Skip to main content

TAMWA ILIVYOFANIKIWA KUWAJENGA WAANDISHI VIJANA MASUALA YA WANAWAKE NA UONGOZI.


Na Nihifadhi Abdulla, UNGUJA.

Jitihada mbalimbali zinaendelea kuchukuliwa siku hadi siku kuhakikisha usawa wa kijinsia unachukua nafasi yake kwa kupitia mikataba ya kimataifa, kikanda, sera, sheria, matamko na mbinu nyengine tofautiMpango wa utekelezaji wa beijing katika maelezo ya dhamira namba 7 imeeleza uezeshaji wa mwanamke na ushiriki katika vyombo vya maamuzi kwa kuangalia uwiano wa jinsia ili kuhakikisha wanawake na wanaume wanapata nafasi sawa ya kushiriki katika ngazi zote za maamuzi

 

Aidha Mkataba wa kikanda wa nchi za kusini mwa afrika kifungu cha 12 kinasisitiza ushiriki sawa wa wanawake kufikia asilimia 50/50 kwenye nyanja za maamuzi, pia kifungu namba 13 kinaeleza kuwekwa mikakati madhubuti ya kuwawezesha wanawake kushiriki katika mchakato mzima wa uchaguzi na upigaji kura na kuondosha mila na desturi potofu zinazopingana na maendeleo ya mwanamke katika siasa na uongozi Chama cha waandishi wa habari wanawake 


TAMWA Zanzibar ni taasisi inayotetea mambo mengi ya haki ikiwemo za wanawake katika kuhakikisha kunakuwepo na fursa sawa na kufikia lengo la uongozi wa 50 kwa 50.


Waswahili husema “kidole limoja hakivunji chawa” katika mipango ya TAMWA ya kuwawezesha wanawake kuingia katika uongozi imeamua kushirikiana na waandishi wa habari Vijana visiwani zanzibar ili kuunga nguvu ya pamoja kuhakikisha lengo linafikiwa.


Mkurugenzi wa chama hicho Dkt. Mzuri issa anasema TAMWA wameamua kushirikiana na waandishi hao kwani wananchi wanaviamini vyombo vya habari na vinawafikia waliowengi wa wakati mmoja


Alieleza kuwa kwa kuhakikisha waandishi vijana wanafanya kazi ya kuelimisha jamii kuhusu usawa wa kijinsia kwa uweledi waliwajenga kwa kuwapa mbinu zitakazowasaidia kuandika na kutangaza yatayoibua upatikanaji wa haki hiyo


“waandishi wa habari wanauwanja mpana na wanayajua mengi hivyo tumeamua kushirikiana nao kwa kuwapatia kwanza mafunzo namna bora ya kuandika na kuhamamsisha masuala ya wanawake katika uongozi,“wananchi waliowengi wanaamini vyombo vya habari na wanajifunza pia kipi kimejiri kwa mfano kila sehemu iwe radio, tv, mitandanao ya kijamii na magazeti wakisikia masuala ya 50 kwa 50 wanawake na uongozi tunaimani wanahamisika zaidi” alifafanua Dkt. Mzuri 


Afisa mradi wa kuwawezesha waandishi wa habari vijana kuandika habari za wanawake na uongozi kutoka TAMWA zanzibar (YMF) Tatu Ali Mtumwa amesema waandishi wa habari Vijana wamekuwa chachu ya maendeleo kwa kuhamasisha usawa wa kijinsia ili kufikia 50/50 kwa wanawake na wanaume katika ngazi za maamuzi. 


“tumeamua kulenga zaidi kwa vijana kazi hii inataka moyo ya kupambana na kujitoa ili wawe waandishi bora na wa mfano kuanza sasa na majukumu yao yote ya kila siku kuwa wahamasishaji wa masuala haya ya wanawake na uongozi na mengineyo yenye lengo kutetea haki na kuleta maendeleo”alisema tatu 


Aliendelea kusema kuwa tamwa imewajenga waandishi hao kuandika kazi zao kwa kuzinagtia mikataba Na wawe wajuzi wa kutumia tamwiku ili iwe rahisi kulinganisha hali iliyopo na inayotarajiwa


“sio kama mwanzo hawaandiki lakini tumeona haja ya kuwapatia ujuzi Zaidi wa kutumia matumizi sahihi takwimu kutumia, mikataba na matamko mbalimbali kwani hiyo ni kielelezo tosha kwamba mwandishi anaandika kitu ambacho anauhakika nacho”alifafanua.


