Na, Hassan Msellem
MOJA
ya sheria kongwe na inayotajwa kutokwenda sambamba na uhuru wa vyombo vya
habari, ni ile nambari 5 ya mwaka 1988 ya Magazeti, Vitabu na Mawakala wa
Habari Zanzibar.
Ni miaka 34 sasa, sheria hii inaendelea kutumika Zanzibar, na kutajwa kuathiri na kutishia utendaji kazi wawaandishi wa habari visiwani.
HISTORIA.
Sheria
hiyo tokea mwaka 2010, ilianza harakati za kutaka kufutwa, kwa wadau wa habari
kujikusanya pamoja, ili sasa iwe na sheria moya ya habari.
Kwa
wakati huo, tasisi za Baraza la Habari Tanzania ‘MCT’ –ofisi ya Zanzibar, vyama
vya waandishi wa habari, taasisi za haki za binadamu na wizara husika, zilianza
harakati hizo.
Mara
kadhaa, kulikuwa na taarifa kuwa, mwaka ujao au mwakani Zanzibar itapatikana
sheria mpya ya habari, ambayo itakuja kufuta sheria ya Magazeti nambari 5 ya
mwaka 1988 na ile ya Tume ya Utangaazji nambari 7 ya mwaka 1977.
Ilikuchakua takriban miongo miwili, kupita bila Zanzibar kuwa na sheria mpya, ingawa kwa Tanzania bara, wao walifanikiwa kufuta sheria ya Magazeti ya mwaka 1976, na kuwa na sheria ya Huduma ya vyombo vya habari ‘MSA’ ya mwaka 2016.
Kwa miongo miwili, wadau wa habari juhudi zao za kuwa na sheria mpya ya habari ziligonga ukuta, na harakati hizo zikaanza tena miaka ya 2018/2019.
SABABU
ZA WADAU KUFUTWA KWA SHERIA YA MAGAZETI, VITABU NA MAWAKALA WA HABARI NO 5,
1988.
Sheria
hii yenye vifungu 81 na sehem 10, sasa inatimiza miaka 34, tokea kutungwa
kwake, na kwa maana nyingine, vipo vifungu zaidi ya 40, ambavyo vyengine
vinahitaji kufutwa.
Vifungu
vyengine vikihitajika kufanyiwa marekebisho na vyengine, vilivyobeba maneno
makali kama uwezo wa waziri, waandishi kudhibitiwa na kufanya uchochezi.
Kwenye sheria hii, ambayo kwa sasa Chama cha Waandishi wa habari Wanawake Tanzania TAMWA-Zanzibar kwa ufadhili wa Internews, wanaharakishwa kufutwa kwa sheria hiyo.
VIFUNGU
KANDAMIZI KWA UHURU WA HABARI.
Moja
ya kifungu ambacho, kwa sasa wadau wanataka kifutwe ni kile cha 43, ambacho
chenyewe, kinaeleza ‘uwezo wa ofisa aliyeidhinishwa’.
Ambapo kwa mujibu wa sheria hiyo, ofisa aliyeidhinishwa ni Polisi mwenye cheo cha Msaidizi Ofisa Mkaguzi au mwenye cheo cha juu ya hapo.
Mchambuzi wa sheria za habari Zanzibar Hawra Shamte, anasema, kwa sasa sheria hiyo na hasa kifungu cha 43 wanakiona, hakina mantiki.
‘’Makosa yote yanayotokana na waandishi wa habari yana sura ya madai na sio jinai, sasa iko wapi nafasi ya Polisi kuingia, kupekua kwenye vyombo vya habari,’’anahoji.
‘’Mfano
kifungu (2) (a) kinaeleza uwezo wa ofisi huyo kuwa ‘anaweza kuingia
sehemu yoyote, jengo, chombo cha ardhini, angani ambamo anaamini kwa maoni kuwa,
mna vifaa vya habari, vilivyopangwa au vitakavyopangwa kukusanyia habari,’’
Hata kifungu kidogo cha 2 (b) kikaongeza kuwa, ofisi huyo anaweza ‘kuchunguza mchakato wowote ambao unaonekana kuelekea kukusanya au kutoa habari yoyote ’.
