Skip to main content

Ongezeko la Madiwani Wanawake Vijana 2025, Tumaini Jipya Wanawake kuwa Viongozi.

MAKALA NA, HASSAN MSELLEM - PEMBA.

Ongezeko la madiwani wanawake katika ngazi mbali mbali Mkoa wa Kusini Pemba limekuwa ishara ya mabadiliko ya kijamii, kiuchumi na kisiasa, pamoja na mwamko mpya wa jamii kutambua uwezo wa wanawake kama viongozi bora na chachu ya maendeleo.

Miongoni mwa Madiwani Wanawake vijana waliopata fursa ya kuteuliwa kushika nafasi hizo na kuwawakilisha Wanawake wenzako vijana ni pamoja Amria Seif Saleh, ambaye ameteuliwa kuwa Diwani wa Baraza la Mji Mkoani na Fatma Khamis Ali, ambaye ni Diwani wa Wadi Kibokoni Vitongoji, wote wakiwa ni vijana chipukizi katika ulingo wa siasa na uongozi Kisiwani Pemba.

Mabadiliko ya Kijamii na Kuongezeka kwa Uelewa katika kipindi cha miaka ya karibuni, kumekuwa na kampeni mbalimbali zinazoendeshwa na mashirika ya kiraia, Serikali na taasisi binafsi zinazolenga kuongeza ushiriki wa wanawake katika uongozi, Elimu kwa jamii kuhusu umuhimu wa usawa wa kijinsia na nafasi ya mwanamke katika maamuzi imechangia kwa kiasi kikubwa kupungua kwa mitazamo ya kimila iliyokuwa ikiwazuia wanawake kushiriki kikamilifu kwenye siasa.

Baadhi ya wananchi wa Jimbo la Chake Chake sasa wana uelewa mpana zaidi kuhusu mchango mkubwa wa viongozi wanawake, hususan katika masuala ya elimu, afya, ustawi wa jamii na ulinzi wa mazingira na ujsiri wao katika Siasa na uongozi.

Ali Omar Ussi miaka 35, mkaazi wa  Mapinduzi Mkoani amesema uteuzi wa Madiwani vijana uteuzi wa Madiwani hao Vijana Wanawake imeleta matumaini na taswira mpya ya ushiri wa vijana kwenye siasa na uongozi huku akiamini kuwa vijana wana uwezo wakufanya makubwa zaidi kuliko wenye umri mkubwa

"Binafsi nimefurahi sana kuona vijana kama Amria ambaye tulikuwa tunapambana pamoja kwenye Chama Leo hii amekuwa Mhe. Diwani wetu kwakweli imetutia moyo sana vijana"

Moja ya sababu kuu za ongezeko la madiwani wanawake ni kuimarika kwa ujasiri na utayari wa wanawake wenyewe kuingia kwenye ushindani wa kisiasa. Wanawake wengi wa Chake Chake wamepata mafunzo ya uongozi, stadi za mawasiliano na mbinu za kampeni, jambo ambalo limewajengea uwezo wa kujitokeza na kugombea nafasi mbalimbali.

Amria Seif Saleh, diwani kijana Baraza la Mji Mkoani amesema uteuzi huo umekuja baada ya Viongozi wa Chama na Serikali kuona uwezo wa vijana siasa na uongozi katika kuwaletea wananchi maendeleo ya kweli wananchi 

"Leo kuwa diwani haikuwa tu ndoto bali imetokana na uwezo mkubwa nilionao ambao umejengwa na Chama changu Cha CCM kwa miaka isiyopungua kumi nami nimekuwa mwanachama msikivu na mtiifu kwa Chama na Viongozi wangu" Amria Seif Saleh Diwani mteule Baraza la Mji Mkoani Pemba

Katibu wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Mkoa wa Kusini Pemba Alisa Ali Salim, amesema kuongeza kwa Wanawake kwenye vyombo vya maamuzi kunatoa taswira ya ongozeko la usawa wa kijinsia katika Siasa na Uongozi ingawa haijafikiwa kwa asilimia 50 kwa 50

