NA, HASSAN MSELLEM, PEMBA "AMINA" KINARA WA UOGELEAJI BONANZA LA UTALII PEMBA Na, Hassan Msellem, Pemba Ni msichana wa miaka 15, Mkaazi wa Tumbe Mashariki anayesoma kidato cha Pili aliwashangaza wengi walioshiriki mashindo ya mchezo wa kuogelea yaliyofanyika huko Vuma Wimbi katika Pwani ya Msuka Kaskazini mwa Kisiwa Cha Pemba kwa kipawa chake cha kupiga mbizi na kuwashinda wapiga mbizi wenzake 14 na hatimae kuibuka mshindi wa pili. Msichana huyo mwenye umri mdogo zaidi kuliko waogeleaji wote walioshiriki mchezo huo aliwaacha vinywa wazi watu wote waliokuwa wakishuhudia mtanange huo wapasua maji pasi na msaaada wowote wa waongoza mashindano hayo yaliyojumuisha urefu wa mita 20 Baada ya ushindi huo mwandishi wa Makala hii alipata nafasi ya kuzungumza na msichana huyo ilikufahamu siri ya kuibuka mshindi wa pili na kusema kufanya mazoezi kwa bidii ndio siri pekee iliyofanya awe na uwezo wa kupasua mawimbi zaidi kuliko wenzake ambao walionekana mapafu yao kukomaa zaidi na...