“TAMWA NA PEGAO” WAWAPIGA PASI WAGOMBEA 35 “WANAWAKE” WA UBUNGE, UWAKILISHI NA UDIWANI-UCHAGUZI 2025.
NA, HASSAN MSELLEM, PEMBA
Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA) upande wa Zanzibar na Jumuiya Utetezi wa Kijinsia na Mazingira Pemba (PEGAO) zimetoa mafunzo ya siku tatu kwa wagombea 37 wanawake kutoka vyama vya Siasa 17 katika nafasi ya Ubunge, Uwakilishi na Udiwani ili waweze kufanya vizuri katika kampeni kuelekea Uchaguzi Mkuu wa 2025.
Akiwasilisha mada ya Kuwajengea uwezo Wagombea Wanawake watakaosimama katika Majimbo ya Uchaguzi Mkuu 2025, huko katika Ukumbi wa Tamwa Mkanjuni Pemba Muezeshaji Bi. Sabahi Mussa Said, amewataka wagombea hao kuishi na agenda na kuzifanyia kazi na kuzijengea uwelewa zaidi ili ziweze kuwafaa wakati wa kampeni.
Aidha amewasihi kuzifahamu Sera mbali mbali na Sheria muhimu kwa mustakbali wa jamii, Wanawake na Taifa kwa Ujumla.
“Wewe ni mwakilishi wa jamii na wananchi hakikisha unazitambua changamoto za jamii na Jimbo lako ili katika ajenda zako uweze kuzipa kipaumbele hapo ndipo wananchi utawagusa na watahamasika na wewe sio changamoto za jamii au Jimbo lako ni Barabara na Kituo cha Afya wewe unaenda kuzungumzia Maji na Skuli Wananchi hawatakuelewa” Bi. Sabahi Mussa Said
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Jumuiya Utetezi wa Kijinsia Pemba (PEGAO) Hafidh Abdi, amesema lengo la mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo wa kujiamini na kujenga hoja wakati wanaponadi Sera zao kwa Wananchi.
Aidha amewataka wagombea hao kuzifahamu Sera na ilani za vyama vyao ili waweze kuandaa ajenda zinazoendana na malengo ya vyama vyao.
“Lengo la mafunzo haya ni kuwajengea uwezo ili muweze kusimama na kujenga hoja kwa wananchi lakini pia kila Chama kina Sera yake rudini katika vyama vyenu muzisome Sera zenu ili muweze kuziwasilisha Sera za vyama vyenu ipaswavyo” Mkurugenzi PEGAO Abdi Said
Mratibu wa PEGAO Bi. Dina Juma Mkota, amewasisitiza wagombea hao kuyafikia makundi yote ikiwemo Watu Wenye Ulemavu na wanaume wa rika la kati ili kupata idadi kubwa ya watu watakaoweza kuwaunga mkono
“Makundi ya Watu Wenye Ulemavu na akina baba yanatengwa linatengwa kwahivyo wanasihi sana munapokwenda kunadi Sera zenu yafikieni makundi yote musibague kwasababu wote wana haki ya kufikiwa na kusikiliza sera zenu” Mratibu wa PEGAO
Nao baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo wamezishukuru taasisi ya Tamwa, Zanzibar na PEGAO kwa kuwapatia mafunzo hayo na kuahidi kuyafanyia kazi ipaswavyo ili kufikia lengo la kuongeza idadi ya wanawake kwenye vyombo vya kutunga Sheria.
“Kwakweli tuemdelee kuzishukuru taasisi ya TAMWA na PEGAO kwa kuendelea kutushika mkono Wanawake kwenye masuala ya Uongozi kwani wao ndio wamechangia kwa kiasi kikubwa hadi leo zaidi ya akina mama ishiriki kutoka vyama mbali mbali vya siasa tupo hapa kwenye mafunzo ya siku tatu tukiwa tumepata ridhaa ya kuviwakilisha vyama vyetu katika nafasi mbali mbali kama vile Ubunge, Uwakilishi na Udiwani hakika haya ni mafanikio makubwa sana kwetu wanawake na Taifa kwa ujumla kwasababu mwanawake ni kiongozi bora na imara sana” Mgombea wa Chama cha ADA TADEA Asha Said Suleiman
Mafunzo hayo ya siku tatu kwa Wagombea Wanawake kutoka vyama 20 vya siasa nchini yameandaliwa na taasisi ya Tamwa, Zanzibar na Jumuiya ya Utetezi wa Kijinsi na Mazingira Pemba (PEGAO) kwa ufadhili wa Ubalozi wa Norway Tanzania ikiwa ni muendelezo wa kuwajengea uwezo Wanawake katika kushiriki katika Siasa, Uongozi pamoja na kukuza Demokrasia.






Comments
Post a Comment