Skip to main content

Mkurugenzi TAMWA ZNZ ataka waandishi wa Habari kutetea upatikanaji Uhuru wa Habari na Kujieleza.

WAANDISHI wa habari wametakiwa kupaza sauti zao kuwatetea wananchi kupitia vyombo vya habari kwa maslahi ya kukuza uhuru wa habari na uhuru wa kujieleza ambao utasaidia kuleta maendeleo ya haraka kwa taifa.

Uhuru huo unaweza kupatikana endapo kutakuwa na sheria rafiki za habari sambamba na waandishi wenyewe kufanya kazi kwa kufuata maadili ya tasnia yao na kuendeleza jukumu la huleta maendeleo kutokana na kuwa kiungo cha kupaza sauti kwa wasio na sauti .

Hayo yameelezwa na Mkurugenzi wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania Zanzibar (TAMWA-ZNZ) Dkt Mzuri Issa Ali wakati wa mafunzo ya siku moja ya kupitia Mikataba ya kikanda na ya Kimataifa na kujadili mapungufu ya sheria zinazokwamisha uhuru wa habari Zanzibar.

Ameeleza kuwa lengo la mafunzo hayo yaliyowakutanisha watendaji wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Vijana na Michezo , Tume ya kurekebisha Sheria Zanzibar, Tume ya Utangazaji na waandishi wa habari ni kukumbushana umuhimu wa kuangalia ni kwa kiasi gani kama nchi imeweza kuzingatia mikataba hiyo ili kupata sheria na sera bora zitakazo simamia masuala ya haki ya kupata habari na kutoa maoni na kukuza demokrasia nchini .     

Aidha amebainisha kuwa pamoja na kuridhia Mikataba ya bado sauti za wananchi hazipewi kipau mbele kusikika katika vyombo vya habari ukilinganisha na sauti za viongozi jambo ambalo linawanyima wananchi haki yao ya kikatiba ya kutoa maoni.

Miongoni mwa mikataba hiyo ni pamoja na Tamko la Kimataifa la Haki za Binadamu (Universal Declaration of Human Rights (UDHR), Mkataba wa Kimataifa wa Haki za Kiraia na Kisiasa (The International Covenant on Civil and Political Rights (ICCPR) na Mkataba wa Haki za Binadamu na Haki za Watu wa Umoja wa Afrika (African Charter on Human and Peoples Rights - ACHPR)

“Nchi nyingi za Afrika zimeweza kupiga hatua za kimaendeleo kwa kuvitumia vyema vyombo vya habari kwa uhuru na kupelekea kuinua uchumi wa nchi ambapo ni pamoja na Ghana, Afrika ya kusini na Mozambique.

Mapema akiwasilisha mada kuhusiana na “Mapungufu ya Sheria za habari” Bibi Hawra Shamte ambae ni mwandishi wa habari mkongwe amesema ingawa kuna sheria zinazosimamia sekta ya habari bado zinaonekana kiuhalisia hazifanyi kazi ipasavyo kwa kulinda usalama wa waandishi wa habari na wananchi hivyo zinahitaji kufanyiwa marekebisho.

“Baadhi ya sheria hizo ni pamoja na Sheria ya Usajili wa Wakala wa Habari, Magazeti na Vitabu No. 5 ya mwaka 1988 iliyofanyiwa marekebisho na sheria No. 8 ya mwaka 1997 na Sheria ya Tume ya Utangazaji Zanzibar No. 7 ya mwaka 1997 iliyofanyiwa marekebisho na sheria No 1 ya 2010”, alieleza muwasilishaji huyo.

Wakichangia katika mafunzo hayo, miongoni mwa waandishi wahabari wamesema wamaekuwa wakikutana na vikwazo mbalimbali katika kufanikisha majukumu yao, hali inayosababisha kukosa uhuru na kutowajibika ipasavyo.

Mafunzo hayo yametolewa na TAMWA-ZNZ kwa watendaji wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Vijana na Michezo,Tume ya kurekebisha Sheria Zanzibar, Tume ya Utangazaji na waandishi wa habari yenye lengo la kuonesha umuhimu wa kuzingatia mikataba ya kikanda na ya kimataifa ili kuwa na sheria na sera bora zitakazo simamia masuala ya haki ya kupata habari na kutoa maoni kwa uhuru.     

