Skip to main content

“Waandishi zijueni Sheria za habari zenye mapungufu muongeze nguvu kuzitetea ili zifanyiwe mabadiliko” Dc Mjaja

Hassan Msellem.

Mkuu wa Wilaya ya Mkoani Pemba, Khatib Juma Mjaja.


Waandishi wa habari Kisiwani Pemba wametakiwa kuzifahamu Sera na Sheria za habari zilizopitwa na wakati ili kuongeza nguvu katika utetezi na kufanyiwa marekebisho chanya.


Mapema akifungua mafunzo ya siku moja kwa waandishi wa habari Kisiwani Pemba Mkuu wa Wilaya ya Mkoani Khatibu Juma Mjaja, amesema waandishi wa habari ni wadau wakubwa wanaoweza kuleta mabadiliko ya Sheria za habari ambazo zinaonekana kukinzaba na uhuru wa habari na Wanahabari.

Aidha mkuu huyo amewaomba waandishi hao kuzifahamu Sheria za mitandao ya kijamii pamoja na takwimu ili kuandika habari zenye ukweli na kuleta mabadiliko chanya kwa jamii.


 “Kwahivyo wajibu wetu wanahabari nikuzifahamu sheria za habari mbali mbali wengi wetu tunafanyakazi na online media tunafanyakazi za takwimu, kwahivyo ni wajibu wetu kuzifahamu hizo sheria ili tufanye kazi zetu kwa ufanisi” alisema


Kwa upande wake Katibu Mtendaji kutoka Baraza la Habari Tanzania (MCT) Kajubi Mukajanga, amesema ili kuchochea nguvu ya marekebisho na maboresho ya Sheria kandamizi za uhuru wa habari wanahabari hawana budi kuzifahamu Sheria hizo.

“Ni lazima wanahabari wazielewe sheria hizo kwasababu kuna usemi kwamba kutojua sheria sio utetezi pale unapoivunja walau wajue vifungu ambavyo vitawahusu mara Kwa mara” alitoa ushauri


Nae wakili kutoka Baraza la Habari Tanzania Mpale Mpoki, amesema ibara ya 18 ya katiba ya jamhuri ya Muungano ya Tanzania na ile ya Zanzibar imeruhusu uhuru wa kutoa maoni, hivyo basi amesema uhuru wa kutoa maoni ni haki ya msingi ya mwanadamu licha uhuru huo kuminywa kwa baadhi ya wakati.


“Uhuru wa maoni ni kitu cha msingi katika maendeleo na kutafuta ukweli na katika kuimarisha demokrasia na utawala bora” alieleza


 Shifaa Said Hassan ni Afisa program mwandamizi wa baraza la habari Tanzania upande wa Zanzibar, amesema Sheria ya mwaka 1988 ya wakala wa habari na magazeti ni Sheria inayokandamiza uhuru wa habari, hivyo basi amewataka waandishi hao kuendelea kufanya uchechemuzi katika kazi zao ili kuhakikisha mabadiliko katika sheria hizo yanafanyika.


 “Kwahivyo tukingalia tutaona kuwa sheria zimetungwa muda mrefu sana na haziendani tena na mazingira ya sasa katika tasnia ya habari kwahivyo wanahabari ni jukumu letu kuhakikisha tunashirikiana kuandika habari na kufanya vipindi ambavyo vitachochea kufanyiwa marekebisho chanya” alisema


Ameongeza kuwa bado kuna uminywaji mkubwa wa uhuru wa habari nchini kwa waandishi kutokuwa na uhuru wa kufanya kazi zao ipaswavyo ikiwemo kunyimwa taarifa, kupewa vitosho, kupigwa, kutekwa, kunyanyaswa kudhalilishwa pamoja kufungwa kwa vyombo vya habari.


