WANAWAKE PEMBA WATAKIWA KUSHIRIKI MCHEZO WA KUOGELEA ILI KUNUFAIKA NA FURSA ZINAZOTOKANA NA MCHEZO HUO.
Wanawake Kisiwani Pemba wametakiwa kushiriki katika mchezo wa kuogelea ili kunufaika na fursa za kiuchumi zinazotokana na mchezo huo.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Wilaya ya Mkoani Khatibu Juma Mjaja wakati akikabidhi zawadi kwa washindi na washiriki wa Bonanza la kuogelea huko katika viwanja vya burudani Furaha Mini Foro Pemba, amesema kupitia mchezo wa kuogelea kuna fursa nyingi za kiuchumi hivyo wanawake wanatakiwa kushiriki katika mchezo huo ili kunufaika na mchezo huo.
“Mchezo wa kuogelea ni miongoni mwa
michezo maarufu sana duniani na una mashindano mengi ya ndani na kimataifa na
chakusikitisha wanaoshiriki mchezo huu mara nyingi wanawakuwa ni wanaume
hususan katika nchi za Afrika, hivyo basi niwasihi sana akina mama mushiriki
mchezo huu kwani una faida nyingi sana ikiwemo faida za kiafya, kujihami,
kifedha n ahata kutembea nchi mbali mbali duniani” alisema
Sambamba na hayo DC Mjaja amewapa
pongezi wanawake watatu kutoka Tumbe Mkoa wa Kaskazini Pemba walioshiriki
Bonanza hilo kuwa wanawake wa mfano kwa wanawake wengine Kisiwani Pemba na
kuwataka wanawake wengine kuiga mfano wa wanawake hao.
“Tukiangalia kwenye Bonanza letu leo
tunao wanawake watatu lakini hawatokei hapa Furaha hii inamaanisha kuwa
wanawake wa Fuhara na viunga vyake bado hatujahamasika na mchezo wa kuogelea
tutafurahi tukiona bonanza la mwakani wanawake wa Furaha, Mvumoni na Vitongoji
nao wanashiriki katika bonanza hili” Mkuu wa Wilaya ya Mkoani Khatib Juma Mjaja
Mkurugenzi wa kampuni ya JAZEERA-MISALI
TOURS & SAFARI Salum Khamis Juma, amesema wameamua kutoa fursa kwa wanawake
kushiriki katika bonanza hilo ili kuweka usawa wa kijinsia pamoja na kuwahamasisha
wanawake wengine kushiriki katika mchezo huo.
Kaije Said Bakar ni mkufunzi wa somo
la kuogelea kwa wanawake amewataka wanawake wenzake kushiriki katika mchezo wa
kuogelea ili kufaidika na fursa za mchezo huo ikiwemo kuwa na afya njema na
kujipatia fedha.
“Mimi ni mwanamke kama wanawake wengine nina mume na watoto 11 lakini nina uwezo mzuri wa kuogelea nina panda mwani katika kina kirefu cha maji napia nawafundisha wanawake wenzangu kuogelea na kama munavyoona hapa leo kuna wenzangu watatu wameshiriki bonanza hili na tayari wemeshazawadiwa fedha taslim elfu 30 sio kidogo kama wangekuwa wako nyumbani wasingeweza kuipata hiyo, kwahivyo nawasihi sana wanawake wenzangu kushiriki ipaswavyo katika mchezo huu” alisema
Comments
Post a Comment