Skip to main content

WANANCHI WA VIJIJI VYA KWA-AZANI NA KUTUKUU WATAKIWA KUWADHIBITI WATOTO WAO “AJIRA ZA UTOTONI”

 NA, HASSAN MSELLEM, PEMBA

Watoto wenye umri kati ya miaka 12 na 13 wakiwa wamebeba Kiroba cha Pweza Bandari ya Msije Wambaa na kupeleka Kijijini Kwa-Azani 

Wazazi na walezi wa Vijiji vya Kwa-Azani na Kutukuu Shehia ya Wambaa Wilaya ya Mkoani Mkoa wa Kusini Pemba, wametakiwa kuwalea Watoto wao katika misingi bora ili kuepukana na matatizo yanayoweza kujitokeza ikiwemo ajira za utoto na udhalilishaji.

Akizungumza na wananchi hao katika Uwanja wa mpira Kwa-Azani Afisa Ustawi wa Jamii Wilaya ya Mkoani Bimchanga Mussa Mohammed, amesema kumekuwepo na wimbi kubwa la Watoto wanaojishughulisha na shughuli za Uvuvi na kutumikishwa na wafanya biashara hali inayosababisha hali inayochangia Watoto hao kuacha kwenda Skuli.

“Jamani tunatakiwa kuwalea Watoto wetu katika misingi bora ya kijamii na kidini sio kuishia tu kuwatunza tu kwa kuwapa chakula na nguo mtoto usipomsimamia ukahakikisha kuwa anawenda Skuli na madrasa vizuri kinachofata ni kujiingiza katika makundi maovu yakiwemo ya udhalilishaji na uhalifu” alisema

Kwa upande Afisa wa Watu Wenye Wilaya ya Mkoani Warda Wally Mohammed, amesema tafiti zinaonesha matukio mengi ya vitendo vya udhalilishaji katika jamii hutokea kwa Watoto waliyoacha masomo na kujiingiza katika vikundi viovu.

Aidha amewataka Wananchi hao kutokuwaficha watoto Wenye Ulemavu na badala yake kuwatoa ili waweze kuchanganyika na wengine, kipata haki yao ya msingi ya elimu sambamba na kuacha kuwaita majina yasifaa ambayo yanaongeza kuwanyanyapaa.

“Ndugu zangu mtoto anapoacha masomo kuna uwezekanao mkubwa wa kufanyiwa vitendo vya udhalilishaji aidha na Watoto wenzake au hata watu wazima kwasababu anakuwa katika mazingira yasiyo rafiki, tofauti na mtoto ambaye muda mwingi yupo shule au madrasa”

Nae Afisa Maendeleo ya Jamii Wilaya ya Mkoani Bi. Asia Abdalla Said, amewataka wazazi na walezi wa vijiji hivyo kuwasimamia Watoto kwenye suala la elimu ili kupata wataalamu wa fani mbali mbali vijiji humo.

“Jamani sasa hivi miji na vijiji vinapambana kufaulisha wanafunzi ili kupata wataalamu na watumishi wa Umma kutoka maeneo yao kwani unapokwenda sehemu kutaka huduma unapomkuta mtu kutoka kwenu roho inakutua pia anapokuwepo hapa mtaani mutapata nafuu ya kwenda kutafuta masafa ya mbali” alisisitiza

Nae afisa Dawati la Jinsia Polisi Mkoani Rehema Omar Mjawiri, wiriamewataka wananchi hao kutokuwa na muhali na vitendo vya udhalilishaji wa Watoto ili kuwaepusha na athari za hivyo ambavyo vinaonekana kushamiri.

“Niwasihi sana kuwalinda Watoto wenu na viashiria vya vitendo vya udhalilishaji kwanini nasema viashiria, kwasababu mtoto akishadhalilishwa ni vigumu kurudi katika hali yake ya zamani hali inayochangia kuathirika kisaikolojia na kutokutimiza ndoto zao”

Sheha (Mwenyekiti) wa Shehia (Kata) Wambaa Mohammed Suleiman, amewaomba wazazi na walezi kuyafanyia kazi miongozo na maelekezo walipewa na maafisa hayo ili kuwa na jamii yenye ustawi bora.

“Tayari wenzetu wameshamitimiza jukumu lao la kutufikishia ukumbusho, sasa ni juu yetu kuyafanyia kazi maelekezo na miongozo waliotufikishia tusisubiri yatufike kisha twende maofisini kwao kuomba msaada wa ushauri huo sio uungwana” Sheha Wambaa

Nao baadhi ya wananchi wa vijiji hivyo walisema miongoni mwa sababu zinachangia Watoto wao kuacha masomo ni pamoja wazazi kutokutambua jukumu lao la malezi sambamba na kutoa vitisho kwa watu wanaosimamia malezi ya watoto wakiwemo Polisi Jamii.

