“Nimeshiriki michezo tangu nikiwa darasa la tatu kwasasa ni kocha wa timu ya wanawake ya mpira wa miguu maadili yangu ya Kizanzibari yako pale pale” Tamasha Kocha wa timu-Wete Women Club
Makala Na, Hassan Msellem-Pemba Mpira wa Miguu au wengi wanapenda kuita Soka, Kandanda, Ndinga au Kabumbu yote yakiwa ni majina sahihi kwa mujibu wa wapenzi wa mchezo huo. Unachezwa uwanjani ukiwa na jumla ya wachezaji 22 kila timu ikiwa na wachezi 11, lengo la mchezo huu ni wachezaji kumiliki mpira kwa kutumia miguu kwa shebaha ya kufunga goli yani kuingiza mpira kwenye wavu zilizosimamishwa kwenye milingoti mitatu yani kulia, kushoto na juu. Inakadiriwa kuwa mnamo karne ya 21, kulikuwa na wachazaji mpira wapatao milioni 250 kati ya watu bilioni 1.3 Duniani. Mwaka 2010 hadhira ya televisheni ya zaidi bilioni 26 ilitazama mashindano ya kwanza ya kombe ya Soka, fainali za Kombe la Dunia za mwezi wa nne. Licha umaarufu nakupendwa kwake hakukuwa na timu za wanawake na hii nikutokana na asili ya mchezo huo kuchezwa na wanaume huku baadhi ya mataifa kutokana na Mila na Tamaduni zao wakiami wanawake kushiriki katika mchezo huo ni kwenda kinyume na mil ana tamad...