Skip to main content

Kamati ya wataalamu wa masuala ya habari Zanzibar yaongeza kasi ufuatiliaji marekebisho sheria za habari.

Kamati ya wataalamu wa masuala ya habari Zanzibar (ZAMECO) imekuwa mstari wa mbele katika jitihada za kufuatilia mchakato wa marekebisho ya sheria za habari ikiwemo sheria ya Utangazaji No. 7 ya 1997, ambayo ilifanyiwa marekebisho na sheria No. 1 ya 2010.

Katika vikao mbalimbali ZAMECO ilitoa mapendekezo kuhusu marekebisho ya sheria hio kwa lengo la kupatikana sharia mpya na rafiki kwa waandishi wa habari na vyombo vya habari nchini.

Aidha mnamo tarehe 9/4/2024 ZAMECO wamefika katika afisi za Tume ya kurekebisha Sheria Zanzibar iliyopo Vuga kwa ajili ya kufuatilia hatua iliyofikiwa baada ya kupokea mapendekezo hayo mwezi wa Octoba mwaka 2023.

Mratibu wa Baraza la Habari Tanzania (MCT) kwa upande wa Zanzibar Shifaa Said ameeleza kuwa hatua hii ya ufuatiliaji imechukuliwa ili kuhakikisha kwamba mchakato wa kupata rasimu ya sharia ya Utangazaji unakwenda vizuri na hatimae sheria mpya itayokidhi vigezo vya kihabari ipatikane.

Kwa upande wake, Salim Said, mwandishi wa habari mkongwe amesisitiza kwamba vyombo vya habari havina nia mbaya na serikali, bali ni washirika muhimu katika kuleta maendeleo kwa jamii hivyo jitihada za ZAMECO na wengine katika kuendeleza maboresho ya sheria ya Utangazaji zinachukuliwa kama sehemu ya ushirikiano mzuri kati ya vyombo vya habari na serikali.

“Vyombo vya habari havina uadui na Serikali, sisi ni washirika wazuri na wenye lengo jema kwa jamii na nchi kwa ujumla, kwa kuzingatia vyombo vya habari ni nguzo ya maendeleo ya uchumi” Alisema Salim Said.

Katibu Tume ya Kurekebisha Sheria ndugu Mussa Kombo Bakari aliwapongeza ZAMECO kwa jitihada wanazozichukuwa kutafuta maendeleo ya tasnia ya habari na kubainisha kuwa mapendekezo waliyowasilisha yamepokelewa na kufanyiwa kazi.

“Tume imekwisha yapeleka mapendekezo hayo katika mamlaka husika na tunatumaini kwamba mapendekezo hayo yatachukuliwa kwa uzito unaostahili ili hatimaye rasimu ya mswaada wa sheria hio ipatikane , alieleza Katibu Mussa.

Nae mkurugenzi wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania, Zanzibar (TAMWA ZNZ), Dkt. Mzuri Issa ametoa shukrani kwa katibu na wafanyakazi wote wa Tume kwa ushirikiano wao katika mchakato huu wa kupata sheria mpya huku akisisitiza umuhimu wa ushirikiano huu katika kuhakikisha upatikanaji wa sheria mpya kwa maslahi ya Zanzibar na wazanzibari wote.

Ni takribani miaka 20 sasa wadau wa maswala ya habari Zanzibar wamekua wakipambania marekebisho ya sheria mbalimbali za habari ikiwemo Sheria ya usajili wa wakala wa habari, magazeti na vitabu No. 5 ya mwaka 1988 iliyofanyiwa marekebisho na sheria No. 8 ya mwaka 1997 na Sheria ya Utangazaji No. 7 ya 1997 ambayo ilifanyiwa marekebisho na Sheria No. 1 ya 2010 , ambapo Oktoba mwaka jana Tume ya kurekebisha sheria Zanzibar ilipokea mapendekezo ya marekebisho ya sheria ya uatangazaji lengo ni kupata sheria huru iliyokua rafiki kwa tasnia ya habari na jamii kwa ujumla.

