Skip to main content

Uhalisia wa sheria zilizobora uendane na mazingira yaliyopo.

 Habari Na, Nihifadhi Issa

Zanzibar.

Mkurugenzi wa chama cha waandishi wa habari wanawake TAMWA Zanzibar Dkt. Mzuri Issa amesema Sheria nambari 5 ya wakala wa habari, magazeti na vitabu ya mwaka 1988, ambayo imefanyiwa marekebisho sheria namba 8 mwaka 1997 sheria hii licha yakuwa ni kongwe imekuwa na mapungufu mengi yanayokwamisha haki na uhuru wa vyombo vya habari Zanzibar. 

Akizungumza katika kikao cha kujadili mapungufu ya sheria zinazokwamisha uhuru wa habari huko katika ukumbi wa TAMWA Tunguu amesema Demokrasia sahihi hutegemea uhuru wa vyombo vya habari unavyoweza kusimamia maslahi ya jamii, ikiwemo uhuru wa kutoa maoni na kujieleza bila ya kuingiliwa pamoja kusambaza taarifa na mawazo ya aina mbalimbali kwa kufuata kanuni zilizowekwa ni haki inayotambuliwa na sheria za kitaifa na kimataifa.

“ikiwa Zanzibar imo ndani ya Tanzania na imeridhia mikataba mbalimbali ambayo inalinda tasnia ya habari ipo haja kufanyika marekebisho kwa sheria ambazo haziendi sambamba na uhuru wa habari ikiwemo sheria hii” alisema 

Dkt MzuriKwa mujibu wa Sheria nambari 5 ya wakala wa habari, magazeti na vitabu ya mwaka 1988, yenye marekebisho ya sheria namba 8 mwaka 1997 katika sheria hii vipo vifungu ambavyo havijatowa uhuru kwa waandishi pia kwa vyombo vya habari kikwemo kifungu cha 14 (1) kilichompa mamlaka mrajisi kumtaka mchapishaji gazeti kupeleka kopi mbili kila siku kwa gharama zake kwa madai ya kuweka kumbukumbu.

Afisa mratibu boresha habari kutoka chama cha waandishi wa habari wanawake tamwa-zanzibar kwa kishirikiana na internews tanzania Zaina Abdalla Mzee uwepo wa sheria hiyo unakinza dhana ya demokrasia na utawala.

“kwanza hii sheria ni kongwe imefikia wakati irekebishwe ili kuchapuza uhuru wa habari ambao tunautaka” 

Waandishi wa habari ndio wahusika wakuu katika hili, Khatib Suleiman ni mwandishi wa habari wa gazeti la Habari Leo anasema vifungu hivyo vya sheria vinarudisha nyuma utendaji wa kazi wa mwandishi wa habari 

“kwa mfano chombo cha habari hakipati mapato kinapata wapi fedha za kupeleka nakala kila siku kupeleka kwa mrajis mimi mawazo yangu ofisi ya mrajis iwe na mtu maalum wa kufuatilia izo habari kama wanataka kuendelea na hiyo sheria” amesema Khatib. 

Wananchi wanayo haki ya kupata habari kupitia vyombo mbalimbali Mfaume muhammed anasema ikiwa vyombo vya habari vitaekewa vikwazo au vizuizi ambavyo si vya lazima itawia vigumu kupata habari 

“lazima vikwazo vingine vitatuliwe ambavyo vinaonekana havina ulazima sana izo nakala mbili ni nyingi wakishindwa kuchapisha na siis wasomaji wa magezeti tutakosa kusoma habari” alifafanua mfaume  

