NA, HASSAN MSELLEM - PEMBA
Tukio Hilo limetokea Novemba 30.2025 saa 11 alfajiri huko Mbuzini Wilaya ya Chake Chake Mkoa wa Kusini Pemba.
Omar Salum Ali, ambaye ni shemeji wa marehemu amesema kabla ya marehemu alikuwa na sumbuliwa na Msongo wa mawazo kutokana na kumpoteza kaka yake ambaye alifariki hivi karibuni, kugundulika kuwa ana maradhi ya sukari, mtoto wake wa kiume wa miaka 25, kuwa na ugonjwa akili hali iliyopelekea kupatwa na Msongo wa mawazo na kuamua kujinyonga.
Katibu wa Sheha (Katibu wa Mwenyekiti) Shehia ya Mbuzini Yakub Ali Msabah, amesema alipata taarifa za tukio Hilo kutoka kwa Sheha wa Mbuzini kuhusu tukio baada ya kufika eneo la tukio waliukuta mwili wa Mama huyo ukiwa unanin'gia kwenye dari ya Nyumba ambayo alikuwa anaishi zamani.
Kutoka tarehe 18 mwezi Novemba 2025 hili ni tukio la tatu la mtu kujinyonga Kisiwani Pemba, likifuatiwa na tukio la mwanzo la tarehe 18 ambapo wasichana wawili wenye umri wa miaka 12, ambao ni mapacha walijinyonga kwenye mti huko Kwale Mpona Wilaya ya Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba kwa kile kilichodaiwa kuwa walipewa majukumu ya kifamilia na mama yao kisha kuchukua hatua hiyo na tukio la pili la tarehe 19 mtoto wa kiume Muhene Seif Muhene miaka 15, kidaiwa kujinyonga kwa kile kilichodaiwa kuwa alikuwa na maradhi ya wasi wasi.

Comments
Post a Comment