Kubwa
zaidi ambalo ni ukiukwaji wa uhuru wa habari, kifungu cha (c) kinampa uwezo
ofisi hiyo ‘kumtaka mwandishi wa habari yeyote, kutoa vitendea kazi
vyake, gazeti au waraka ambao, uko chini yake kukabdhi kwake’.
Kifungu
2 (d) ofisi huyo amepewa mamlaka ya ‘kunakili sehemu yoyote ya
vitendea kazi vya waandishi wa habari au akiamiani tu kufanya
hivyo, kuna uhusiano na uchunguuzi wake juu ya kosa chini ya sheria hii’.
Kubwa
zaidi, pia ofisi hiyo kwenye kifungu hicho cha 43 (2) (e) anaweza ‘kuagiza
taarifa zenye uhusiano na uchunguuzi wake kutoka kwa mtu yeyote, ambae anaamini aliajiriwa
au ataajiriwa katika jengo alilokuwa akitunza kumbu kumbu’.
Pamoja
na uwezo huo, ambao wadau wa haki za uhuru wa habari wanaona ni uminywaji wa
haki za waandishi wa habari, sasa kifungu cha 44 kimekuja kumlinda.
Kifungu
hicho 44 (1) kinaeleza kuwa, ‘mtu yeyote atakayempinga, kumzuia, au
kumkwaza kwa ofisa huyo atakuwa ametenda kosa’
Na
adhabu kwa kosa hilo lipo kifungu cha 73, ambapo ni faini ya shilingi 200,000
au kifungo cha miaka miwili chuo cha mafunzo au adhabu zote mbili kwa pamoja.
WADAU WA HABARI WANASEMAJE JUU YA KIFUNGU HIKI.
Kwa
upande wake mwandishi wa habari mwandamizi Zanzibar Rashid Omar Kombo, amesema
kifungu cha sheria kinachomruhusu afisa wa Polisi kuchunguza mchakato wowote au
utendaji wa masuala ya habari kinyume na hati ya mahakama ni Sheria
zinazokinzanza na mikataba mbali mbali ya kikanda na kimataifa juu ya uhuru wa
vyombo vya habari.
“Kimsingi
mataifa yote ya kidekrasia ambayo yanafuata misingi ya demokrasia na utawala
bora masuala ya afisa wa polisi kukamata na kukagua yanahitaji idhini na vibali
vya mahakama afisa wa Polisi hawezi kuwa yeye ndiye anatuhumu na yeye ndiye
anakamata hiyo itakuwa ni Sheria ya ajabu” alisema
Fathiya
Mussa Said ni mratibu wa chama cha waandishi wa habari wanawake Tanzania
Kisiwani Pemba (TAMWA), amesema uwepo wa kifungu cha sheria kinachompa mamlaka
afisa yoyote wa Polisi kufanya ukaguzi wa majengo pamoja na kukamata gazeti ni
kifungu cha sheria ambacho inakandamiza uhuru wa vyombo vya habari na
wanahabari kwa ujumla.
"Lakini sheria yetu ya Mgazeti nambari 5 ya mwaka 1988 ya Zanziba na hasa kifungu cha 43 kinaipinga hata katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984, iliyotoa haki ya kutoa maoni,’’anaeleza
Nihifadhi Issa mwandishi wa Kati Fm Radio, anasema kifungu hicho sio rafiki, na hakitarajii kukiona kwenye sheria mpya ijayo ya habari.
Anasema "studio na vyumba vya habari ni ofisi nyeti kama zilivyonyengine, hivyo
utaratibu wa kuingia, uwepo kama zilivyo ofisi nyingine" anahoji
Mwandishi wa UGA ONLINE TV Essau Simon Kalikubilla, anasema kifungu hicho hakifai kuwepo, maana kinahalalisha ukandamizaji wa uhuru wa waandishi wa habari.
Katibu
Mtendaji wa Baraza la Habari Tanzania ‘MCT’ Kajubi Mukajanga wakati akizungumza
na waandishi wa habari kisiwani Pemba wiki iliyopita, alisisitiza vyombo vya
dola kuwaachia waandishi watekeleze kazi zao.
‘’Kuwapasha habari wananchi juu ya matukio ya ndani na nje ni haki kikatiba, sasa kama kuna sheria au kifungu kinampa uwezo mkubwa Polisi kuingia na kufanya atakavyo sio sahihi,’’anasema.
