NA, HASSAN MSELLEM, PEMBA Ubalozi wa Norway Nchini Tanzania umekutana na wadau mbali mbali Kisiwani Pemba wakiwemo Viongozi wa Jumuiya zisizo za Kiserikali (NGOs), Wahamasishaji wajamii(CBs) Waandishi wa Habari pamoja na Wagombea Wanawake kutoka vyama vya Siasa kujadili Mafanikio yanayotokana na Mradi wa Uhamasishaji Wanawake kushiriki katika nafasi za Uongozi, Strength Women In Leadership (SWIL). Akizungumza na wadau hao huko katika Ofisi za TAMWA Mkanjuni Pemba Balozi Norway Tanzania Tonnis Tinnes, amesema ripoti zinaonesha mradi huo umewawesha wanawake zaidi ya elfu mbili kupata elimu na hamasa ya kushiriki katika vyama vya siasa na uongozi kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025. Aidha Balozi Tonnis huyo amesema Ubalozi Norway Tanzania utaendelea kushirikiana na wadau hao katika kukuza na kuongeza ushiriki wa Wanawake katika Siasa na Uongozi. Mshauri Mkuu wa Masuala ya Jinsia Anette Otilie kutoka Norway, amesema Ushiriki wa Wanawake katika Siasa, Uongozi na Demokrasia kusaidia katika kwa kiasi...