“WAAMBIENI AKINA MAMA WAJE NA WAUME ZAO KLINIKI, WAKIJA BILA YA WAUME ZAO MARA YA PILI MUSIWAPE HUDUMA” MWENYEKITI WA BARAZA LA MJI WETE- ZULFA ABDALLA SAID
Wafanyakazi wa afya wa jamii (CHW) na Wauguzi Kisiwani Pemba wametakiwa kuwahamasisha akina mama kwenda kiliniki na wenza wao ili kuimarisha afya ya mama na mtoto.
Akizungumza na wafanyakazi
hao huko katika ukumbi wa Baraza la Mji Wete Mwenyekiti wa Baraza la Mji Wete Bi.
Zulfa Abdalla Siad, katika ufunguzi wa mradi wa miaka miwili wa Kubadilisha Mtazamo
wa Majukumu ya Kijinsia na Kuimarisha Maisha ya Wanawake na Wajawazito na Wanaonyonyesha
katika familia za Vijijini Pemba unaondeshwa na Jumuiya kupunguza , amesema
tafiti zinaonesha bado kuna ushiriki mdogo wa akina baba kuongozana na wake zao
kwenda kwenye vituo vya afya hali
inayosababisha maendeleo duni ya kiafya ya mama na mtoto.
Aidha Mwenyekiti huyo
amewata wahuduma hao kuwatokuwapatia huduma za afya akina mama ambao
wanashindwa kuongozana na wenzao kwenda kiliniki kwa mara zaidi ya mbili ili kuwashajihisha
akina baba juu ya muhimu wa kuongozana na wake zao kwenda kwenye vituo vya
afya.
Alisema “Ili kuonesha umuhimu wa hili jambo nawaomba wakija akina mama katika vituo vyenu vya afya kwa mara ya kwanza wapeni elimu kuhusu umuhimu wakuja na wenza wao kiliniki lakini wakija kwa mara ya pili musiwape huduma ili kuwaonesha umuhimu wa jambo hilo”
Mratibu wa Jumuiya ya kupunguza
umasikini na kuboresha Maisha ya watu Pemba (PEPOHUDA) Said Mbarouk Juma,
amesema lengo la mradi huo ni kutoa elimu na kuwahamasisha akina baba kushirikiana
na wenzao kwenda katika vituo vya afya ili kuimarisha afya ya mama wajawazito
na mtoto.
“Tumeiona bado kuna tatizo la akina baba kutokuongozana na wenza wao kwenda kwenye vituo vya afya pamoja na kiliniki huku wakidhani jukumu hilo ni la mama peke yao wakati kiuhalisia ni jukumu la wazazi wote” alisema
Kwa upande wake Afisa
Usaili kutoka Ofisi ya Mrajiswa Jumuiya zisizo za Kiserikali Pemba Sada Abuubakar
Khamis, amesema wameamua kushirikiana na jumuiya hiyo kutokana na utekelezaji
wa miradi yenye tija katika jamii ili kufanikishamalengo ya mradi huo kikamilifu.
“Jumuiya Pepohuda ni miongoni mwa Jumuiya tulizozipa usajili Kisiwani Pemba na tunashirikiana nayo kwa ukaribu sana kutokana na uteketelezaji wa miradi yake yenye tija kwa wananchi ili kuona miradi wanayoitekeleza inafanikiwa kwa asilimia mia moja” alisema
Mgeni Seif Mohammed ni
miongoni mwa washiriki wa mkutano huo, ameahidi kufuata maekelezo waliyopatiwa ili
lengo la mradi huo yaweze kufikiwa.
“Tumetakiwa kuwahamasisha akina mama kwenda na wenzao wao kiliniki na mimi nikiwa mshiriki wa mkutano huu naahidi kutekeleza jukumu hilo kadri ya uwezo wangu na bahati mzuri wapo akina baba ambao wanapenda kuongozana na wake zao kwenda kiliniki sema tu jamii kubwa haijapatiwa elimu ya umuhimu wa jambo hilo” Mgeni Seif Mohammed, Mshiriki
Mradi huo wa miaka miwili ambao umeanza mwezi July 2024 na kutarajiwa kukamilika Mwezi December 2026 unaendeshwa na Jumuiya ya kupunguza umasikini na kuboresha Maisha ya watu Pemba (PEPOHUDA) na kufadhiliwa na Shirika la Y+Global kupitia mfuko wa HER VOICE FUND
Comments
Post a Comment