemavu ili nao waweze kupatiwa haki zao za msingi ambazo wamezikosa kwa muda mrefu sana kama vile haki ya kuchanganyika na wengine, haki ya elimu, kufanya kazi na kushiriki kwenye siasa ili waweze kuchagua na kuchaguliwa” alisema

Akiwasilisha mada katika mafunzo hayo Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanawake Wenye Ulemavu Zanzibar (JUWAUZA) Bi. Salma Haji Saadat, amesema kwa mujibu wa matokeo ya Sensa ya Watu na Makaazi ya 2022, kati ya Wazanzibari milioni 1 na laki nane asilimia 11.4% ni wenye ulemavu idadi inayoonekana kuongezeka maradufu kutoka asilimia 5.4% kwa mujibu wa Sensa ya Watu na Makaazi ya 2012.

Ameongeza kuwa kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) 2025 idadi ya Watu Wenye Ulemavu imefikia asilimia 16% saw ana ongezeko la asilimia 1 kutoka asilimia 15% kutoka mwaka 2011 wakati Dunia ikiwa idadi ya watu zaidi ya bilioni saba

“Tafiti zinaonesha idadi ya watu wenye ulemavu inaongezeka kila uchao na hii inatokana na sababu mbali mbali ikiwemo vita kama tunavyoshuhudia vita vya muda mrefu Izrael na Palestina, Izrael na Iran, Urusi na Ukrine, umasikini, ajali nakadhalika” alisema

Aliongozekuwa changamoto kubwa inayowakabili watu wenye ulemavu ni kutokukubaliwa na katika jamii licha ya uwezo mkubwa walionao katika Nyanja mbali mbali kama vile vipawa vya kielimu, uongozi, sanaa, biashara na ujasiriamali.

Alisema “Watu Wenye Ulemavu hawana matatizo matatizo wanayo wanajmii wenyewe kutokuwakubali na kuwaamini watu wenye ulemavu kutokana na ulemavu wao wakati watu wenye ulemavu wana uwezo na vipawa vya kufanya vizuri kama wasio na ulemavu jambo la msingi ni kuaminiwa na kupewa nafasi ili waweze kuonesha uwezo na vipawa vyao”

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanawake Wenye Ulemavu Zanzibar (JUWAUZA) Bi. Salma Haji Saadat

Nao waandishi wa Habari walioshiriki katika mafunzo hayo wameahidi kuyatumia mafunzo waliopatiwa katika kuandika na kuripoti Habari za utetezi wa haki za watu wenye ulemavu ili waweze kutimiza ndoto na malengo waliyojiwekea

Mwandishi wa Radio Jamii Micheweni Asha Kazambo.

Mafunzo hayo ya siku 3 kwa waandishi wa Habari 10 Kisiwani Pemba, yametolewa na TAMWA-ZNZ kupitia mradi wa miaka mitano wenye jina la Collective Actions for Disability Right (CADiR) wenye lengo la kutetea na kukuza haki za Watu Wenye Ulemavu kwa kushirikiana na Taasisi ya Watu Wenye Ulamavu ya Norway (NAD)


Comments

Popular posts from this blog

MWANAMKE AJINYONGA, SABABU WASI WASI - PEMBA

NA, HASSAN MSELLEM - PEMBA PICHA KUTOKA MAKTABA Mwanamke aliyefahamika kwa jina la Raya Darusi Abdallla miaka 48, mkaazi wa Mbuzini Wilaya ya Chake Chake Mkoa wa Kusini Pemba, amefariki Dunia kwa kidaiwa kujinyonga kutokana na Msongo wa mawazo. Tukio Hilo limetokea Novemba 30.2025 saa 11 alfajiri huko Mbuzini Wilaya ya Chake Chake Mkoa wa Kusini Pemba. Omar Salum Ali, ambaye ni shemeji wa marehemu amesema kabla ya marehemu alikuwa na sumbuliwa na Msongo wa mawazo kutokana na kumpoteza kaka yake ambaye alifariki hivi karibuni, kugundulika kuwa ana maradhi ya sukari, mtoto wake wa kiume wa miaka 25, kuwa na ugonjwa akili hali iliyopelekea kupatwa na Msongo wa mawazo na kuamua kujinyonga. Katibu wa Sheha (Katibu wa Mwenyekiti) Shehia ya Mbuzini Yakub Ali Msabah, amesema alipata taarifa za tukio Hilo kutoka kwa Sheha wa Mbuzini kuhusu tukio baada ya kufika eneo la tukio waliukuta mwili wa Mama huyo ukiwa unanin'gia kwenye dari ya Nyumba ambayo alikuwa anaishi zamani. Kutoka tarehe 18 ...

Mariam Muhene – mfano wa kuigwa kwa wanawake kwenye ulingo wa siasa ni

MAKALA NA, HASSAN MSELLEM -PEMBA Tangu Tanzania iruhusu mfumo wa vyama vingi mwaka 1992, Mariam Muhene alijiunga na chama cha Civic United Front (CUF) ambapo mwaka 1995, aligombea nafasi ubunge wa viti maalumu na kuvuka hatua zote ikiwemo kula kiapo mahkamani lakini hakufanikiwa kukikalia kiti hicho. “Mwaka 1995 niligombea ubunge wa viti maalum na nikapita kila kipengele mtu wa kwanza wilaya, taifa bodi ya uongozi, nikala kiapo mahkmanai lakini katika nafasi mbili zilizoletwa kwa kila mkoa Kusini na Kaskazini Pemba mimi sikubahatika” amesema  Safari yake ya kisiasa za upinzani iliendelea na mnamo mwaka 2000, aligombea nafasi ya ubunge wa kuchahguliwa kupitia chama cha Allience for Democratic Change (ADC) Jimbo la Chake Chake lakini kutokana na changamoto zilizojitokeza ikiwe mawakala wa Chama chake kutokuruhisiwa kuingia kwenye vya kupiga kura jambo ambalo amesema lilichangia kukosa nafasi hiyo. Kwasasa Mariam Mohammed Muhene anashika nafasi ya Kamishna wa ADC kanda ya Pemba, nafas...

WATOTO KUJINYONGA ZANZIBAR, UTAFITI WAHITAJIKA.

HABARI NA, HASSAN MSELLEM, PEMBA Picha kutoka mtandaoni Visa vya watoto kujinyonga vimeanza kuwatia khofu na mashaka wazazi na walezi katika Visiwa vya Unguja na Pemba. Mashaka na khofu hiyo imeibuka baada ya matukio mawili mfululizo ya watoto wawili mmoja akiwa umri wa miaka (5) na mwengine (9) kuripotiwa kufariki dunia kwa kujinyonga kati ya tarehe 7 na 9 mwezi huu wa kumi mwaka 2025 kupitia kipindi cha Mawio kinachorushwa na Shirika la Utangazaji Zanzibar ZBC kila siku kuanzia saa 12:40 asubuhi. Katika tukio la kwanza mnamo tarehe 7.10.2025 mwandishi Masanja Mabula aliripoti tukio la Fatma Omar Kidere mwenye umri wa miaka tisa (9) mkaazi wa Mtondoo Jeuri Makaangale Wilaya ya Micheweni Mkao wa Kaskazini Pemba, amekutwa amefariki dunia na mwili wake ukiwa unanin’ginia kwa kutumia mtandio Jirani wa marehemu aliyefahamika kwa jina la Khamis Ali, amesema amepata taarifa za tukio hilo akiwa kazini baada ya kupigiwa simu na mke wake kumpa taarifa za kutokea kwa tukio hilo na kuondoka kazin...