“Bado kuna pengo kubwa kwa Waandishi wa Habari kuandika Habari za mabadililo ya tabia ya Nchi na Usawa wa Kijinsi” Dr. Mzuri Issa Mkurugenzi Tamwa, Zanzibar
Waandishi wa Habari Zanzibar wametakiwa kuongeza bidii katika kuandika Habari zinazohusu Usawa wa Kijinsia na Mabadiliko ya Tabia ya Nchi ili kuleta msukumo wa mabadiliko katika jamii na Taifa.
Akizungumza na Waandishi
wa Habari na wadau mbali mbali Mkutano wa Uchambuzi kwa vyombo vya Habari juu Usawa
wa Kijinsia na Uongozi na Mabadiliko ya Tabia ya Nchi Mkurugenzi wa Tamwa Zanzibar
Dr. Mzuri Issa, amesema tafiti zinaonesha bado kuna nafasi ndogo kwa vyombo vya
Habari kuandika na kuripoti Habari za Usawa wa Kijinsia na Mabadiliko ya Tabia
ya Nchi hali inayobabisha ufahamu mdogo wa jamii katika Nyanja hiyo.
“Utafiti unaonesha
ushiriki wa Waandishi wa Habari kuandika Habari za usawa wa kijinsia na mabadiliko
ya tabia ya nchi bado ni mdogo sana na badala yake waandishi wa Habari wanaelekeza
zaidi macho yao kwenye Habari za udhalilishaji, michezo kiasi kwamba hata
kwenye vyombo vyao Habari za usawa wa kijinsia na mabadiliko ya tabia ya nchi
hazipewi kipaumbele” alisema
Akitoa mapendekezo katika
mkutano huo Mkufunzi wa chuo kikuu cha Zanzibar (ZU) na Mtafiti wa Mazingira na
vyombo vya Habari Salum Suleiman, amependekeza kuboreshwa kwa Sera zitakazowawezesha
wanawake kupewa kipaumbele kushiriki katika shughuli za mabadiliko ya tabia ya
Nchi.
Alisema “Tutokeni kwenye
ile tafsiri kwamba vyombo vya Habari vina jukumu la kuhabarisha, kuelimisha na
kuburudisha na badala yake tutumieni vyombo vyetu kuandika Habari zenye kuleta
mabadiliko Chanya kwenye jamii zetu n ahata taifa kwa ujumla”
Kwa upande wake mwakilishi
kutoka taasisi ya Community Forest Pemba, amesema kutokana shughuli za kibidamu
ikiwemo kilimo na upigaji wa mkaa maeneo mengi ya Kisiwa cha Pemba na Unguja
yameathirika kutokana na mabadiliko ya tabia ya Nchi.
“Kama tunavyofahamu kuwa
kadri siku zinavyosonga idadi ya watu inaoongezeka na shughuli za kibinadamu
zinaongezeka pia ikiwemo ujenzi nakdhalika kwahivyo kuna kila haja ya kubuni
njia mbadala wa kutumia miti kwa kiasi kikubwa katika shughuli zetu za kila
siku ikiwemo nishati za kupikia ili kuepukana na madhara ya mabadiliko ya tabia
ya nchi ambayo kwa kiasi kikubwa yanamuathiri mwanamke” alisema
Nao washiriki wa Mkutano
huo wamependekeza kutolewa kwa mafunzo maalumu kwa Waandishi wa Habari na Wadau
wa Mazingira na Usawa wa Kijinsia ili waweze kuandika na kuripoti Habari hizo
kwa ufanisi.
“Katika Uchambuzi wetu
hapa tumeona kuwa miongoni mwa sababu zinazosababisha vyombo vya Habari kutokuandika
Habari za Usawa wa Kijinsia na Mabadiliko ya tabia ya Nchi ni pamoja na
kutokuwa na ujuzi wa kutosha katika Nyanja hiyo hivyo basi napendekeza
kuandaliwe kwa mafunzo maalumu kwa waandishi wa Habari na wadau wengine waweze
kufahamu kwa kina kuhusu usawa wa kijinsia na mabadiliko ya tabia ya Nchi ili
waweze kaundika Habari hizo kwa ufanisi zaidi na ziweze kuleta tija katika
jamii na taifa kwa ujumla”
Comments
Post a Comment