NA, HASSAN MSELLEM, PEMBA
Mahakama ya Kupambana na Makosa ya Udhalilishaji Mkoa wa Kusini Pemba Chake Chake, Jana April 14 imemuhukumu kutumikia Chuo cha Mafunzo Ismail Ussi Makame miaka 19, mkaazi wa Mikarafuuni kwa makosa mawili ya Ubakaji.
Mbele ya Hakimu wa Mahakama hiyo Taki Abdalla Habib, imeelezwa na mwendesha Mashtaka Asia Ibrahim Mohamed, kuwa tarehe 19.12.2025 saa 7:00 za usiku huko Kinyasini Mkoani Wilaya ya Mkoani Mkoa wa Kusini Pemba, mshtakiwa alimbaka msichana wa miaka 16 baada ya kumtorosha msichana huyo kutoka nyumbani kwao na kwenda nae sehemu anayolala, jambo ambalo ni kosa kisheria kwa mujibu wa kifungu cha 108(1)(2) na 109(1) Shehia ya adhabu Sheria Nambari 6 ya mwaka 2018 Sheria ya Zanzibar likiwa ni kosa la kwanza.
Katika kosa la pili, tarehe 20.12.2025 saa 7:30 za usiku mshtakiwa alimbaka tena msichana huyo.
Kesi hiyo ilianza kusikilizwa Mahakamani hapo 06.01.2026 na idadi ya mashahidi 6 walitoa ushahidi ambao haukuacha chembe ya shaka, hivyo Mahakama imemtia hatiani mshtakiwa na kumuhukumu kutumikia chuo cha Mafunzo miaka 30 kwa kosa la kwanza na miaka 30 kwa kosa la pili, hata hivyo Mahakama imeamua adhabu hizo ziende sambamba hivyo mshtakiwa atatumikia Chuo cha Mafunzo miaka 30 mshtakiwa ili iwe fundisho kwake na kwa wengine wenye tabia kama hizo.
Hukumu hii inafikisha jumla ya hukumu saba (7) za makosa ya Udhalilishaji na Ubakaji ambazo zimetolewa na Mahakama ya kupambana na Makosa ya Udhalilishaji Mkoa wa Kusini Pemba Chake Chake kutoka mwezi March, 2026 Hadi May 14.2026 ambapo katika kesi hizo washtakiwa sita (6) ambao wengi wao ni Vijana wenye umri kati ya miaka 18 na 20 walitiwa hatiani na kuhukumiwa vifungo tofauti ikiwemo miaka 15 na 30.

Comments
Post a Comment