“Kwakweli asilimia 90% ya wazazi tunakiri kuwa hatutambui jukumu yetu kwa Watoto wetu zaidi ya kulisha na kuvisha lakini ni wachache sana miongoni mwetu ambao wanatambua kuwa mtoto kwenda skuli na chuoni ni jukumu lake la msingi cha kusikitisha zaidi hata wale Polisi jamii ambao kwa hiari yao bila ya malipo wanajitolea kupambana na vitendo viovu ikiwemo Watoto kutokwenda skuli na kuiba baadhi ya wazazi wanawatishia amani Polisi Jamii” Kiongozi wa Polisi Jamii Kijiji cha Kutukuu Ussi Haji 

Mkutano huo umefanyika kufuatilia mwandishi wa Habari hizi kushuhudia idadi kubwa ya Watoto wasio na maendeleo mazuri ya kielimu pamoja na walioacha masomo.


MWISHO

 

Comments

Popular posts from this blog

MWANAMKE AJINYONGA, SABABU WASI WASI - PEMBA

NA, HASSAN MSELLEM - PEMBA PICHA KUTOKA MAKTABA Mwanamke aliyefahamika kwa jina la Raya Darusi Abdallla miaka 48, mkaazi wa Mbuzini Wilaya ya Chake Chake Mkoa wa Kusini Pemba, amefariki Dunia kwa kidaiwa kujinyonga kutokana na Msongo wa mawazo. Tukio Hilo limetokea Novemba 30.2025 saa 11 alfajiri huko Mbuzini Wilaya ya Chake Chake Mkoa wa Kusini Pemba. Omar Salum Ali, ambaye ni shemeji wa marehemu amesema kabla ya marehemu alikuwa na sumbuliwa na Msongo wa mawazo kutokana na kumpoteza kaka yake ambaye alifariki hivi karibuni, kugundulika kuwa ana maradhi ya sukari, mtoto wake wa kiume wa miaka 25, kuwa na ugonjwa akili hali iliyopelekea kupatwa na Msongo wa mawazo na kuamua kujinyonga. Katibu wa Sheha (Katibu wa Mwenyekiti) Shehia ya Mbuzini Yakub Ali Msabah, amesema alipata taarifa za tukio Hilo kutoka kwa Sheha wa Mbuzini kuhusu tukio baada ya kufika eneo la tukio waliukuta mwili wa Mama huyo ukiwa unanin'gia kwenye dari ya Nyumba ambayo alikuwa anaishi zamani. Kutoka tarehe 18 ...

Mariam Muhene – mfano wa kuigwa kwa wanawake kwenye ulingo wa siasa ni

MAKALA NA, HASSAN MSELLEM -PEMBA Tangu Tanzania iruhusu mfumo wa vyama vingi mwaka 1992, Mariam Muhene alijiunga na chama cha Civic United Front (CUF) ambapo mwaka 1995, aligombea nafasi ubunge wa viti maalumu na kuvuka hatua zote ikiwemo kula kiapo mahkamani lakini hakufanikiwa kukikalia kiti hicho. “Mwaka 1995 niligombea ubunge wa viti maalum na nikapita kila kipengele mtu wa kwanza wilaya, taifa bodi ya uongozi, nikala kiapo mahkmanai lakini katika nafasi mbili zilizoletwa kwa kila mkoa Kusini na Kaskazini Pemba mimi sikubahatika” amesema  Safari yake ya kisiasa za upinzani iliendelea na mnamo mwaka 2000, aligombea nafasi ya ubunge wa kuchahguliwa kupitia chama cha Allience for Democratic Change (ADC) Jimbo la Chake Chake lakini kutokana na changamoto zilizojitokeza ikiwe mawakala wa Chama chake kutokuruhisiwa kuingia kwenye vya kupiga kura jambo ambalo amesema lilichangia kukosa nafasi hiyo. Kwasasa Mariam Mohammed Muhene anashika nafasi ya Kamishna wa ADC kanda ya Pemba, nafas...

WATOTO KUJINYONGA ZANZIBAR, UTAFITI WAHITAJIKA.

HABARI NA, HASSAN MSELLEM, PEMBA Picha kutoka mtandaoni Visa vya watoto kujinyonga vimeanza kuwatia khofu na mashaka wazazi na walezi katika Visiwa vya Unguja na Pemba. Mashaka na khofu hiyo imeibuka baada ya matukio mawili mfululizo ya watoto wawili mmoja akiwa umri wa miaka (5) na mwengine (9) kuripotiwa kufariki dunia kwa kujinyonga kati ya tarehe 7 na 9 mwezi huu wa kumi mwaka 2025 kupitia kipindi cha Mawio kinachorushwa na Shirika la Utangazaji Zanzibar ZBC kila siku kuanzia saa 12:40 asubuhi. Katika tukio la kwanza mnamo tarehe 7.10.2025 mwandishi Masanja Mabula aliripoti tukio la Fatma Omar Kidere mwenye umri wa miaka tisa (9) mkaazi wa Mtondoo Jeuri Makaangale Wilaya ya Micheweni Mkao wa Kaskazini Pemba, amekutwa amefariki dunia na mwili wake ukiwa unanin’ginia kwa kutumia mtandio Jirani wa marehemu aliyefahamika kwa jina la Khamis Ali, amesema amepata taarifa za tukio hilo akiwa kazini baada ya kupigiwa simu na mke wake kumpa taarifa za kutokea kwa tukio hilo na kuondoka kazin...