Skip to main content

Posts

"AMINA" KINARA WA UOGELEAJI BONANZA LA UTALII PEMBA

 NA, SALIM FAKI, PEMBA "AMINA" KINARA WA UOGELEAJI BONANZA LA UTALII PEMBA Na, Hassan Msellem, Pemba Ni msichana wa miaka 15, Mkaazi wa Tumbe Mashariki anayesoma kidato cha Pili aliwashangaza wengi walioshiriki mashindo ya mchezo wa kuogelea yaliyofanyika huko Vuma Wimbi katika Pwani ya Msuka Kaskazini mwa Kisiwa Cha Pemba kwa kipawa chake cha kupiga mbizi na kuwashinda wapiga mbizi wenzake 14 na hatimae kuibuka mshindi wa pili. Msichana huyo mwenye umri mdogo zaidi kuliko waogeleaji wote walioshiriki mchezo huo aliwaacha vinywa wazi watu wote waliokuwa wakishuhudia mtanange huo wapasua maji pasi na msaaada wowote wa waongoza mashindano hayo yaliyojumuisha urefu wa mita 20 Baada ya ushindi huo mwandishi wa Makala hii alipata nafasi ya kuzungumza na msichana huyo ilikufahamu siri ya kuibuka mshindi wa pili na kusema kufanya mazoezi kwa bidii ndio siri pekee iliyofanya awe na uwezo wa kupasua mawimbi zaidi kuliko wenzake ambao walionekana mapafu yao kukomaa zaidi na kwa...

GHARAMA ZA VIFAA VYA MICHEZO, KIKWAZA KWA WANAWAKE KUSHIRIKI MICHEZO.

 N A, SALIM HAMAD, PEMBA Gharama za Vifaa vya Michezo ni miongoni mwa kikwazo kinachowafanya wanawake kushiriki michezo mbali mbali Kisiwani Pemba. WAKATI Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na taasisi mbali mbali za kiraia nchini ikiwemo Chama Cha Waandishi wa Habar wanawake Tanzania Zanzibar (TAMWA) zikielekeza nguvu zake katika kuhamasisha wanawake kushiriki michezo, ingawa bado kumekuwa na kikwazo katika upatikanaji wa vifaa vya michezo. Michezo ni jambo zuri ambalo limekuwa na umuhimu wa kipekee katika kuimarisha afya za wananchi. Pia michezo ni suala ambalo serikali na wadau wengine wamekua wakielekeza nguvu zao na kuekeza katika sekta hiyo, hivyo imekua ni kichocheo kikubwa cha kupata fursa ambazo zinaweza kuinua uchumi wa wanamichezo. Kutokana na umuhimu wa michezo hata jukwaa la Beijing kupitia mkutano ulioandaliwa na shirika la UN Women likishirikiana na Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki, wakati wa vikao vya 59 vilitambua pia umuhimu wa michezo na elimu ya mazoezi ya mw...

WASEMAJI WANAWAKE KWENYE TIMU WAONGEZA HAMASA MICHEZONI.

Na Amina Mchezo  Uhamasishaji michezoni unatokana na uwepo  wa watu maalum ambao hutumia muda wao mwingi kutafakari namna gani ya kuwaleta watu karibu na Kwa mbinu gani. Michezo kikawaida huhitaji mvuto mkubwa Kwa jamii kwani uwepo wake huleta furaha na kujuana na watu mbalimbali. Maafisa habar i kwenye michezo wananafasi kubwa ya kutoa taarifa zinazohusu vilabu na wanachama wengine. Inaelezwa kuwa ili upatiwa leseni ya timu yako na shirikisho la mpira wa miguu ni lazima uwe umetimiza vgezo ikiwemo kipengele Cha kuwa na afisa habari wa timu. Huku cha kusikitisha zaidi ni Kuona timu ambazo zinategemewa kibeba Zanzibar hata hawaoni umuhimu. kuwa na afisa habari. Hadi Sasa maafisa wa habari wanawake katika michezo ni wawili tu Kwa Zanzibar huku Timu Zote 16 znazoshiriki ligi kuu Zanzibar hakuna timu yenye msemaji mwanamke, wakati ligi daraja la kwanza Kanda ya unguja timu Moja tu kati ya timu 18 ndio yenye msemaji mwanamke na timu Moja tu ilio mkoa ndio yenye msemaji mwanamke....

