Skip to main content

WALIMU, VIJANA NA WANANCHI WARIDHISHWA NA MGOMBEA UWAKILISHI WA JIMBO LA MTAMBWE-MARIAM ALI RASHID

NA, HASSAN MSELLEM, PEMBA 


Wananchi wa Jimbo la Mtambwe wakiwemo Walimu wa Skuli, Wanafunzi na Vijana, wamesema wanaridhishwa na kasi ya maendeleo inayofanywa na Mgombea wa nafasi ya Uwakilishi kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi CCM Mariam Ali Rashid, kwa kuwapatia misaada mbali mbali ikiwemo Sare, Rim Paper kwa Skuli 10 za Jimbo hilo.

Wakizungumza na Pemba Post Blog kwa nyakati tofauti wananchi hao wamesema moyo wa kujitoa kwa Mgombea huyo kumesaidia kutatua baadhi ya changamoto za ukosefu wa na rim paper hali iliyosaidia kuondokana na changamoto hizo.

Mgombea wa Uwakilishi Jimbo la Mtambwe kwa tiketi ya CCM Bi. Mariam Ali Rashid 

“Ni kweli baadhi ya wanafunzi walikuwa hawana sare lakini Bi. Mariam alikuja kuwapatia sare wanafunzi hao na sasa wanaendelea na masomo vizuri tunamshukuru sana” Mwalimu Mkuu Skuli ya Mleteni Hadija Ali Hamad

Mwalimu Mkuu wa Skuli ya Mleteni, Hadija Ali Hamad

Nae Mtakwimu wa Skuli hiyo Bishara Mbarouk Hamad, alisema Bi. Mariam ni Mgombea wa kwanza kutoa msaada tangu kuanzishwa kwa Skuli hiyo mwaka 2023

“kwakweli Bi. Mariam ni mgombea wa kwanza kabisa kutupa msaada katika skuli yetu tangu ilipoanzishwa mwaka 2020 kwahivyo anaonesha mwanzo nzuri kabla hajapata nafasi ya kuwa mwakilishi, hivyo basi ni Imani yetu kuwa akipata ridhaa ya kuwa muakilishi atatufanyia makubwa zaidi” alisema 

Mtakwimu wa Skuli ya Mleteni, Bishara Mbarouk Hamad

Mwalimu Mkuu wa Skuli za Kijumbani Kisiwani Hamad Khamis Hamad, alisema walikuwa wanakabilishwa na changamoto ya rim paper hasa kipindi cha mitihani ya muhula lakini kupatiwa msaada huo wa rim paper kumetatua changamoto hiyo.

Mwalimu Mkuu wa Skuli za Kijumbani Kisiwani, Hamad Khamis Hamad

Kwa upande wake Mwalimu Mkuu Sekisheni Skuli ya Piki Tauhida Mohammed Hemed, amewaomba wananchi na wanachama wa CCM wa Jimbo la Mtambwe kumchagua Bi. Mariam kutokana na moyo wake wa kujitoa na Uzalendo ili kanufaika na mazuri aliyoyapanga kwa wananchi wa Jimbo hilo

“Mimi ni wasihi tu wananchi wa Jimbo la Mtambwe hasa wanachama wa CCM, kumpa ridhaa Bi. Mariam kuongoza Jimbo hili kwasababu Bi. Mariam ana moyo wa kujitoa na uzalendo kama bado hajapata ridhaa na ameanza kutuonesha mfano nzuri wa kuwasaidia wananchi katika sekta ya elimu je, akipata ridhaa” alisema 

Mkuu wa Sekisheni Skuli ya Piki, Tauhida Mohammed Hemed

Nao wananchi wa Jimbo hilo walisema wanamfahamu Bi. Mariam kama kijana mwenzao mwenye maono na ubunifu katika uongozi na kuahidi kumchagua ili aendeleze juhudi zake za kuwaletea maendeleo.

“Yani ameanza vizuri sana sana kwasababu bado hajawa muakilishi anaanza kuwasaidia wananchi kiasi hichi Imani yetu akipata nafasi wananchi wa Jimbo Mtambwe tutanufaika sana katika Nyanja mbali mbali” Time Shaaban Seif Mkaazi wa Kisiwani 

"Kwakweli Vijana tumeridhika sana kuona kijana mwenzetu shupavu amepewa ridhaa na chama kwenda Barazani kuwakilisha Jimbo letu la Mtambwe pamoja na kutuwakilisha Vijana wenzake kwakweli tunamkubali tunaimani nae tunampenda na tunamuahidi kumchagua kwa kura nyingi sana na tunaamini atashinda kwa kishindo” Mahfudh Sudi Seif Dereva Bodaboda Mzambarauni


Walimu wa Skuli ya Piki, wakiwa na Rim Paper msaada kutoka kwa Mgombea Uwakilishi Jimbo la Mtambwe Bi. Mariam Ali Rashid

Mwisho.