Mjumbe wa Kamati tendaji wa Jumuiya ya wanawake wenye ulemavu Zanzibar ‘JUWAZA’ Hidaya Mjaka Ali, anasema sheria bora ni chachu ya kupata waandishi wa habari bora.
Kamanda
wa Polisi mkoa wa Kusini Pemba, anasema sio sahihi kwa afisa wa Jeshi la Polisi mwenye cheo chochote anaweza kuvamia ikiwa hakuna viashiria vya uhalifu.
Mwandishi
wa blog ya The Chanzo Najat Omar, alisema sheria hiyo imeshapitwa na wakati na
moja ya vifungu vibaya ni cha 43 na vifungu vyake vidogo.
‘Haiwezekani
suala la haki ya kikatiba ya kupata na kutoa habari, apewe uwezo wa kupindukia
Polisi, juu ya kuingia na kupekua kwenye ofisi za waandishi wa
habari,’’alissema.
Mchambuzi wa sheria za Habari Zanzibar Hawra Shamte wakati akiwasilisha mada ya Sheria zenye mapungufu ndani ya ukumbi wa Tamwa, Pemba alisema kwenye nchi zinazojali kwa vitendo utawala bora na utawala wa sheria, suala la kupata na kutoa habari haliwekewi masharti mazito.
Mwenyekiti
wa klabu ya waandishi wa habari Zanzibar ‘ZPC’ Abdalla Abudull-rahman Mfaume na
mwenzake wa PPC Bakari Mussa Juma, walisema vifungu ambavyo vinampa wasi wasi
waandishi wa Habari katika kutekeleza majukumu yake havipaswi kufumbiwa macho
na badala yake mamlaka husika zinapaswa kusikiliza maoni ya wadau wa Habari na
kuvifanyia marekebisho vifungu na sheria hizo.
Mhariri wa habari wa shirika la Magazeti ya serikali Zanzibar Haji Mwadini aliwahi kusema kuwa, ukuaji wa maendeleo ya taifa lolote duniani, waandishi wa habari mchango wao upo.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kusini Pemba Abdalla Hussein Mussa, alisema Sheria inayomruhusu afisa yeyote wa Jeshi la Polisi anaweza kukamata Gazeti lolote, popote linapopatikana haipo sahihi licha ya kwamba Jeshi la Polisi linajukumu la kusimamia usalama katika eneo husika, na kupendekeza Sheria hiyo ibadilishwe ifanyiwe marekebisho.
Hakimu wa Mahakama ya Mkoa Chake Chake Faraji Shomari Juma, alisema Sheria inayompa ruhusa hakimu kumpa hati inspekta wa Jeshi la Polisi ni sahihi kwani baadhi ya maudhui ya Habari yasipodhibitiwa yanaweza kupelekea athari kubwa.
NINI
KIFANYIKE?
Kaimu Mratibu wa Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar ‘ZLSC’ Pemba Safia Saleh Sultan, anasema lazima kwenye sheria ijayo ya habari, kifungu hicho kifutwe.
‘’Sheria ijayo ya habari, sitamani kurejeshwa kwa kifungu hichi, maana kwa upande mwengine ni kudhoofisha juhudi za waandishi katika kazi zao,’’anasema.
Mkuu
wa wilaya ya Mkoani Khatib Juma Mjaja, anasema sheria bora ya habari huchangia
kuwa na jamii bora na inayofanya uamuzi sahihi.
Zuhura
Juma Said mwandishi wa habari wa Shirika la Magazeti Pemba, anasema sheria hiyo
ya Magazeti, Vitabu na Mawakala wa Habari nambari 5 ya mwaka 1988, imekuwa
kikwazo kwao.
Mwandishi wa habari Plus Fm Radio Khalfan Abdul-kadir, anasema sheria hiyo hasa kwenye upatikanaji wa kibali umekuwa shida.
Mkurugenzi wa TAMWA-Zanzibar Dk. Mzur Issa Ali, anasema ujio wa sheria mpya ya habari vifungu vinavyompa uwezo mkubwa waziri visiwmo.
‘’Ndio
maana TAMWA -Zanzibar kwa kushirikiana na wafadhili wetu Shirika la Internews
Tanzania tunaomradi wa miezi minne, ili kuwawezesha waandishi, kusukuma
upatikanaji wa sheria mpya habari Zanzibar,’’anasema.
Mwisho.

Comments
Post a Comment