VIONGOZI WA 'ACT' KIZUIZINI UWANJA WA NDEGE ANGOLA

Mwenyekiti wa Chama cha ACT-Wazalendo, Othman Masoud Othman na Mwenyekiti wa Chadema Tundu Lissu wanadaiwa kuzuiwa kuingia nchini Angola kushiriki mazungumzo ya Jukwaa la Demokrasia Afrika (PAD).  Othman, ambaye pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar kwenye msafara wake ameambatana na Kiongozi wa ACT-Wazalendo, Dorothy Semu, Waziri Kivuli wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Dk Nasra Nassor Omar na maofisa wengine wa chama hicho. Makamu Mwenyekiti wa ACT Wazalendo-Zanzibar, Ismail Jussa ameliambia Mwananchi leo Alhamisi Machi 13, 2025 kuwa Othman na msafara wake wamezuiwa kwenye Uwanja wa Ndege wa Luanda jijini Angola.   Tayari ACT Wazalendo imetoa taarifa ya kulaani tukio hilo ililoliita la udhalilishaji wa kiongozi huyo huku kamati yake ya uongozi ikikutana kwa dharura kujadili suala hilo, ambalo mamlaka za Angola hazijajitokeza kulizungumzia. Wakati huohuo, Lissu ameandika kwenye ukurasa wake wa X kuwa mamlaka za uhamiaji za Angola zimewazuia na kukataa kuwaruh...

MAREKANI KUFUTA ASILIMIA 80 YA PROGRAMU ZINAZOFADHILIWA NA USAID.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Marco Rubio amesema kuwa zaidi ya asilimia 80 ya programu zinazofadhiliwa na Shirika la Marekani la Misaada ya Kimataifa (USAID) zitafutwa. #AzamTVUpdates Mhariri | John Mbalamwezi

JESHI LA POLISI LAENDELEA KUMSHIKILIA MWAKINYO

JESHI la Polisi Mkoa wa Tanga limetoa sababu ya kuendelea kumshikilia bondia maarufu nchini Hassan Mwakinyo (29), anayetuhumiwa kumshambulia mkazi wa jijini Tanga Mussa Ally akimtuhumu kuwa ni mwizi. Akizungumza na waandishi wa habari Ofisini kwake leo Jumatatu Machi 10, 2025, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Almachius Mchunguzi amesema Mwakinyo anatuhumiwa kumshambulia na kumjeruhi Mussa Ally ambae anadai ni mvuvi alipopita kwenye makazi yake huku akibainisha kuwa uchunguzi utakapokamilika atatoa taarifa kwa vyombo vya habari ikiwa ni sambamba na kumfikisha mahakamani ili ajibu tuhuma zitakazomkabili.  Kamanda Mchunguzi amesemna wamemkamata Mwakinyo kwa tuhuma za kumjeruhi mvuvi, ambapo ni tuhuma za jinai huku akifafanua kuwa mtu yeyote akifanya makosa kama hayo bila kuangalia nafasi yake kwenye jamii, anatakiwa kuchukuliwa hatua za kisheria na suala la umaarufu haliwezi kubadili kile kilichotendeka. “Jeshi la polisi Mkoa wa Tanga linamshikilia Hassan Mwakinyo (29) mkazi wa Sahare...

ALIYEBUNI JINA 'TANZANIA' AFARIKI DUNIA

Aliyebuni jina la taifa la Tanzania, Mohanmmed Iqbal Dar, amefariki Dunia akiwa usingizini jijini Birmingham, Uingereza alikokuwa akiishi akiwa na umri wa miaka 80. Mohammed Iqbal Dar aliyezaliwa Agosti 8, 1944, mjini Tanga, alikuwa mtoto wa Dk Tufail Ahmad Dar, daktari maarufu aliyehudumu katika mikoa ya Tanga na Morogoro nchini Tanzania. Mwaka 1965 alihamia Uingereza alipokuwa akiishi hadi kifo chake. Igbal alishiriki katika shindano la kutafuta jina la Tanzania lililoandaliwa mwaka 1964 kabla ya Muungano ambako yeye alikuwa mmoja wa wanafunzi 80 walioshindana na hatimaye yeye kuibuka mshindi. Akizungumzia jinsi alivyobuni jina TANZANIA enzi za uhai wake Iqbal alisema alichukua herufi tatu kutoka jina la nchi ya Tanganyika yaani TAN na kwa upande wa Zanzibar nikachukua herufi tatu za mwanzo ZAN, kisha nikaunganisha nikapata jina TANZAN. Baada ya hapo alichukua herufi ya kwanza ya jina lake ‘lqbal’ kisha akachukua herufi ya kwanza A ya jina la dini yake yaani Ahmadiya na kuunda jina ...