Comments

Popular posts from this blog

MWANAMKE AJINYONGA, SABABU WASI WASI - PEMBA

NA, HASSAN MSELLEM - PEMBA PICHA KUTOKA MAKTABA Mwanamke aliyefahamika kwa jina la Raya Darusi Abdallla miaka 48, mkaazi wa Mbuzini Wilaya ya Chake Chake Mkoa wa Kusini Pemba, amefariki Dunia kwa kidaiwa kujinyonga kutokana na Msongo wa mawazo. Tukio Hilo limetokea Novemba 30.2025 saa 11 alfajiri huko Mbuzini Wilaya ya Chake Chake Mkoa wa Kusini Pemba. Omar Salum Ali, ambaye ni shemeji wa marehemu amesema kabla ya marehemu alikuwa na sumbuliwa na Msongo wa mawazo kutokana na kumpoteza kaka yake ambaye alifariki hivi karibuni, kugundulika kuwa ana maradhi ya sukari, mtoto wake wa kiume wa miaka 25, kuwa na ugonjwa akili hali iliyopelekea kupatwa na Msongo wa mawazo na kuamua kujinyonga. Katibu wa Sheha (Katibu wa Mwenyekiti) Shehia ya Mbuzini Yakub Ali Msabah, amesema alipata taarifa za tukio Hilo kutoka kwa Sheha wa Mbuzini kuhusu tukio baada ya kufika eneo la tukio waliukuta mwili wa Mama huyo ukiwa unanin'gia kwenye dari ya Nyumba ambayo alikuwa anaishi zamani. Kutoka tarehe 18 ...

"ZU" YAANDAA MAHAFALI YA 23, DISEMBA 17.2025.

HABARI NA, HASSAN MSELLEM - PEMBA UONGOZI WA CHUO KIKUU CHA ZANZIBAR (ZU) UNAYOFURAHA KUWAALIKA WAHITIMU WOTE WA MWAKA WA MASOMO 2024/2025, PAMOJA NA WAZAZI, WALEZI, NDUGU, JAMAA, MARAFIKI, NA WADAU WOTE WA MAENDELEO YA ELIMU KUSHIRIKI KATIKA MAHAFALI YA 23 YA CHUO KIKUU CHA ZANZIBAR (ZU). MAHAFALI HAYO YANATARAJIWA KUFANYIKA SIKU YA JUMAATANO 17 MWEZI DISEMBA 2025, KATIKA KIWANJA CHA CHUO KIKUU TUNGUU KIBELE KUANZIA SAA MBILI ASUBUHI, AMBAPO MGENI RASMI KATIKA MAHAFALI HAYO ANATARAJIWA KUWA RAISI WA ZANZIBAR NA MWENYEKITI WA BARAZA LA MAPINDUZI DKT. HUSSEIN ALI MWINYI. UONGOZI WA CHUO UNAWASHAURI WAHITIMU WOTE KUKAMILISHA TARATIBU ZOTE IKIWA NI PAMOJA NA KUCHUKUWA MAJOHO KUANZIA SIKU YA ALHAMISI YA TAREHE 11 HADI TAREHE 15.  MAZOEZI YA MAHAFALI YANI REHASAL ITAFANYIKA TAREHE 16. WATU WOTE WANAKARIBISHWA KATIKA MAHAFALI HAYO. CHUO KIKUU CHA ZANZIBAR (ZU) NI CHEM CHEM YA MAADILI NA TAALUMA. KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NA SIMU NAMBARI  0714843480/0718321095/0778777878 AHSANTENI

WATOTO KUJINYONGA ZANZIBAR, UTAFITI WAHITAJIKA.

HABARI NA, HASSAN MSELLEM, PEMBA Picha kutoka mtandaoni Visa vya watoto kujinyonga vimeanza kuwatia khofu na mashaka wazazi na walezi katika Visiwa vya Unguja na Pemba. Mashaka na khofu hiyo imeibuka baada ya matukio mawili mfululizo ya watoto wawili mmoja akiwa umri wa miaka (5) na mwengine (9) kuripotiwa kufariki dunia kwa kujinyonga kati ya tarehe 7 na 9 mwezi huu wa kumi mwaka 2025 kupitia kipindi cha Mawio kinachorushwa na Shirika la Utangazaji Zanzibar ZBC kila siku kuanzia saa 12:40 asubuhi. Katika tukio la kwanza mnamo tarehe 7.10.2025 mwandishi Masanja Mabula aliripoti tukio la Fatma Omar Kidere mwenye umri wa miaka tisa (9) mkaazi wa Mtondoo Jeuri Makaangale Wilaya ya Micheweni Mkao wa Kaskazini Pemba, amekutwa amefariki dunia na mwili wake ukiwa unanin’ginia kwa kutumia mtandio Jirani wa marehemu aliyefahamika kwa jina la Khamis Ali, amesema amepata taarifa za tukio hilo akiwa kazini baada ya kupigiwa simu na mke wake kumpa taarifa za kutokea kwa tukio hilo na kuondoka kazin...