Communications Department,

Tanzania Media Women's Association- TAMWA Zanzibar,

Address: P.o. Box 741, Tunguu Zanzibar, 

Mob: +255 675834720 I 

E-mail: gaspary@tamwaznz.or.tz I I

 Web: www.tamwaznz.or.tz

Follow us: Twitter I

 Instagram I YouTube I Facebook  

Comments

Popular posts from this blog

MWANAMKE AJINYONGA, SABABU WASI WASI - PEMBA

NA, HASSAN MSELLEM - PEMBA PICHA KUTOKA MAKTABA Mwanamke aliyefahamika kwa jina la Raya Darusi Abdallla miaka 48, mkaazi wa Mbuzini Wilaya ya Chake Chake Mkoa wa Kusini Pemba, amefariki Dunia kwa kidaiwa kujinyonga kutokana na Msongo wa mawazo. Tukio Hilo limetokea Novemba 30.2025 saa 11 alfajiri huko Mbuzini Wilaya ya Chake Chake Mkoa wa Kusini Pemba. Omar Salum Ali, ambaye ni shemeji wa marehemu amesema kabla ya marehemu alikuwa na sumbuliwa na Msongo wa mawazo kutokana na kumpoteza kaka yake ambaye alifariki hivi karibuni, kugundulika kuwa ana maradhi ya sukari, mtoto wake wa kiume wa miaka 25, kuwa na ugonjwa akili hali iliyopelekea kupatwa na Msongo wa mawazo na kuamua kujinyonga. Katibu wa Sheha (Katibu wa Mwenyekiti) Shehia ya Mbuzini Yakub Ali Msabah, amesema alipata taarifa za tukio Hilo kutoka kwa Sheha wa Mbuzini kuhusu tukio baada ya kufika eneo la tukio waliukuta mwili wa Mama huyo ukiwa unanin'gia kwenye dari ya Nyumba ambayo alikuwa anaishi zamani. Kutoka tarehe 18 ...

Mariam Muhene – mfano wa kuigwa kwa wanawake kwenye ulingo wa siasa ni

MAKALA NA, HASSAN MSELLEM -PEMBA Tangu Tanzania iruhusu mfumo wa vyama vingi mwaka 1992, Mariam Muhene alijiunga na chama cha Civic United Front (CUF) ambapo mwaka 1995, aligombea nafasi ubunge wa viti maalumu na kuvuka hatua zote ikiwemo kula kiapo mahkamani lakini hakufanikiwa kukikalia kiti hicho. “Mwaka 1995 niligombea ubunge wa viti maalum na nikapita kila kipengele mtu wa kwanza wilaya, taifa bodi ya uongozi, nikala kiapo mahkmanai lakini katika nafasi mbili zilizoletwa kwa kila mkoa Kusini na Kaskazini Pemba mimi sikubahatika” amesema  Safari yake ya kisiasa za upinzani iliendelea na mnamo mwaka 2000, aligombea nafasi ya ubunge wa kuchahguliwa kupitia chama cha Allience for Democratic Change (ADC) Jimbo la Chake Chake lakini kutokana na changamoto zilizojitokeza ikiwe mawakala wa Chama chake kutokuruhisiwa kuingia kwenye vya kupiga kura jambo ambalo amesema lilichangia kukosa nafasi hiyo. Kwasasa Mariam Mohammed Muhene anashika nafasi ya Kamishna wa ADC kanda ya Pemba, nafas...

WATOTO KUJINYONGA ZANZIBAR, UTAFITI WAHITAJIKA.

HABARI NA, HASSAN MSELLEM, PEMBA Picha kutoka mtandaoni Visa vya watoto kujinyonga vimeanza kuwatia khofu na mashaka wazazi na walezi katika Visiwa vya Unguja na Pemba. Mashaka na khofu hiyo imeibuka baada ya matukio mawili mfululizo ya watoto wawili mmoja akiwa umri wa miaka (5) na mwengine (9) kuripotiwa kufariki dunia kwa kujinyonga kati ya tarehe 7 na 9 mwezi huu wa kumi mwaka 2025 kupitia kipindi cha Mawio kinachorushwa na Shirika la Utangazaji Zanzibar ZBC kila siku kuanzia saa 12:40 asubuhi. Katika tukio la kwanza mnamo tarehe 7.10.2025 mwandishi Masanja Mabula aliripoti tukio la Fatma Omar Kidere mwenye umri wa miaka tisa (9) mkaazi wa Mtondoo Jeuri Makaangale Wilaya ya Micheweni Mkao wa Kaskazini Pemba, amekutwa amefariki dunia na mwili wake ukiwa unanin’ginia kwa kutumia mtandio Jirani wa marehemu aliyefahamika kwa jina la Khamis Ali, amesema amepata taarifa za tukio hilo akiwa kazini baada ya kupigiwa simu na mke wake kumpa taarifa za kutokea kwa tukio hilo na kuondoka kazin...