Imetolewa na:

Communications Department,

Tanzania Media Women's Association- TAMWA Zanzibar,

Comments

Post a Comment

Popular posts from this blog

MWANAMKE AJINYONGA, SABABU WASI WASI - PEMBA

NA, HASSAN MSELLEM - PEMBA PICHA KUTOKA MAKTABA Mwanamke aliyefahamika kwa jina la Raya Darusi Abdallla miaka 48, mkaazi wa Mbuzini Wilaya ya Chake Chake Mkoa wa Kusini Pemba, amefariki Dunia kwa kidaiwa kujinyonga kutokana na Msongo wa mawazo. Tukio Hilo limetokea Novemba 30.2025 saa 11 alfajiri huko Mbuzini Wilaya ya Chake Chake Mkoa wa Kusini Pemba. Omar Salum Ali, ambaye ni shemeji wa marehemu amesema kabla ya marehemu alikuwa na sumbuliwa na Msongo wa mawazo kutokana na kumpoteza kaka yake ambaye alifariki hivi karibuni, kugundulika kuwa ana maradhi ya sukari, mtoto wake wa kiume wa miaka 25, kuwa na ugonjwa akili hali iliyopelekea kupatwa na Msongo wa mawazo na kuamua kujinyonga. Katibu wa Sheha (Katibu wa Mwenyekiti) Shehia ya Mbuzini Yakub Ali Msabah, amesema alipata taarifa za tukio Hilo kutoka kwa Sheha wa Mbuzini kuhusu tukio baada ya kufika eneo la tukio waliukuta mwili wa Mama huyo ukiwa unanin'gia kwenye dari ya Nyumba ambayo alikuwa anaishi zamani. Kutoka tarehe 18 ...

"ZU" YAANDAA MAHAFALI YA 23, DISEMBA 17.2025.

HABARI NA, HASSAN MSELLEM - PEMBA UONGOZI WA CHUO KIKUU CHA ZANZIBAR (ZU) UNAYOFURAHA KUWAALIKA WAHITIMU WOTE WA MWAKA WA MASOMO 2024/2025, PAMOJA NA WAZAZI, WALEZI, NDUGU, JAMAA, MARAFIKI, NA WADAU WOTE WA MAENDELEO YA ELIMU KUSHIRIKI KATIKA MAHAFALI YA 23 YA CHUO KIKUU CHA ZANZIBAR (ZU). MAHAFALI HAYO YANATARAJIWA KUFANYIKA SIKU YA JUMAATANO 17 MWEZI DISEMBA 2025, KATIKA KIWANJA CHA CHUO KIKUU TUNGUU KIBELE KUANZIA SAA MBILI ASUBUHI, AMBAPO MGENI RASMI KATIKA MAHAFALI HAYO ANATARAJIWA KUWA RAISI WA ZANZIBAR NA MWENYEKITI WA BARAZA LA MAPINDUZI DKT. HUSSEIN ALI MWINYI. UONGOZI WA CHUO UNAWASHAURI WAHITIMU WOTE KUKAMILISHA TARATIBU ZOTE IKIWA NI PAMOJA NA KUCHUKUWA MAJOHO KUANZIA SIKU YA ALHAMISI YA TAREHE 11 HADI TAREHE 15.  MAZOEZI YA MAHAFALI YANI REHASAL ITAFANYIKA TAREHE 16. WATU WOTE WANAKARIBISHWA KATIKA MAHAFALI HAYO. CHUO KIKUU CHA ZANZIBAR (ZU) NI CHEM CHEM YA MAADILI NA TAALUMA. KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NA SIMU NAMBARI  0714843480/0718321095/0778777878 AHSANTENI

WATOTO KUJINYONGA ZANZIBAR, UTAFITI WAHITAJIKA.

HABARI NA, HASSAN MSELLEM, PEMBA Picha kutoka mtandaoni Visa vya watoto kujinyonga vimeanza kuwatia khofu na mashaka wazazi na walezi katika Visiwa vya Unguja na Pemba. Mashaka na khofu hiyo imeibuka baada ya matukio mawili mfululizo ya watoto wawili mmoja akiwa umri wa miaka (5) na mwengine (9) kuripotiwa kufariki dunia kwa kujinyonga kati ya tarehe 7 na 9 mwezi huu wa kumi mwaka 2025 kupitia kipindi cha Mawio kinachorushwa na Shirika la Utangazaji Zanzibar ZBC kila siku kuanzia saa 12:40 asubuhi. Katika tukio la kwanza mnamo tarehe 7.10.2025 mwandishi Masanja Mabula aliripoti tukio la Fatma Omar Kidere mwenye umri wa miaka tisa (9) mkaazi wa Mtondoo Jeuri Makaangale Wilaya ya Micheweni Mkao wa Kaskazini Pemba, amekutwa amefariki dunia na mwili wake ukiwa unanin’ginia kwa kutumia mtandio Jirani wa marehemu aliyefahamika kwa jina la Khamis Ali, amesema amepata taarifa za tukio hilo akiwa kazini baada ya kupigiwa simu na mke wake kumpa taarifa za kutokea kwa tukio hilo na kuondoka kazin...