Comments

Popular posts from this blog

MWANAMKE AJINYONGA, SABABU WASI WASI - PEMBA

NA, HASSAN MSELLEM - PEMBA PICHA KUTOKA MAKTABA Mwanamke aliyefahamika kwa jina la Raya Darusi Abdallla miaka 48, mkaazi wa Mbuzini Wilaya ya Chake Chake Mkoa wa Kusini Pemba, amefariki Dunia kwa kidaiwa kujinyonga kutokana na Msongo wa mawazo. Tukio Hilo limetokea Novemba 30.2025 saa 11 alfajiri huko Mbuzini Wilaya ya Chake Chake Mkoa wa Kusini Pemba. Omar Salum Ali, ambaye ni shemeji wa marehemu amesema kabla ya marehemu alikuwa na sumbuliwa na Msongo wa mawazo kutokana na kumpoteza kaka yake ambaye alifariki hivi karibuni, kugundulika kuwa ana maradhi ya sukari, mtoto wake wa kiume wa miaka 25, kuwa na ugonjwa akili hali iliyopelekea kupatwa na Msongo wa mawazo na kuamua kujinyonga. Katibu wa Sheha (Katibu wa Mwenyekiti) Shehia ya Mbuzini Yakub Ali Msabah, amesema alipata taarifa za tukio Hilo kutoka kwa Sheha wa Mbuzini kuhusu tukio baada ya kufika eneo la tukio waliukuta mwili wa Mama huyo ukiwa unanin'gia kwenye dari ya Nyumba ambayo alikuwa anaishi zamani. Kutoka tarehe 18 ...

Mariam Muhene – mfano wa kuigwa kwa wanawake kwenye ulingo wa siasa ni

MAKALA NA, HASSAN MSELLEM -PEMBA Tangu Tanzania iruhusu mfumo wa vyama vingi mwaka 1992, Mariam Muhene alijiunga na chama cha Civic United Front (CUF) ambapo mwaka 1995, aligombea nafasi ubunge wa viti maalumu na kuvuka hatua zote ikiwemo kula kiapo mahkamani lakini hakufanikiwa kukikalia kiti hicho. “Mwaka 1995 niligombea ubunge wa viti maalum na nikapita kila kipengele mtu wa kwanza wilaya, taifa bodi ya uongozi, nikala kiapo mahkmanai lakini katika nafasi mbili zilizoletwa kwa kila mkoa Kusini na Kaskazini Pemba mimi sikubahatika” amesema  Safari yake ya kisiasa za upinzani iliendelea na mnamo mwaka 2000, aligombea nafasi ya ubunge wa kuchahguliwa kupitia chama cha Allience for Democratic Change (ADC) Jimbo la Chake Chake lakini kutokana na changamoto zilizojitokeza ikiwe mawakala wa Chama chake kutokuruhisiwa kuingia kwenye vya kupiga kura jambo ambalo amesema lilichangia kukosa nafasi hiyo. Kwasasa Mariam Mohammed Muhene anashika nafasi ya Kamishna wa ADC kanda ya Pemba, nafas...

WATOTO KUJINYONGA ZANZIBAR, UTAFITI WAHITAJIKA.

HABARI NA, HASSAN MSELLEM, PEMBA Picha kutoka mtandaoni Visa vya watoto kujinyonga vimeanza kuwatia khofu na mashaka wazazi na walezi katika Visiwa vya Unguja na Pemba. Mashaka na khofu hiyo imeibuka baada ya matukio mawili mfululizo ya watoto wawili mmoja akiwa umri wa miaka (5) na mwengine (9) kuripotiwa kufariki dunia kwa kujinyonga kati ya tarehe 7 na 9 mwezi huu wa kumi mwaka 2025 kupitia kipindi cha Mawio kinachorushwa na Shirika la Utangazaji Zanzibar ZBC kila siku kuanzia saa 12:40 asubuhi. Katika tukio la kwanza mnamo tarehe 7.10.2025 mwandishi Masanja Mabula aliripoti tukio la Fatma Omar Kidere mwenye umri wa miaka tisa (9) mkaazi wa Mtondoo Jeuri Makaangale Wilaya ya Micheweni Mkao wa Kaskazini Pemba, amekutwa amefariki dunia na mwili wake ukiwa unanin’ginia kwa kutumia mtandio Jirani wa marehemu aliyefahamika kwa jina la Khamis Ali, amesema amepata taarifa za tukio hilo akiwa kazini baada ya kupigiwa simu na mke wake kumpa taarifa za kutokea kwa tukio hilo na kuondoka kazin...