Berema Suleiman ni miongoni mwa waandishi wa habari vijana anasema awali alikua akifanya kazi zake kikawaida bila ya kutumia tawimu 


“baada ya kupata elimu kutoka TAMWA mwanzo iliniwia vigumu lakini sasa naona utofauti kwani kazi ambayo inavielelezo huwa na mvuto haichoshi kusoma wala kusikiliza‘‘


Hii imenifanya kujua mambo mengi mfano suala la masheha kumbe ni asilimia ndogo sana ya wanawake mwanzo niliona ni kitu cha kawaida tu sasa nikiaandaa kazi zangu sipati shida kuwasilisha kwa jamii kwani huwa imeshiba takwimu na pia natumia mikataba au sheria kuithibitishia jamii kwamba kitu ninachowasilisha kipo sahihi kisheria’’alieleza Berema 


Mbali na hayo TAMWA Zanzibar imeamua kuchukua juhudi mahususi za kuandaa tuzo ili jamii itambue mchango wa wanawake na uongozi katika sekta mbalimbali ili kuinua hali za wanawake na kuongeza ushiriki wao katika masuala ya uongozi katika ngazi zote za maamuzi kama ilivyoelezwa katika katiba ya nchi, mikataba, na itifaki mbalimbali za kimataifa.


Kwa muda wa miaka mitatu mfululizo sasa hutolewa tuzo hizo za umahiri wa uandishi wa habari za wanawake na uongozi zinazoangazia maeneo mbalimbali ya kupigania haki ya wanawake na mabadiliko ya kufikia 50/50Kwa mwaka huu tuzo hizo zilitolewa machi 9, 2024 katika ukumbi wa SHAA uliopo mkoa wa mjini magharib ambapo jumla ya kazi 529 ziliwasilishwa kutoka vyombo vya habari mbalimbali vya Zanzibar ikiwa na dhamira ya endelevu inayoakisi waandishi wa habari kuongeza sauti za wanawake na kuchangia katika maendeleo yao.


Katika mkutano mkuu wa wanachama wa TAMWA Zanzibar uliofanyika April 4, mwaka huu huko Tunguu Dkt. Mzuri alisema juhudi za TAMWA za kuwajengea uwezo waandishi wa habari vijana zimezaa matunda.


“vijana wetu wa YMF wengi wamewasilisha kazi za kushindanisha na asilimia kubwa walioshinda katika vipengele vile ni wao hii inaonesha dhahiri kuwa tayari wameanza kubobea kwani ushindani ulikuwa mkubwa na wengine ni marra yao ya kwanza kushindanisha kazi zao“


Hatujakosea kuekeza nguvu kwao kwani tayari matunda yameonekana huu usiwe mwanzo kwao bali waendeleze juhudi hizo kama sehemu ya masiha yao katika kuwatetea wanawake kupata haki yao ya uongozi na kufikia usawa wa kijinsia” alieleza Dkt. Mzuri. 


Hassan Msellem mwandishi wa Habari wa Blog ya Pemba Post alisema akiwa mwandishi wa habari kijana TAMWA imemjenga kujiamini katika kazi zake kwa kumuelekeza namna bora ya kuandaa vipindi kwani mwanzo hakuwa mtumiaji wa takwimu huku akieleza kuwa taasisi zinazotetea ghaki za wanawake zinapaswa kuiga juhudi za TAMWA.


“binafsi naipongeza TAMWA kuwa miongoni mwa wanufaika wa mradi hii imenisadia kufanya kazi zangu kwa uweledi tofauti na mwanzo na ikanipelekea kupata ushindi katika tunzo za uandishi wa habari mahiri za takwimu kuhusu masuala ya wanawake na uongozi yalioandaliwa na wenyewe TAMWA


"juhudi hizi zinapaswa kuigwa na taasisi nyengine katika kuhakikisha lengo hasa la usawa wa kijinsia linafikiwa kwa bila ya kuibua na kuonesha uwezo wa mwanamke katika kuongoza hatutofika tunapopataka” alimalizia Hassan na Zuhura Juma Said ambae ni mwandishi kijana alieibuka mshindi katika tuzo hizo kupitia mtandao wa kijamii amesema kabla ya mafunzo hakuwa na uelewa mpana wa masuala ya wanawake na uongozi na mara nyingi alikua akiandika habari kuhusu changamoto zinazowakwamisha wanawake kufikia ndoto za uongozi.


“kiukweli awali nilikua naandika vinavyokwamisha wanawake kuwa viongozi lakini sasa naandika hata kazi wanazozifanya ambazo zinaonesha utendaji na uwajibikaji wao hivyo jamii inaona uwezo wa mwanamke katika uongozi, “naishukuru TAMWA kwa kunipika bila wao nahisi nisingefika hapa wamenipa fursa ambayo nimeona manufaa yake naomba huu usiwe mwanzo iwe ni endelevu kwa wengine ili nao wapate kuandika habari ama makala zenye ubora” alimalizia zuhra 


Mradi uliotekelezwa na TAMWA Zanzibar kwa kushirikiana na shirika la National Endowment for Democracy (NED) wa kuwawezesha waandishi wa habari vijana YMF kuandika habari za wanawake na uongozi umewashirikisha waandishi vijana ishirini na nne (24) kutoka Unguja na Pemba.

