TAMWA ZNZ, ZAFELA, CYD Zasherehekea Michezo kwa Maendeleo na Usawa wa Kijinsia Zanzibar.
JAMII imetakiwa kutilia mkazo ushiriki wa watoto katika michezo mbalimbali ili kuwajengea uwezo na kukuza ujuzi wa sitadi za maisha ktika kukabiliana na vikwazo mbalimbali ikiwemo udhalilishaji wa kijinsia. Hayo yameelezwa na wadau katika kongamano la mashindano ya riadha kwa wanafunzi wa skuli mbalimbali za Zanzibar yaliyoandaliwa na Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania, Zanzibar (TAMWA ZNZ) kwa kushirikiana na Idara ya Michezo, Jumuiya ya Wanasheria Wanawake Zanzibar (ZAFELA), Taasisi ya Maendeleo ya Mashirikiano ya Ujerumani (GIZ) na Kituo cha Mijadala kwa Vijana (CYD) kwa lengo la kuhamasisha usawa wa kijinsia katika michezo. Akizungumzia juhudi za kuimarisha usawa wa kijinsia na kuhamasisha michezo kwa maendeleo, Dkt. Mzuri Issa, Mkurugenzi wa TAMWA ZNZ, alisisitiza umuhimu wa kuendeleza na kuhamasisha michezo kwa wote ili kukuza ushiriki wa jinsi zote katika michezo. "Tuwe mifano mizuri ya kuwa na heshima katika jamii, kwasababu sisi tuna nafasi ya kupata mawaidha...