"Hatua tuliofikia sio ndogo tukilinganisha na zamani, sasa tunaona kati ya wajumbe 300 walioko Bungeni Wanawake ni zaidi ya mia moja wakati miaka ya nyuma walikuwa hawafiki hata 50 sasa haya yote yatoa picha kuwa Bado hatufikia Ile sera ya 50 kwa 50 lakini hata hapa tulipofika sio padogo" Katibu wa UWT Mkoa wa Kusini Pemba Alisa Ali Salim

Ushindi wa Madiwani Wanawake unatokana na athari mabadiliko makubwa yaliyofanywa na baadhi ya Viongozi Wanawake katika majimbo mbali mbali ya Mkoa huko akiwemo Mwakilishi wa Jimbo la Chambani Bahati Khamis Kombo ni miongoni mwa Viongozi Wanawake vinara wanaowawashia taa ya kijani Wanawake wenzao katika nyanja ya siasa na uongozi kutokana utekelezaji wa sera na ilani ya vyama vyao katika kuwaletea wananchi maendeleo ndani na nje ya majimbo yao.

"Nashukuru kuona nimepata ridha ya wananchi wa Jimbo kwa mara nyengine na hii inadhihirisha wazi kuwa nimetekeleza ipaswavyo ilani ya Chama changu katika kuwaletea maendeleo wananchi wetu basi iwe chachu kwa viongozi wengine Wanawake kufanya vizuri ili tuendelee kuwaaminisha wananchi kuwa Wanawake pia tunaweza kuleta maendeleo" Mwakilishi wa Jimbo la Chambani Bahati Khamis Kombo 

Madiwani wanawake wamekuwa mstari wa mbele kusukuma ajenda za kuimarisha huduma za afya, ikiwemo afya ya mama na mtoto uboreshaji wa elimu, hususan kwa mtoto wa kike miradi ya uhifadhi wa mazingira na usafi wa mji, kwani wao ndio waganga wakuu endapo huduma hizo zikisua sua.

Halima Ali Awesu mkaazi wa Kipitacho Mkoani, amesema kuteuliwa na kushinda kwa viongozi wanawake kunawapa moyo wa kuondokana na shida mbali mbali ikiwemo changamoto ya upatikanaji wa Maji safi na Salama, huduma za Afya na vitambulisho vya Taifa kwani hayo yamekuwa ni matatizo sugu kwao licha ya kuwa na viongozi wanaume kwa miaka mingi

Uwezeshaji wa wanawake kiuchumi kupitia vikundi na mikopo midogo abadiliko haya yamekuwa na matokeo ya moja kwa moja katika kuboresha ustawi wa familia na jamii kwa ujumla.

Pamoja na mafanikio haya, bado kuna changamoto kadhaa zinazoendelea kukwamisha ushiriki wa wanawake. Baadhi ya changamoto hizo ikiwemo vikwazo vya kiuchumi vinavyowafanya wanawake kusita kugombea nafasi, ukosefu wa mtandao mpana wa kisiasa kwa wanawake wapya pamoja na mitazamo hasi ya baadhi ya wanajamii kuhusu uwezo wa wanawake

Hata hivyo, juhudi za Asasi za Kiraia Visiwani Zanzibar kama Vile Chama Cha Waandishi wa Habari Tanzania (TAMWA) upande wa Zanzibar, PEGAO, TUJIPE na ZAFELA na mashirika ya kiraia na viongozi wa dini zinaendelea kusaidia kupunguza changamoto hizi siku hadi siku.

Kaimu Mratib wa TAMWA, Pemba Amina Mohamed Ahmed, amesema ongezeko hilo ni miongoni mwa juhudi zinazofanywa na TAMWA, Zanzibar kwa kushirikiana na Asasi mbali mbali za Kiraia ambazo zimekitoa elimu ya Wanawake kushiriki katika Haki yao ya Siasa na uongozi.

Kwa kuendelea kuwapa wanawake nafasi na kuwaunga mkono kisiasa,. uongozi na kiuchumi kutaongeza Ari na hamasa za wanawake kushiriki katika Haki ya Kisiasa na uongozi wenye mtazamo mpana zaidi, unaogusa mahitaji ya jamii nzima na kuchochea maendeleo endelevu.