Comments

Popular posts from this blog

MWANAMKE AJINYONGA, SABABU WASI WASI - PEMBA

NA, HASSAN MSELLEM - PEMBA PICHA KUTOKA MAKTABA Mwanamke aliyefahamika kwa jina la Raya Darusi Abdallla miaka 48, mkaazi wa Mbuzini Wilaya ya Chake Chake Mkoa wa Kusini Pemba, amefariki Dunia kwa kidaiwa kujinyonga kutokana na Msongo wa mawazo. Tukio Hilo limetokea Novemba 30.2025 saa 11 alfajiri huko Mbuzini Wilaya ya Chake Chake Mkoa wa Kusini Pemba. Omar Salum Ali, ambaye ni shemeji wa marehemu amesema kabla ya marehemu alikuwa na sumbuliwa na Msongo wa mawazo kutokana na kumpoteza kaka yake ambaye alifariki hivi karibuni, kugundulika kuwa ana maradhi ya sukari, mtoto wake wa kiume wa miaka 25, kuwa na ugonjwa akili hali iliyopelekea kupatwa na Msongo wa mawazo na kuamua kujinyonga. Katibu wa Sheha (Katibu wa Mwenyekiti) Shehia ya Mbuzini Yakub Ali Msabah, amesema alipata taarifa za tukio Hilo kutoka kwa Sheha wa Mbuzini kuhusu tukio baada ya kufika eneo la tukio waliukuta mwili wa Mama huyo ukiwa unanin'gia kwenye dari ya Nyumba ambayo alikuwa anaishi zamani. Kutoka tarehe 18 ...

Mariam Muhene – mfano wa kuigwa kwa wanawake kwenye ulingo wa siasa ni

MAKALA NA, HASSAN MSELLEM -PEMBA Tangu Tanzania iruhusu mfumo wa vyama vingi mwaka 1992, Mariam Muhene alijiunga na chama cha Civic United Front (CUF) ambapo mwaka 1995, aligombea nafasi ubunge wa viti maalumu na kuvuka hatua zote ikiwemo kula kiapo mahkamani lakini hakufanikiwa kukikalia kiti hicho. “Mwaka 1995 niligombea ubunge wa viti maalum na nikapita kila kipengele mtu wa kwanza wilaya, taifa bodi ya uongozi, nikala kiapo mahkmanai lakini katika nafasi mbili zilizoletwa kwa kila mkoa Kusini na Kaskazini Pemba mimi sikubahatika” amesema  Safari yake ya kisiasa za upinzani iliendelea na mnamo mwaka 2000, aligombea nafasi ya ubunge wa kuchahguliwa kupitia chama cha Allience for Democratic Change (ADC) Jimbo la Chake Chake lakini kutokana na changamoto zilizojitokeza ikiwe mawakala wa Chama chake kutokuruhisiwa kuingia kwenye vya kupiga kura jambo ambalo amesema lilichangia kukosa nafasi hiyo. Kwasasa Mariam Mohammed Muhene anashika nafasi ya Kamishna wa ADC kanda ya Pemba, nafas...

WATOTO KUJINYONGA ZANZIBAR, UTAFITI WAHITAJIKA.

HABARI NA, HASSAN MSELLEM, PEMBA Picha kutoka mtandaoni Visa vya watoto kujinyonga vimeanza kuwatia khofu na mashaka wazazi na walezi katika Visiwa vya Unguja na Pemba. Mashaka na khofu hiyo imeibuka baada ya matukio mawili mfululizo ya watoto wawili mmoja akiwa umri wa miaka (5) na mwengine (9) kuripotiwa kufariki dunia kwa kujinyonga kati ya tarehe 7 na 9 mwezi huu wa kumi mwaka 2025 kupitia kipindi cha Mawio kinachorushwa na Shirika la Utangazaji Zanzibar ZBC kila siku kuanzia saa 12:40 asubuhi. Katika tukio la kwanza mnamo tarehe 7.10.2025 mwandishi Masanja Mabula aliripoti tukio la Fatma Omar Kidere mwenye umri wa miaka tisa (9) mkaazi wa Mtondoo Jeuri Makaangale Wilaya ya Micheweni Mkao wa Kaskazini Pemba, amekutwa amefariki dunia na mwili wake ukiwa unanin’ginia kwa kutumia mtandio Jirani wa marehemu aliyefahamika kwa jina la Khamis Ali, amesema amepata taarifa za tukio hilo akiwa kazini baada ya kupigiwa simu na mke wake kumpa taarifa za kutokea kwa tukio hilo na kuondoka kazin...