Skip to main content

'YUNA CLUB' SKULI YA SEKONDARI UWELENI YAADHIMISHA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI.

 Wanafunzi Kisiwani Pemba wamehimizwa kushirikiana ili kufanya vizuri kwenye masomo sambamba na kutimiza ndoto walizojiwekea

Akizungumza na wanafunzi wa Sekondari wa Klabu za Vijana wa Umoja wa Mataifa Upande wa Zanzibar (YUNA CLUB) huko Skuli ya Sekondari Mkoani Pemba katika maadhimisho ya siku ya wanawake duniani kwa niaba ya Jaji mkaazi wa mahakama Kuu Pemba mratibu wa mahakama ya ardhi Pemba Abdalla Omar shamuhuni, amesema katika mkataba wa kimaitafa wa haki za binadamu, Katiba za nchi na sheria mbali mbali zinapiga vita suala ubaguzi hivyo wanafunzi wanapaswa kushirikiana ili kufikia malengo la kuanzishwa kwa klabu hizo

“Nawasihi sana muwe na mashirikiano popote mulipo mshirikiane na musitengane na msibaguane, kwenye haki za binadamu suala la ubaguzi kuanzia kwenye Katiba zetu na kwenye sheria za kimataifa suala la ubaguzi limekatazwa, kinyume cha kuacha ubaguzi ni kushirikiana na kupendana kwa wema” alisema

Nae Afisa Elimu Wilaya Mohammed Abdalla Omar amesema sera ya elimu Zanzibar imetoa fursa sawa kwa wananfuzi wote ili waweze kupata haki yao ya msingi ya elimu

“Tukizungumzia usawa kwasasa hakuna jinsia ambayo inabaguliwa na kuachwa nyuma kwenye sekta zote ikiwemo sekta ya elimu kuanzia ngazi ya maandalizi, msingi hadi sekondari watu wote wanapata elimu sawa, imefika pahala mpaka Serikali imeunda wizara maalumu inayosimamia mambo yanayowahusu Wanawake na Watoto wakike ili waweze kupatiwa haki zao zote za msingi” afisa elimu Wilaya ya Mkoani Pemba

Mohammed Hassan Ali ni Naibu Mkurugenzi wa Klabu za Vijana Umoja wa Mataifa Upande wa Zanzibar (YUNA CLUB) amesema lengo la kuanzishwa kwa klabu hiyo ni kutoa fursa za maendeleo kwa vijana pindi wanapokuwa masheleni na baada ya kumaliza

Aliongeza” lengo letu nikiwaonesha vijana fursa pindi wanapokuwa mashuleni na hata baada ya kumaliza masomo ili kusudi waweze kuwa wabunifu na kuweza kujitegemea wenyewe”

Kwa upande wake mlezi wa Klabu ya YUNA Skuli ya Uwelini Suleiman Saleh Mohammed, amesema lengo la kuadhimisha siku ya wanawake duniani ni kutoa elimu juu ya umuhimu wa usawa wa kijinsia katika nyanja mbali mbali ikiwemo fursa za uongozi

“Leo tumeadhimisha siku ya Wanawake duniani ambayo kitaifa inaadhimishwa tarahe 8 mwezi March kila mwaka, kwahivyo na sisi kama YUNA CLUB tumeamua kuadhimisha siku hii ya Wanawake ili kukumbushana mambo yanayowahusu Wanawake na Wasicha kama vile kunyimwa, fursa haki zao” mlezi wa Klabu ya YUNA Skuli ya Uwelini Suleiman Saleh Mohammed

Nao baadhi ya wanafunzi walioshiri katika maadhisho hayo ya siku ya Wanawake duniani walisema wamejifunza kuwepo kwa usawa wa kijinsia na uwezeshaji wa Wanawake Nchini

Raya ni mwanafunzi wa Kidato cha sita Skuli ya Sekondari Uweleni alisema “Nichojifunza haswa nikuona kwamba usawa na uwezashaji wa haki za Wanawake upatikana  nchini mzima na duniani mzima kwa ujumla”

"Wanawake kwanza tupaswa tushirikiane kwamba tukishirikiana tutaweza kujipatia maendeleo kwenye maisha yetu” Mwajuma Khamis Haji mwanafunzi wa kidato cha tano skuli ya Kiwani Sekondari

Hidaya Salum Mohammed mwanafunzi wa kidato cha tano Skuli ya Sekondari Shamiani alisema “miongoni mwa changamoto zinazowakabili wanawake na wasichana ni udhalilishaji wa kijinsia pamoja na unyanyapaji hali inayochangia kujiona dhaifu na kutokutumiza ndoto zao walizojiwekea”

Katika maadhimisho hayo ya siku ya Wanawake duniani ambayo huadhimishwa kila ifikapo tarehe8 mwezi March kila mwaka yenye kauli mbiu inayosema WANAWAKE NA WASICHANA 2025 TUIMARISHE HAKI, USAWA NA UWEZESHAJI’ maonesho mbali mbali yalifanyika ikiwemo mchezo wa kuigiza, matumizi wa lugha za kigeni pamoja na maswali na majibu juu ya mambo mbali mbali ya kitaifa na kimataifa.


