Skip to main content

"Endeleeni kuandika habari za 'Afya ya Uzazi' ili muisaidie jamii” Zaina Mzee – Mratibu wa Mradi SRHR





NA, HASSAN MSELLEM - PEMBA

Waandishi wa Habari Kisiwani Pemba wametakiwa kuendelea kuandika Habari zinazohusu afya ya uzazi ili kuioa jamii dhidi ya changamoto mbali mbali ikiwemo uzazi wa mpango, lishe, saratani na shingo ya kizazi, matiti nakdhalika.

Akizungumza na waandishi wa Habari huko katika Ofisi za Tamwa Mkanjuni Pemba Mratibu wa mradi wa kukuza upatikanaji wa Haki ya Afya ya Uzazi kwa Wanawake na Wasichana (SRHR) Zaina Abdalla Mzee, katika Mkutano wa kupeana mrejesho baada ya waandishi baada ya kupewa mafunzo na kufanya kazi juu ya mradi huo, amesema licha utolewaji wa elimu ya afya ya uzazi bado jamii inahitaji kuelimishwa zaidi juu ya suala la afya ya uzazi ili kuona umuhimu wa suala hilo na kuwaepusha matatizo mbali mbali yanayoweza kujitokeza.

Kwa upande wake afisa tathmini na ufuatiliaji Mohammed, amewataka waandishi hao kutumia mfumo wa kuzihifadhi kazi wanazozifanya sambamba na kufuatilia ili kupata mrejesho wa kazi hizo.

“naomba niwasisitize kuziweka kazi zenu kwenye mfumo ili tuweze kujua tumefanya kazi ngapi za aina gani lakini pia tufuatilie kazi zetu ili kujua ni kwa namna gani zimechochea mabadiliko katika jamii au kuchukuliwa kwa hatua fulani kutokana na kazi zenu” amesema 

Aidha amewataka Waandishi hao kuendelea kuzisemea changamoto zinazoikumba Sekta ya afya ili kuboresha huduma za afya ya mama na mtoto.

Kwa upande wake msimamizi wa vituo huduma rafiki kwa Vijana Shaame Haji Shaame, amesema katika mwezi Septemba 2025 wamefanikiwa kupata wateja 88 ambao wamejitokeza kupima saratani ya matiti na shingo ya kizazi katika hospitali ya Micheweni na Konde wateja 77, jambo linaloashiria jamii kuwa na muamko juu ya Saratani ya shingo ya Kizazi na Matiti.

Ameongeza kuwa bado kuna ushiriki mdogo wa wanaume katika kujitokeza kupima maradhi mbali mbali.

Fatma Hassan Khamis Msimamizi Wa Vituo Vya Huduma Rafiki Za Vijana, amesema kumekuwa na ongezeko la vijana kuvitumia vituo vya huduma rafiki kwa Vijana kwa ongezeko la asilimia 9% mwaka 2023 na mwaka 2024 ni 11% vijana waliopatiwa elimu ya afya ya uzazi.

Pia amesema Vijana waliotumia njia ya uzazi wa mpango mwaka 2023 walikuwa asilimia 63% na mwaka 2024 walikuwa Vijana aslimia 63.6%

Amesema “inghawa bado kuna changamoto kubwa ya kwenye mambo afya ya uzazi kutokana na baadhi ya wazazi kuwa na uelewa potofu wa kuwapeleka Watoto wajawazito katika vituo vya afya kujifungua na badala yake kutumia dawa za kienyeji kutoa mimba hasa wale wanaopata mimba za mapema kwa khofu kujuilikana kuwa mtoto wake kumbe ni mjamzito hali inayosababisha baadhi yao kupata madhara ya kupoteza damu nyingi na wengine kupoteza maisha” 

Wakitoa maoni katika Mkutano huo baadhi waandishi hao wamesema bado jamii inakabiliwa na matatizo mbali mbali ikiwemo utekelezwaji wa familia, lishe na dhana potofu kuhusu uzazi wa mpango hali inayosababisha ustawi wa jamii kuporomoka

“Binafsi nimekutana mkasa wa baba kuitelekeza familia yake kutokana na ugomvi wa baba na mama, hali hiyo ikasababisha mama kubeba majukumu yote ya familia kwakweli hali yake ilikuwa ngumu sana lakini kwa kushirikiana na wadau mbali mbali tumefanikiwa kuiunganisha familia hiyo na kwasasa” Mwandishi wa Blog ya Pemba ya Leo Fatma Hamad

Mwisho.

