Skip to main content

AJISALIMISHA KITUO CHA POLISI KUDAI MTOTO WAKE ALIYEMTUPA.


Novemba 15.2025 kipindi Cha Mawio kiliripoti tukio la mtoto mchanga wakike mweye umri wa wiki moja kutupwa huko Kitope ambapo aliyemtupa mtoto hakufahamika

Hatimae Jana Novemba 21.2025 Mwanamke aliyefahamika kwa jina la Tattu Mohamed mwenye umri wa miaka 26, mkaazi wa Mfenesini Unguja, Zanzibar amejisalimisha katika Kituo cha Polisi Mahonda kudai mtoto wake na kusema sababu zilizopelekea kumtupa mtoto wake ni tatizo la kupatwa na mashetani.

Kamanda wa Polisi Kamishna Msaidizi wa Polisi Mkoa wa Kaskazini Unguja Benedict Mapujila, amesema Mama huyo alikwenda kujisalimisha Kituo Cha Polisi Mahonda na kukiri kuwa yeye ndiye aliyemtupa mtoto huyo kutokana na kupatwa na matatizo ya mashetani ambaye ni mtoto wake Tatu ingawa alimzaa nje ya ndoa.

Aidha Kamanda Mapujila, amesema kumtupa mtoto ni Kosa Kisheria hivyo Jeshi la Polisi litamshtaki Mama ili Sheria ifate mkondo wake na kutoa wito kwa jamii kutokufanya maamuzi ambayo yako kinyume na Sheria na badala yake kufata Sheria ili kupata ufafanuzi ni changamoto zinawakabili.  

Matukio ya watoto kutupwa, kutelekezwa na hata kuuawa yamekuwa yakitokeza mara kwa mara Visiwani Zanzibar, ikumbukwe kuwa Agosti 1.2025 Amina Rashid Abass miaka 22, mkaazi wa Michakweni Shehia ya Kiwani Wilaya ya Mkoani Mkoa wa Kusini Pemba alishikiliwa na Jeshi la Polisi kwa Kosa la kumtumbukiza mtoto wake mchanga kwenye shimo la Choo baada ya kujifungua kwa kile kinachodaiwa kuwa alihisi aibu baada ya kujifungua nje ya ndoa.

Ijumaa Agosti 29.08.2025 saa 1:30 usiku huko eneo la Mkanjuni Chake Chake Mkoa wa Kusini Pemba, alionekana mtoto mchanga anayekadiwa kuwa na wiki moja kutelekezwa pembezoni mwa msikiti na mwezi July 30.2025 Amina Rashid Abass miaka 22, mkaazi wa Michakweni Shehia ya Kiwani Wilaya ya Mkoani Mkoa wa Kusini Pemba alishikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kujifungua na kumtupa mtoto kwenye shimo la choo na kufariki Dunia.

Comments

Popular posts from this blog

MWANAMKE AJINYONGA, SABABU WASI WASI - PEMBA

NA, HASSAN MSELLEM - PEMBA PICHA KUTOKA MAKTABA Mwanamke aliyefahamika kwa jina la Raya Darusi Abdallla miaka 48, mkaazi wa Mbuzini Wilaya ya Chake Chake Mkoa wa Kusini Pemba, amefariki Dunia kwa kidaiwa kujinyonga kutokana na Msongo wa mawazo. Tukio Hilo limetokea Novemba 30.2025 saa 11 alfajiri huko Mbuzini Wilaya ya Chake Chake Mkoa wa Kusini Pemba. Omar Salum Ali, ambaye ni shemeji wa marehemu amesema kabla ya marehemu alikuwa na sumbuliwa na Msongo wa mawazo kutokana na kumpoteza kaka yake ambaye alifariki hivi karibuni, kugundulika kuwa ana maradhi ya sukari, mtoto wake wa kiume wa miaka 25, kuwa na ugonjwa akili hali iliyopelekea kupatwa na Msongo wa mawazo na kuamua kujinyonga. Katibu wa Sheha (Katibu wa Mwenyekiti) Shehia ya Mbuzini Yakub Ali Msabah, amesema alipata taarifa za tukio Hilo kutoka kwa Sheha wa Mbuzini kuhusu tukio baada ya kufika eneo la tukio waliukuta mwili wa Mama huyo ukiwa unanin'gia kwenye dari ya Nyumba ambayo alikuwa anaishi zamani. Kutoka tarehe 18 ...

Mariam Muhene – mfano wa kuigwa kwa wanawake kwenye ulingo wa siasa ni

MAKALA NA, HASSAN MSELLEM -PEMBA Tangu Tanzania iruhusu mfumo wa vyama vingi mwaka 1992, Mariam Muhene alijiunga na chama cha Civic United Front (CUF) ambapo mwaka 1995, aligombea nafasi ubunge wa viti maalumu na kuvuka hatua zote ikiwemo kula kiapo mahkamani lakini hakufanikiwa kukikalia kiti hicho. “Mwaka 1995 niligombea ubunge wa viti maalum na nikapita kila kipengele mtu wa kwanza wilaya, taifa bodi ya uongozi, nikala kiapo mahkmanai lakini katika nafasi mbili zilizoletwa kwa kila mkoa Kusini na Kaskazini Pemba mimi sikubahatika” amesema  Safari yake ya kisiasa za upinzani iliendelea na mnamo mwaka 2000, aligombea nafasi ya ubunge wa kuchahguliwa kupitia chama cha Allience for Democratic Change (ADC) Jimbo la Chake Chake lakini kutokana na changamoto zilizojitokeza ikiwe mawakala wa Chama chake kutokuruhisiwa kuingia kwenye vya kupiga kura jambo ambalo amesema lilichangia kukosa nafasi hiyo. Kwasasa Mariam Mohammed Muhene anashika nafasi ya Kamishna wa ADC kanda ya Pemba, nafas...

WATOTO KUJINYONGA ZANZIBAR, UTAFITI WAHITAJIKA.

HABARI NA, HASSAN MSELLEM, PEMBA Picha kutoka mtandaoni Visa vya watoto kujinyonga vimeanza kuwatia khofu na mashaka wazazi na walezi katika Visiwa vya Unguja na Pemba. Mashaka na khofu hiyo imeibuka baada ya matukio mawili mfululizo ya watoto wawili mmoja akiwa umri wa miaka (5) na mwengine (9) kuripotiwa kufariki dunia kwa kujinyonga kati ya tarehe 7 na 9 mwezi huu wa kumi mwaka 2025 kupitia kipindi cha Mawio kinachorushwa na Shirika la Utangazaji Zanzibar ZBC kila siku kuanzia saa 12:40 asubuhi. Katika tukio la kwanza mnamo tarehe 7.10.2025 mwandishi Masanja Mabula aliripoti tukio la Fatma Omar Kidere mwenye umri wa miaka tisa (9) mkaazi wa Mtondoo Jeuri Makaangale Wilaya ya Micheweni Mkao wa Kaskazini Pemba, amekutwa amefariki dunia na mwili wake ukiwa unanin’ginia kwa kutumia mtandio Jirani wa marehemu aliyefahamika kwa jina la Khamis Ali, amesema amepata taarifa za tukio hilo akiwa kazini baada ya kupigiwa simu na mke wake kumpa taarifa za kutokea kwa tukio hilo na kuondoka kazin...