“Kama tunavyofahamu mara kwa mara tunapata taarifa za vyombo vya habari mbali mbali kufungiwa na baadhi ya wanahabari kupigwa na kudhalilishwa hii yote inatoa picha kuwa bado uhuru wa vyombo vya habari na wanahabari hatujakuwa na uhuru wa kuridhisha katika utekelezaji wa majukumu yetu” aliongeza


Akitoa ufafanuzi juu ya tuzo zinazotelewa na baraza hilo Afisa programu kutoka baraza la habari Tanzania (MCT) Saumu Mwalimu, amewaomba wanahabari hao kuandika habari zinazogusa maisha ya wananchi nakuleta mabadiliko chanya katika jamii ili ziweze kuwa na vigezo vya kuchaguliwa kuwania tuzo hizo

“Kama tunavyojua kwamba baraza la habari Tanzania kila mwaka hua tuna mashindano ya kuwania tuzo katika categories mbali mbali hivyo basi niwasihi mufanye kazi zenye kuleta mabadiliko Fulani katika jamii na sio kuandika habari nani kasema ambazo hazimgusi mwananchi wa kawaida” alieleza afisa programu

Afisa programu kutoka Baraza la Habari Tanzania (MCT) akitoa ufafanuzi na historia kuhusu tuzo EjAT zinazotolewa kila mwaka

Essau Kalikubira ni mwandishi wa UGA ONLINE TV, amesema sheria ya usimamizi wa vyombo vya habari vya mtandaoni ni sheria kandamizi kwani inanyima uhuru wa waandishi kuafanyakazi ipaswavyo, hivyo basi ameliomba baraza la habari Tanzania kuendelea kukutana na wadau wa Sheria ili kuifanyia marekebisho Sheria hiyo.

“Kwakweli hii Sheria ya Mitandaoni bado naiyona ni Sheria kandamizi sana kwa waandishi wa habari wa mtandaoni kwasababu inamfanya mwandishi ashindwe kufanyakazi kwa ulaini na haraka kwani kila tukio inamlazimu kutoa taarifa kwa mamlaka husika ndipo aweze kufanyakazi” alisema


Nao waandishi hao wameahidi kuyafanyia kazi mafunzo hayo na kuwa mabalozi wazuri kwenye vyombo vyao ili kuhakikisha wanafanyakazi kwakuzingatia Sheria pamoja na kuongeza nguvu katika uchechemuzi wa marekebisho ya Sheria hizo.

Waandishi wa Habari Pemba wakiwa katika mafunzo ya siku moja ya kuwajengea uwezo Waandishi wa Habari kuhusu Sheria mbali mbali za Habari.


Bado Waandishi wa habari nchini Tanzania wanatumia Sheria kuu za habari ambazo ni Sheria Nambari 5, ya mwaka 1998 ya usajili mawakala wa habari, magazeti na vitabu na Sheria ya tume ya utangazaji Zanzibar nambari 7 ya mwaka 1997 ambazo zinaonekana kuminya uhuru wa Habari na wanahabari

Mwaka 2021, vyombo kadhaa vya Habari kama vile magazeti na runinga vilifungwa kwa nyakati tofauti pamoja na baadhi ya wandishi kunyanyaswa na kupigwa.

 

Miongoni mwa vyombo hivyo ni gazeti la Raia Mwema ambalo lilifungiwa kwa kipindi Cha Siku 30, gazeti la Uhuru siku 14, Wasafi TV miezi 6, kufungiwa Kwa Kipindi Cha Take One Cha Clouds TV kwa kipindi cha miezi 3 pamoja na kupigwa kwa mwandishi wa Habari wa gazeti la Mwananchi Zanzibar Josse Mikofu.

 

Mafunzo hayo ya Siku Moja yaliyojumuisha Wanahabari kutoka vyombo mbali mbali Kisiwani Pemba yameandaliwa na Baraza la Habari Tanzania (MCT).

Afisa Habari kutoka Chama Cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA) Kisiwani Pemba Gaspery Charles, akieleza jinsi alivyowahi kushiri katika tuzo za EJAT nakuibuka mshindi.

 