Comments

Popular posts from this blog

MWANAMKE AJINYONGA, SABABU WASI WASI - PEMBA

NA, HASSAN MSELLEM - PEMBA PICHA KUTOKA MAKTABA Mwanamke aliyefahamika kwa jina la Raya Darusi Abdallla miaka 48, mkaazi wa Mbuzini Wilaya ya Chake Chake Mkoa wa Kusini Pemba, amefariki Dunia kwa kidaiwa kujinyonga kutokana na Msongo wa mawazo. Tukio Hilo limetokea Novemba 30.2025 saa 11 alfajiri huko Mbuzini Wilaya ya Chake Chake Mkoa wa Kusini Pemba. Omar Salum Ali, ambaye ni shemeji wa marehemu amesema kabla ya marehemu alikuwa na sumbuliwa na Msongo wa mawazo kutokana na kumpoteza kaka yake ambaye alifariki hivi karibuni, kugundulika kuwa ana maradhi ya sukari, mtoto wake wa kiume wa miaka 25, kuwa na ugonjwa akili hali iliyopelekea kupatwa na Msongo wa mawazo na kuamua kujinyonga. Katibu wa Sheha (Katibu wa Mwenyekiti) Shehia ya Mbuzini Yakub Ali Msabah, amesema alipata taarifa za tukio Hilo kutoka kwa Sheha wa Mbuzini kuhusu tukio baada ya kufika eneo la tukio waliukuta mwili wa Mama huyo ukiwa unanin'gia kwenye dari ya Nyumba ambayo alikuwa anaishi zamani. Kutoka tarehe 18 ...

Mariam Muhene – mfano wa kuigwa kwa wanawake kwenye ulingo wa siasa ni

MAKALA NA, HASSAN MSELLEM -PEMBA Tangu Tanzania iruhusu mfumo wa vyama vingi mwaka 1992, Mariam Muhene alijiunga na chama cha Civic United Front (CUF) ambapo mwaka 1995, aligombea nafasi ubunge wa viti maalumu na kuvuka hatua zote ikiwemo kula kiapo mahkamani lakini hakufanikiwa kukikalia kiti hicho. “Mwaka 1995 niligombea ubunge wa viti maalum na nikapita kila kipengele mtu wa kwanza wilaya, taifa bodi ya uongozi, nikala kiapo mahkmanai lakini katika nafasi mbili zilizoletwa kwa kila mkoa Kusini na Kaskazini Pemba mimi sikubahatika” amesema  Safari yake ya kisiasa za upinzani iliendelea na mnamo mwaka 2000, aligombea nafasi ya ubunge wa kuchahguliwa kupitia chama cha Allience for Democratic Change (ADC) Jimbo la Chake Chake lakini kutokana na changamoto zilizojitokeza ikiwe mawakala wa Chama chake kutokuruhisiwa kuingia kwenye vya kupiga kura jambo ambalo amesema lilichangia kukosa nafasi hiyo. Kwasasa Mariam Mohammed Muhene anashika nafasi ya Kamishna wa ADC kanda ya Pemba, nafas...

WATOTO KUJINYONGA ZANZIBAR, UTAFITI WAHITAJIKA.

HABARI NA, HASSAN MSELLEM, PEMBA Picha kutoka mtandaoni Visa vya watoto kujinyonga vimeanza kuwatia khofu na mashaka wazazi na walezi katika Visiwa vya Unguja na Pemba. Mashaka na khofu hiyo imeibuka baada ya matukio mawili mfululizo ya watoto wawili mmoja akiwa umri wa miaka (5) na mwengine (9) kuripotiwa kufariki dunia kwa kujinyonga kati ya tarehe 7 na 9 mwezi huu wa kumi mwaka 2025 kupitia kipindi cha Mawio kinachorushwa na Shirika la Utangazaji Zanzibar ZBC kila siku kuanzia saa 12:40 asubuhi. Katika tukio la kwanza mnamo tarehe 7.10.2025 mwandishi Masanja Mabula aliripoti tukio la Fatma Omar Kidere mwenye umri wa miaka tisa (9) mkaazi wa Mtondoo Jeuri Makaangale Wilaya ya Micheweni Mkao wa Kaskazini Pemba, amekutwa amefariki dunia na mwili wake ukiwa unanin’ginia kwa kutumia mtandio Jirani wa marehemu aliyefahamika kwa jina la Khamis Ali, amesema amepata taarifa za tukio hilo akiwa kazini baada ya kupigiwa simu na mke wake kumpa taarifa za kutokea kwa tukio hilo na kuondoka kazin...