Comments

Popular posts from this blog

MWANAMKE AJINYONGA, SABABU WASI WASI - PEMBA

NA, HASSAN MSELLEM - PEMBA PICHA KUTOKA MAKTABA Mwanamke aliyefahamika kwa jina la Raya Darusi Abdallla miaka 48, mkaazi wa Mbuzini Wilaya ya Chake Chake Mkoa wa Kusini Pemba, amefariki Dunia kwa kidaiwa kujinyonga kutokana na Msongo wa mawazo. Tukio Hilo limetokea Novemba 30.2025 saa 11 alfajiri huko Mbuzini Wilaya ya Chake Chake Mkoa wa Kusini Pemba. Omar Salum Ali, ambaye ni shemeji wa marehemu amesema kabla ya marehemu alikuwa na sumbuliwa na Msongo wa mawazo kutokana na kumpoteza kaka yake ambaye alifariki hivi karibuni, kugundulika kuwa ana maradhi ya sukari, mtoto wake wa kiume wa miaka 25, kuwa na ugonjwa akili hali iliyopelekea kupatwa na Msongo wa mawazo na kuamua kujinyonga. Katibu wa Sheha (Katibu wa Mwenyekiti) Shehia ya Mbuzini Yakub Ali Msabah, amesema alipata taarifa za tukio Hilo kutoka kwa Sheha wa Mbuzini kuhusu tukio baada ya kufika eneo la tukio waliukuta mwili wa Mama huyo ukiwa unanin'gia kwenye dari ya Nyumba ambayo alikuwa anaishi zamani. Kutoka tarehe 18 ...

Mariam Muhene – mfano wa kuigwa kwa wanawake kwenye ulingo wa siasa ni

MAKALA NA, HASSAN MSELLEM -PEMBA Tangu Tanzania iruhusu mfumo wa vyama vingi mwaka 1992, Mariam Muhene alijiunga na chama cha Civic United Front (CUF) ambapo mwaka 1995, aligombea nafasi ubunge wa viti maalumu na kuvuka hatua zote ikiwemo kula kiapo mahkamani lakini hakufanikiwa kukikalia kiti hicho. “Mwaka 1995 niligombea ubunge wa viti maalum na nikapita kila kipengele mtu wa kwanza wilaya, taifa bodi ya uongozi, nikala kiapo mahkmanai lakini katika nafasi mbili zilizoletwa kwa kila mkoa Kusini na Kaskazini Pemba mimi sikubahatika” amesema  Safari yake ya kisiasa za upinzani iliendelea na mnamo mwaka 2000, aligombea nafasi ya ubunge wa kuchahguliwa kupitia chama cha Allience for Democratic Change (ADC) Jimbo la Chake Chake lakini kutokana na changamoto zilizojitokeza ikiwe mawakala wa Chama chake kutokuruhisiwa kuingia kwenye vya kupiga kura jambo ambalo amesema lilichangia kukosa nafasi hiyo. Kwasasa Mariam Mohammed Muhene anashika nafasi ya Kamishna wa ADC kanda ya Pemba, nafas...

WATOTO KUJINYONGA ZANZIBAR, UTAFITI WAHITAJIKA.

HABARI NA, HASSAN MSELLEM, PEMBA Picha kutoka mtandaoni Visa vya watoto kujinyonga vimeanza kuwatia khofu na mashaka wazazi na walezi katika Visiwa vya Unguja na Pemba. Mashaka na khofu hiyo imeibuka baada ya matukio mawili mfululizo ya watoto wawili mmoja akiwa umri wa miaka (5) na mwengine (9) kuripotiwa kufariki dunia kwa kujinyonga kati ya tarehe 7 na 9 mwezi huu wa kumi mwaka 2025 kupitia kipindi cha Mawio kinachorushwa na Shirika la Utangazaji Zanzibar ZBC kila siku kuanzia saa 12:40 asubuhi. Katika tukio la kwanza mnamo tarehe 7.10.2025 mwandishi Masanja Mabula aliripoti tukio la Fatma Omar Kidere mwenye umri wa miaka tisa (9) mkaazi wa Mtondoo Jeuri Makaangale Wilaya ya Micheweni Mkao wa Kaskazini Pemba, amekutwa amefariki dunia na mwili wake ukiwa unanin’ginia kwa kutumia mtandio Jirani wa marehemu aliyefahamika kwa jina la Khamis Ali, amesema amepata taarifa za tukio hilo akiwa kazini baada ya kupigiwa simu na mke wake kumpa taarifa za kutokea kwa tukio hilo na kuondoka kazin...