Comments

Popular posts from this blog

MWANAMKE AJINYONGA, SABABU WASI WASI - PEMBA

NA, HASSAN MSELLEM - PEMBA PICHA KUTOKA MAKTABA Mwanamke aliyefahamika kwa jina la Raya Darusi Abdallla miaka 48, mkaazi wa Mbuzini Wilaya ya Chake Chake Mkoa wa Kusini Pemba, amefariki Dunia kwa kidaiwa kujinyonga kutokana na Msongo wa mawazo. Tukio Hilo limetokea Novemba 30.2025 saa 11 alfajiri huko Mbuzini Wilaya ya Chake Chake Mkoa wa Kusini Pemba. Omar Salum Ali, ambaye ni shemeji wa marehemu amesema kabla ya marehemu alikuwa na sumbuliwa na Msongo wa mawazo kutokana na kumpoteza kaka yake ambaye alifariki hivi karibuni, kugundulika kuwa ana maradhi ya sukari, mtoto wake wa kiume wa miaka 25, kuwa na ugonjwa akili hali iliyopelekea kupatwa na Msongo wa mawazo na kuamua kujinyonga. Katibu wa Sheha (Katibu wa Mwenyekiti) Shehia ya Mbuzini Yakub Ali Msabah, amesema alipata taarifa za tukio Hilo kutoka kwa Sheha wa Mbuzini kuhusu tukio baada ya kufika eneo la tukio waliukuta mwili wa Mama huyo ukiwa unanin'gia kwenye dari ya Nyumba ambayo alikuwa anaishi zamani. Kutoka tarehe 18 ...

"ZU" YAANDAA MAHAFALI YA 23, DISEMBA 17.2025.

HABARI NA, HASSAN MSELLEM - PEMBA UONGOZI WA CHUO KIKUU CHA ZANZIBAR (ZU) UNAYOFURAHA KUWAALIKA WAHITIMU WOTE WA MWAKA WA MASOMO 2024/2025, PAMOJA NA WAZAZI, WALEZI, NDUGU, JAMAA, MARAFIKI, NA WADAU WOTE WA MAENDELEO YA ELIMU KUSHIRIKI KATIKA MAHAFALI YA 23 YA CHUO KIKUU CHA ZANZIBAR (ZU). MAHAFALI HAYO YANATARAJIWA KUFANYIKA SIKU YA JUMAATANO 17 MWEZI DISEMBA 2025, KATIKA KIWANJA CHA CHUO KIKUU TUNGUU KIBELE KUANZIA SAA MBILI ASUBUHI, AMBAPO MGENI RASMI KATIKA MAHAFALI HAYO ANATARAJIWA KUWA RAISI WA ZANZIBAR NA MWENYEKITI WA BARAZA LA MAPINDUZI DKT. HUSSEIN ALI MWINYI. UONGOZI WA CHUO UNAWASHAURI WAHITIMU WOTE KUKAMILISHA TARATIBU ZOTE IKIWA NI PAMOJA NA KUCHUKUWA MAJOHO KUANZIA SIKU YA ALHAMISI YA TAREHE 11 HADI TAREHE 15.  MAZOEZI YA MAHAFALI YANI REHASAL ITAFANYIKA TAREHE 16. WATU WOTE WANAKARIBISHWA KATIKA MAHAFALI HAYO. CHUO KIKUU CHA ZANZIBAR (ZU) NI CHEM CHEM YA MAADILI NA TAALUMA. KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NA SIMU NAMBARI  0714843480/0718321095/0778777878 AHSANTENI

WATOTO KUJINYONGA ZANZIBAR, UTAFITI WAHITAJIKA.

HABARI NA, HASSAN MSELLEM, PEMBA Picha kutoka mtandaoni Visa vya watoto kujinyonga vimeanza kuwatia khofu na mashaka wazazi na walezi katika Visiwa vya Unguja na Pemba. Mashaka na khofu hiyo imeibuka baada ya matukio mawili mfululizo ya watoto wawili mmoja akiwa umri wa miaka (5) na mwengine (9) kuripotiwa kufariki dunia kwa kujinyonga kati ya tarehe 7 na 9 mwezi huu wa kumi mwaka 2025 kupitia kipindi cha Mawio kinachorushwa na Shirika la Utangazaji Zanzibar ZBC kila siku kuanzia saa 12:40 asubuhi. Katika tukio la kwanza mnamo tarehe 7.10.2025 mwandishi Masanja Mabula aliripoti tukio la Fatma Omar Kidere mwenye umri wa miaka tisa (9) mkaazi wa Mtondoo Jeuri Makaangale Wilaya ya Micheweni Mkao wa Kaskazini Pemba, amekutwa amefariki dunia na mwili wake ukiwa unanin’ginia kwa kutumia mtandio Jirani wa marehemu aliyefahamika kwa jina la Khamis Ali, amesema amepata taarifa za tukio hilo akiwa kazini baada ya kupigiwa simu na mke wake kumpa taarifa za kutokea kwa tukio hilo na kuondoka kazin...