Comments

Popular posts from this blog

MWANAMKE AJINYONGA, SABABU WASI WASI - PEMBA

NA, HASSAN MSELLEM - PEMBA PICHA KUTOKA MAKTABA Mwanamke aliyefahamika kwa jina la Raya Darusi Abdallla miaka 48, mkaazi wa Mbuzini Wilaya ya Chake Chake Mkoa wa Kusini Pemba, amefariki Dunia kwa kidaiwa kujinyonga kutokana na Msongo wa mawazo. Tukio Hilo limetokea Novemba 30.2025 saa 11 alfajiri huko Mbuzini Wilaya ya Chake Chake Mkoa wa Kusini Pemba. Omar Salum Ali, ambaye ni shemeji wa marehemu amesema kabla ya marehemu alikuwa na sumbuliwa na Msongo wa mawazo kutokana na kumpoteza kaka yake ambaye alifariki hivi karibuni, kugundulika kuwa ana maradhi ya sukari, mtoto wake wa kiume wa miaka 25, kuwa na ugonjwa akili hali iliyopelekea kupatwa na Msongo wa mawazo na kuamua kujinyonga. Katibu wa Sheha (Katibu wa Mwenyekiti) Shehia ya Mbuzini Yakub Ali Msabah, amesema alipata taarifa za tukio Hilo kutoka kwa Sheha wa Mbuzini kuhusu tukio baada ya kufika eneo la tukio waliukuta mwili wa Mama huyo ukiwa unanin'gia kwenye dari ya Nyumba ambayo alikuwa anaishi zamani. Kutoka tarehe 18 ...

Mariam Muhene – mfano wa kuigwa kwa wanawake kwenye ulingo wa siasa ni

MAKALA NA, HASSAN MSELLEM -PEMBA Tangu Tanzania iruhusu mfumo wa vyama vingi mwaka 1992, Mariam Muhene alijiunga na chama cha Civic United Front (CUF) ambapo mwaka 1995, aligombea nafasi ubunge wa viti maalumu na kuvuka hatua zote ikiwemo kula kiapo mahkamani lakini hakufanikiwa kukikalia kiti hicho. “Mwaka 1995 niligombea ubunge wa viti maalum na nikapita kila kipengele mtu wa kwanza wilaya, taifa bodi ya uongozi, nikala kiapo mahkmanai lakini katika nafasi mbili zilizoletwa kwa kila mkoa Kusini na Kaskazini Pemba mimi sikubahatika” amesema  Safari yake ya kisiasa za upinzani iliendelea na mnamo mwaka 2000, aligombea nafasi ya ubunge wa kuchahguliwa kupitia chama cha Allience for Democratic Change (ADC) Jimbo la Chake Chake lakini kutokana na changamoto zilizojitokeza ikiwe mawakala wa Chama chake kutokuruhisiwa kuingia kwenye vya kupiga kura jambo ambalo amesema lilichangia kukosa nafasi hiyo. Kwasasa Mariam Mohammed Muhene anashika nafasi ya Kamishna wa ADC kanda ya Pemba, nafas...

WATOTO KUJINYONGA ZANZIBAR, UTAFITI WAHITAJIKA.

HABARI NA, HASSAN MSELLEM, PEMBA Picha kutoka mtandaoni Visa vya watoto kujinyonga vimeanza kuwatia khofu na mashaka wazazi na walezi katika Visiwa vya Unguja na Pemba. Mashaka na khofu hiyo imeibuka baada ya matukio mawili mfululizo ya watoto wawili mmoja akiwa umri wa miaka (5) na mwengine (9) kuripotiwa kufariki dunia kwa kujinyonga kati ya tarehe 7 na 9 mwezi huu wa kumi mwaka 2025 kupitia kipindi cha Mawio kinachorushwa na Shirika la Utangazaji Zanzibar ZBC kila siku kuanzia saa 12:40 asubuhi. Katika tukio la kwanza mnamo tarehe 7.10.2025 mwandishi Masanja Mabula aliripoti tukio la Fatma Omar Kidere mwenye umri wa miaka tisa (9) mkaazi wa Mtondoo Jeuri Makaangale Wilaya ya Micheweni Mkao wa Kaskazini Pemba, amekutwa amefariki dunia na mwili wake ukiwa unanin’ginia kwa kutumia mtandio Jirani wa marehemu aliyefahamika kwa jina la Khamis Ali, amesema amepata taarifa za tukio hilo akiwa kazini baada ya kupigiwa simu na mke wake kumpa taarifa za kutokea kwa tukio hilo na kuondoka kazin...